Nani anayefundishwa uongozi na Humphrey Polepole?

Nani anayefundishwa uongozi na Humphrey Polepole?

Joined
Oct 13, 2018
Posts
35
Reaction score
260
Na Thadei Ole Mushi.

Mwenezi wetu wa Chama Mstaafu ameanzisha kipindi chake Cha kufundisha watu uongozi. Kwanza sijajua ANAYEFUNDISHWA hapa ni yupi ni wale waliopo kwenye Madaraka tayari au ni sisi ambao hatuna hayo Madaraka. Naangalia Kazi kubwa ya Polepole anayoifanya Kwa jamii Kwa Sasa ni hii ya kufundisha uongozi. Kuna mambo mawili nayaona kwake.

1. Haamini waliopo madarakani kama wanaifahamu mkubwa kuhusu masuala ya uongozi au

2. Hajui Majukumu ya Mbunge au Hana Kazi za kufanya kama Mbunge za kuwasemea wananchi...... Labda Kwa sababu ni nafasi ya viti maalumu vya Rais Hana Jimbo hivyo ameona wenzeke Wana upungufu kwenye eneo Hilo la uongozi ameamua kuwapa SoMo.

Uongozi haufudishwi Kwa nadharia za Polepole twende kwenye reference ya nchi iliyofanikiwa na Rafiki yetu mkubwa CHINA.

Zhang Weiwei ni Director Katika chuo kikuu cha Fudah University China aliwahi kuelezea ni kwa namna gani china inapata viongozi wake wa kisiasa.

Weiwe anasema viongozi wote wa China lazma wapitie mchakato unaojulikana kama Selection plus Election. Yaani kabla ya kuwa kiongozi china lazma mchakato wa kuwachuja ufanyike kwa kuangalia ulishawahi kufanya nini kabla.

Maeneo muhimu wanayoangalia ni uwezo wako wa kupambana na Umaskini, uwezo wako wa kutengeneza Ajira, uwezo wako wa kuyatunza Mazingira na uwezo wako katika local economic Growth.

Wanawapima toka wakiwa huku chini yaani ngazi za chini kwenye Clip hii anadai viongozi Sita kati ya saba ambao ni Top kabisa katika serikali yao wamepitia mchakato huo na wamepimwa toka wakiwa katika ngazi za Chini za Kiuongozi.

Wao wachina wanacriticize mfumo wa Westerns ambao mtu anatokea from nowhere anakuwa kiongozi. Hapa anatoa mfano kuwa Kama Trump na Bush wangepitia mfumo wa selection na election kamwe wasingelikuwa Viongozi kwa kuwa mfumo huo ungewatema na wasingelifikia kuwa Viongozi.

Suala la kuandaa Viongozi China huchukuwa muda Kuna hatua tano ambazo utapitia katika kipindi fulani Cha muda ukifanyiwa assessment hatua ya kwanza huitwa analysis and proposal, hatua ya Pili huitwa democratic recommendation, hatua ya tatu huitwa appraisal, hatua ya nne huitwa discussion and decision na hatua ya Mwisho ni appointment. Katika hili wachina wao hutumia msemo wao maarufu kuwa "It takes seven years to see if a tree can grow into suitable building materials." Kwa maana ya kuwa huchukua miaka Sana kugundua Kama mti flani unaweza kutumika kwenye ujenzi.

Pamoja na hayo kila mtumishi pale China ambaye ni mtumishi wa umma haingilii dirishani tu Kama hapa kwetu wanavyofanya bali lazima ufanye mtihani wa utumishi wa Umma unaojulikana Kama "KEJU".

Keju ni mtihani ambao kimuondo huwa na maswali 135 multiple choice na maswali Mengine ya kujieleza. Mtihani huo hujumuisha hesabu, Lugha, world affairs na Logic, uwezo wa kusoma, psychological potentials, uwezo wa kutatua matatizo nk. Hapa hata Viongozi wa Umma lazima wafanye mtihani huu, huwezi kuwa kiongozi Kama cv yako haionyeshi kuwa uliwahi kufanya KEJU na ukafaulu.

Mimi nadhani Polepole atusaidie pale kwenye Chuo chetu Cha Siasa Kigamboni. Huku kwenye Ubunge tuwaachie watu wanaotafuta suluhu ya shida za wananchi na wanaoongelea sera na Mipango ya nchi na namna ya kumkwamua Mnyonge.

Ni ukweli ulio dhahiri Polepole haamini aliopo nao kwenye Uongozi kama Wana Uwezo. Huyu ana hangover za Serikali ya Awamu ya Tano.


Ole Mushi.
0712702602

FB_IMG_1631263705530.jpg
 
Una tatizo binafsi na polepole. Malizaneni wenyewe huko msituletee bifu zenu huku.
Ila pia hili suala la kupost alafu chini unaweka namba ya simu ni ushamba na ulimbukeni uliopitiliza, na inaonyesha ni kiasi gani upo very low.
 
ROBOT, POLEPOLE, kwa hesabu zake, anaamini kwa nguvu zote kuwa kama watanzania million kumi wakiambukizwa korona na laki mbili tu wakifa basi ni poa tuu!
... NIJIFUNZE UONGOZI GANI WA BINAADAM KWA ROBOT HILI LILILOWEKEWA SOFTWARE ZA ITIKADI ZA KI'NAZI'?
 
Sasa kosa la Polepole ni nini?
Kasoma masters ya mambo ya uongozi, ana experience "kiasi chake" kwenye uongozi, Sasa wewe nongwa yako juu yake ni nini?, Muache afundishe, kuna watu wananufaika na utirio wake
Huko kwenye masomo yake ya uongozi walimfundisha kuwavimbia wananchi ?
 
Hivi wabunge wa viti maalum kwa teketiya rais ofisi zao huwa wapi?
 
Mushi kuna namna utetezi wako kwa uli choandika unaangukia kuwa chuki binafsi na si ukosoaji wenye lengo la kuleta uchanya.

lile ni darasa huru.mwenye talanta kamili kamwe hawezi kuificha,haizuiliki na haogopi maana kuna msukumo wa ndani.
tunajifunza uzalendo,utaifa , uwajibikaji,uongozi na mengine mengi yafaayo.

H Polepole endelea sana ili tuone makandokando yaliyoingia uongozini kwa kuvunja ukuta au kupitia dirishani.
tunataka tujue MITI IFAAYO KWA UJENZI.
 
Ili umuekewe Polepole na ujengwe na elimu yake, sharti uwe neutral. Ukileta hisia za chama na itikadi utaona kero.vivva H P
 
Tatizo la CCM mijinga kweli. Yaani hawataki kukosolewa wala kufundishwa wanaona wao wanajua kila kitu.

Sioni kosa la Pole pole. That is creativity hakuna aliyelazimishwa kupewa elimu ya uongozi wala hakuna sehemu Polepole ameandika kuwa hawaamini viongozi walioko madarakani. Labda Kama unataka kutengeneza bifu kati ya pole pole na viongozi walioko madarakani.

Kwani mtu kutoa elimu ya uongozi mpaka awe chuo fulani?

Ina maana wewe huwezi kuelimisha ndugu zako au wananchi wako mpaka waende Shule?
Acha akili finyu mkuu elimu ni popote.
 
Uko biased kinyama mkuu. Kazi ya mbunge ni kutetea taifa zima pia sio kuongelea ya jimbo tu.
 
Achana na huyo chawa wa mwendazake, anafundisha uongozi yeye anamuongoza nani?
 
Too judgmental criticism based on your perception toward him.
Una tatizo binafsi na polepole. Malizaneni wenyewe huko msituletee bifu zenu huku.
Ila pia hili suala la kupost alafu chini unaweka namba ya simu ni ushamba na ulimbukeni uliopitiliza, na inaonyesha ni kiasi gani upo very low.
Sasa kosa la Polepole ni nini?
Kasoma masters ya mambo ya uongozi, ana experience "kiasi chake" kwenye uongozi, Sasa wewe nongwa yako juu yake ni nini?, Muache afundishe, kuna watu wananufaika na utirio wake
Mushi kuna namna utetezi wako kwa uli choandika unaangukia kuwa chuki binafsi na si ukosoaji wenye lengo la kuleta uchanya.
lile ni darasa huru.mwenye talanta kamili kamwe hawezi kuificha,haizuiliki na haogopi maana kuna msukumo wa ndani.
tunajifunza uzalendo,utaifa , uwajibikaji,uongozi na mengine mengi yafaayo.
H Polepole endelea sana ili tuone makandokando yaliyoingia uongozini kwa kuvunja ukuta au kupitia dirishani.
tunataka tujue MITI IFAAYO KWA UJENZI.
Mimi sijaona chuki ya Ole Mushi dhidi ya Polepole...

Mimi sijaona akimhukumu Polepole (he's not judgemental) Mwanga Mkali

Kwa msomaji makini wa hoja ya Ole Mushi, atagundua kuwa andiko lake lote limlenga kumpa changamoto ya kuboresha zaidi shule yake ya uongozi..

Ndiyo maana katumia reference ya China na Prof. Zhang WeiWei namna wanavyopata viongozi wao...

Ole Thadei Mushi, amesema hili akitambua kuwa Humphrey Polepole ni mwana CCM aliyewahi kushika nafasi nyeti chamani na bado anazo zingine na pia ni mbunge na kwa hiyo anaweza kulichukua wazo hili na kulipeleka kwa wenzake...

Mimi sijaona kosa la Mwandishi hata astahili kushambuliwa kwa kiasi hiki...
 
Wewe anzisha kozi yako tufundishe huo uongozi kwa kichina. Tutakufwatilia.

Polepole anatumia muda wake vizuri kutushirikisha anachojua wether ni western or whatever pamoja na majukumu yake amabayo naona anakwenda nayo vizuri.

Nadhani pia anachofundisha polepole SIO KWA AJILI YA KILA MTU.

Mimi nafundishwa naye uongozi na wewe pia una nafasi nzuri ya kunifundisha maana huwa napenda kujifunza toka kwa wengi.
 
Back
Top Bottom