Nani anapanga vipaumbele vya taifa letu?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
21,440
40,534
Unapoangalia Moto unavyoteketeza Mali za watu binanfsi na za umma kwa kukosekana kwa Magari ya zimamoto, unajiuliza ni kwa nini tulitumia fedha nyingi sana kununulia Magari ya maji ya kuwasha badala ya Magari ya Zimamoto ambayo ni ya muhimu zaidi kwenye maisha ya kila siku ya watanzania.

Inapokuwa Mgonjwa (Baraka Elias Mashauri) inashindikana kutibiwa Kwenye Hospitali ya Taifa Mhimbili kwa kukosekana vifaa vya kusaidia kupatiwa tiba, unajiuliza ni kwa nini fedha vya kununulia vifaa hivyo inakosekana ila serikali inazo fedha za kununulia Mashangingi.

Ukiangalia kuanzia utungaji wa sheria, mikakati ya kimaendeleo, mipango ya kiuchumi, na mambo mengine mengi ambayo mwisho wa siku taifa linapata hasara, wali la msingi ni nani hasa anaweka vipaumbele vya taifa letu? Inakuwaje tunatangatanga kama wana Israel walivyokuwa wanatangatanga Jangwani kwa miaka 40 mahali walikoweza kufika kwa siku arobaini tu?
 
swali bado halijajibiwa
Leo wanaleta mfumo wa GPA kesho wanarudisha mambo ya "Division". wanafuta michezo mashuleni mara wanaibuka na kusema bila michezo Mashuleni hakuna kupatikana kwa timu bora za taifa.

Hawa hawa walipigana kufa na kupona ili "mwekezaji" Acacia apate na achimbe madini lakini leo wanawaita hao wawekazaji wao ni wezi. Hakuna mwendelezo wa jambo lolote linalofika mwisho.
 
Kwasasa tunataka kuhakikisha kila mtz anapanda ndege,

Tutahakikisha barabara zote nchini zinakuwa za kiwango cha lami watanzania wasipate shida

Ndio bipaumbele vyetu kwa sasa
 
Leo wanaleta mfumo wa GPA kesho wanarudisha mambo ya "Division". wanafuta michezo mashuleni mara wanaibuka na kusema bila michezo Mashuleni hakuna kupatikana kwa timu bora za taifa.

Hawa hawa walipigana kufa na kupona ili "mwekezaji" Acacia apate na achimbe madini lakini leo wanawaita hao wawekazaji wao ni wezi. Hakuna mwendelezo wa jambo lolote linalofika mwisho.
Mkuu, hii ni nchi ya majaribio. Kila mmoja anakuja na kuujaribu mfumo wake, ukishindwa anarudi kwenye wa zamani... akija mwingine hivyohivyo hadi Yesu atarudi bado tunazunguka palepale...
 
Inachosha sana na tunaopata hasara ni sisi wananchi tunaolipishwa kodi!
 
Msukuma mkokoteni a.k.a mataputapu
Hayo ya zima moto hayana kipaumbele sana. Lengo letu wanaccm ni kutumia nguvu na pesa nyingi sana kuondoa upinzani.
Wakisikia raia wanaandamana watakuja na gari za washa washa hata 200 lkn ikitokea janga la moto
teh teh teh kila abiria achunge mzigo wake
 
Mwizi wewe!
Kama hutaki kulipa kodi hama nchi;omba uraia kwa wazungu!
Huyu jamaa na mla pesa za watu waliokufa (rambi rambi), kafuta ajira na kala increment bila kusahau fao la kujitoa nani ni mwizi?
Chama cha majambazi kujitoa ufahamu.
Leo maandamano yakitokea polisiccm watakuja na gari za kuwasha washa hata 200 lkn kweny zima moto wanakuja mikono mitupu.
Mpe pole mataputapu
 
Unapoangalia Moto unavyoteketeza Mali za watu binanfsi na za umma kwa kukosekana kwa Magari ya zimamoto, unajiuliza ni kwa nini tulitumia fedha nyingi sana kununulia Magari ya maji ya kuwasha badala ya Magari ya Zimamoto ambayo ni ya muhimu zaidi kwenye maisha ya kila siku ya watanzania.

Inapokuwa Mgonjwa (Baraka Elias Mashauri) inashindikana kutibiwa Kwenye Hospitali ya Taifa Mhimbili kwa kukosekana vifaa vya kusaidia kupatiwa tiba, unajiuliza ni kwa nini fedha vya kununulia vifaa hivyo inakosekana ila serikali inazo fedha za kununulia Mashangingi.

Ukiangalia kuanzia utungaji wa sheria, mikakati ya kimaendeleo, mipango ya kiuchumi, na mambo mengine mengi ambayo mwisho wa siku taifa linapata hasara, wali la msingi ni nani hasa anaweka vipaumbele vya taifa letu? Inakuwaje tunatangatanga kama wana Israel walivyokuwa wanatangatanga Jangwani kwa miaka 40 mahali walikoweza kufika kwa siku arobaini tu?
Jamani Watanzania wenzangu mbona sisi tuna hii hulka ya kutegemea mtu mwengine (serikali au mfadhili) kutufanyia hata kile kilichopo ndani ya uwezo wetu?

Upinzani unaweza kutusaidia sana kwa kufanya vitu vya kuigwa nchi nzima.

Mifano:
1. Zimamoto
Kwa nini kwenye majimbo na mitaa ilioko chini ya upinzani wasiunde vikosi vya zimamoto wa kujitolea (hawalipwi) wawe zimamoto wa mtaa, kijiji, au mji.

Wabunge, madiwani, na viongozi wengine wa sehemu hizi wanaweza kutoa posho zao, sehemu ya mishahara yao, n.k. kuchangia kunua magari na vifaa vingine vya zimamoto. Hapa pia tunaweza kuwaomba wafanyabiashara wa sehemu hiyo kuchangia.

Hii italifanya jukumu la zimamoto kuwa la jamii ya hilo eneo na sio jukumu la serikali.

2. Vifaa Hospitalini
Hapa pia viongozi wa upinzani wanaweza kutoa mfano. Katika majimbo yao wanaweza kuanzisha mfuko utakaochangiwa (kwa hiyari) na watu wote pamoja na biashara za eneo hilo ili kuweka vifaa muhimu katika mahospitali yao.

Mambo makubwa kama majengo, mashine za bei mbaya, n.k. vinaweza kutolewa na serikali. Lakini kuna vifaa vingi muhimu vinavyoweza kununuliwa kwa kutumia huu mfuko.

Tusiisubiri serikali kwa kila kitu jamani. Badala ya kuilaumu serikali kuwa haifanyi hiki au kile, mambo mengine tunaweza kufanya wenyewe kama tuna uongozi mzuri.

Hapa upinzani unaweza kuonyesha mfano wa kuigwa. Mnataka kupata kaulimbiu wakati wa uchaguzi mkuu, fanyeni haya.

Vipaumbele tunaviweka sisi wananchi ambao ndio tunaofaidika na hayo mabadiliko na sio serikali. Tukionyesha ni kipi cha muhimu kwetu, serikali itafuata. Tunahitaji mtu atuongoze. Hii ni kazi muhimu kwa upinzani.

Upinzani, show your leadership please na sio kupinga, kulaumu au kukosoa serikali tu.
 
Maandishi marefu upuuzi tu

Mwananchi ananini LA kufanya?

Japokuwa yy ndo mwakilishi km mnqvyodai lkn kwenye maamuzi hayupo,
 
Back
Top Bottom