Fumadilu Kalimanzila
JF-Expert Member
- Dec 10, 2016
- 1,719
- 5,368
Katika miaka na siku za hivi karibuni Taifa letu limekumbwa na matukio ya aibu ya utekaji, mauaji ya kikatili , ulawiti na matendo mengine ya hovyo sana!
Na katika matukio mengi ya hovyo yanayofanyika Vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vimenyooshewa sana vidole!
Katika udadisi wangu nimegundua mambo mengi lakini nitakayoyaelezea hapa ni ya msingi.
Awali ya yote niweke wazi kwamba mimi ni mwana CCM (declare interest) ambaye sipendezwi kabisa na namna tunavyo manage mambo hususani siasa (politics) katika Nchi yetu.
Elimu duni na Rushwa zimepelekea katika miaka ya hivi karibuni kuajiriwa baadhi ya watu wa hovyo na wasiokuwa na maadili na uelewa mpana wa mambo na Dunia inavyo operate katika vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama!
Ukiingia katika mikono ya watu hao wa hovyo ni Bora ukutane na shetani ujue moja!!!
Tukio la wale vijana waliombaka na kumlawiti yule Binti wa Yombo
Taifa hili ni kubwa na ni muhimu kuliko CCM au Chama chochote kingine cha siasa! HAWAJUI!
Mjinga mmoja akawa anadai eti imekuwaje Marehemu Mohamedi Ali Kibao ili hali ni mstaafu wa Jeshi akafanya kazi au akawa Mwana CHADEMA!
Eti pengine kuna siri kavujisha na hata huko kwenye mtandao wa X ( zamani Twitter) Kuna wajinga wanamsontea Mchungaji Peter Msigwa kuwa pengine ndiye "kamchoma " Mzee Kibao kwa " wajinga" wanaotuhumiwa kumuua.
Sasa unajiuliza kwa watu wenye akili, hivi Kuna siri za Taifa hili ambazo CHADEMA wakizijua ni tatizo na CCM wakizijua hakuna tatizo! HUU NI UJINGA WA KIWANGO CHA SGR!!
Mimi sioni tatizo lolote kwa Mstaafu yeyote kufanya siasa CHADEMA, CCM au ktk Chama kingine cha siasa , cha msingi ni uzalendo wake kwa Taifa lake.
Mzee Mohamed Ali Kibao , mzalendo wa kweli na mpiganaji wa kweli ambaye tunaambiwa amepigana hadi vita ya Kagera dhidi ya Nduli Idd Amini ukute ameuawa na mazumbukuku, , machawa na wajinga wajinga fulani ambao pengine wameajiriwa mahali fulani kwa kujuana na RUSHWA tu! Kama ndivyo inauma sana!!!
Marekani leo katika mbio za Urais Tim Walz ambaye ni mstaafu wa Jeshi la Marekani ni mgombea mwenza wa Kamala Harris kwa tiketi ya Democrats na JD Vance ambaye pia ni mstaafu wa Jeshi la Marekani ni mgombea mwenza wa Donald Trump kwa Tiketi ya Republican!
Kinachowaunganisha ni Maslahi ya Taifa lao basi! America First!
Huwezi kukuta operation za kijinga jinga kama alizofanya Kamanda Awadhi Juma hivi karibu dhidi ya Wana CHADEMA na viongozi wao!!
Matumizi wa vifaa vya Teknolojia na Utandawaji vimefanya kama Taifa tumekuwa na watu wa hovyo , wakatili kupindukia na wasiokuwa na maadili na utamaduni wa Taifa letu!
Waovu hawa wamejifunza tabia za ushoga kupitia mitandao na utandawazi na hawaheshimu kabisa haki za binadamu na sasa Wana kiu ya kuingilia Kila mtu na kiumbe chochote kinachoweza maliza haja zao!
Ebu fikiria walio muua Mzee Mohamed Ali Kibao ni watu/vijana katika Taifa lililoasisiwa na Hayati Julius Kambarage Nyerere!!
Kweli siku HAZIGANDI!!!
Viongozi wenye dhamana ya kusimamia vyombo vya Ulinzi na Usalama wanapaswa kufanya upya sensorship na kujua aina ya watu wanaowaongoza ,pengine kuna mamluki katika vyombo vyetu maana matukio mengine hayana dalili za Utanzania.
Ni ukatili wa kutisha sana!!
Pia elimu ya uraia na haki za binadamu itolewe Kila mara kuwajengea uweledi ktk shughuli zao za ulinzi na usalama.
Wakuu wa Vyombo vyetu hivi wengine tunawajua ni watu wenye uweledi, maadili mazuri na wacha Mungu kiasi ambacho ukianza kuhisi kuwa uovu huu unaweza kufanyika chini ya Uongozi wao? Ni ngumu sana kuamini!