Nani anaongoza nchi?

Nani anaongoza nchi?

Ashasembeko

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2017
Posts
226
Reaction score
914
Hili ni swali kila mtanzania inabidi ajiulize.

Unakuwa na Rais anasema polisi waache kuonea watu, hapo hapo anasema ameruhusu mikutano ya ndani ila haya maagizo yake yanakaidiwa na watu ambao inabidi wamtii kama Amri Jeshi Mkuu.

Tunaona polisi wakiendelea kuzuia wanasiasa kufanya mikutano yao na kuwakamata hovyo hata wakiwa makanisani.

Leo Mbatia amesema walipozuiwa kufanya mikutano yao ya ndani, aliwauliza polisi nani amewatuma, akaambiwa kuwa ni maagizo kutoka juu.

Mbatia akasema akawapigia simu IGP na Simbachawene kuwauliza kuhusu nani kaagiza, wakamwambia kuwa hilo sio sawa na polisi wamekosea na hayo maagizo hayakutoka kwao.

Sasa yanayoka wapi? Kwa Rais? Rais ambae alishasema jukwaani kuwa waruhusiwe kufanya mikutano ya ndani? Je Rais ni mnafki?

Kama Rais sio mnfafki kuna kikundi cha watu kinachokaidi maagizo yake. Ninkikundi gani hili tusichokijua. Tundu Lissu na Zitto Kabwe walishadokeza mara kadhaa kuwa kuna watu kwenye "security na political establishment" hawataki mabadiliko, ni kina nani hawa wenye nguvu zaidi ya Rais?

Mi nilisikia sehemu kuwa Samia "sio Rais" na yupo pale kwa maonyesho tu, kufanya uzinduzi, kutoa hotuba nk, ila kuna watu nyuma ndio wanafanya maamuzi. Kama ni kweli ni kina nani hawa?

Hawa "watu" naskia wameenda mbali na kumpunguzia Samia mawasiliano na watu waliomuingiza madarakani. Rais sa hizi hana uhusiano na mawasiliano wa karibu na MaRais wastaafu na baadhi ya viongozi wa upinzani waliokuwa wakimshauri katika miezi ya mwanzoni.

Samia asikubaki kupelekeshwa, atambue kuwa yeye ni Rais na mamlaka yote ni yake. Kama alivyosema Zitto kwenye mahojiano na Star TV juzi, "hakuna Rais nusu".

Akilitambua hili, ataanza fanya maamuzi anayoyaamini yy sio yale wengine qanaotaka ayafanye. At the end of the day sisi wananchi tunajua ni YEYE ndio anasimamia ukandamizwaji huu sio watu hao nyuma. She needs fo protect her image. Kama anaona yamemshinda ajiuzulu.

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app
 
JK
 
Nani JK au Magu? Wote hawakuwa na maajabu... hakumbukwi mtu, tunataka kiongozi anayeheshimu katiba na taasisi zetu.

Sent from my SM-G975U using JamiiForums mobile app

354506.jpg
 
Acheni Story za vijiweni, raisi wa Tanzania ni rank ya mwisho ya uongozi katika taifa letu,

Zaidi ya katiba hakuna mtu anayeweza kumlazimisha kufanya asichokitaka,

"Nasikia nasikia" umesikia kutoka kwa nani?
 
Kwani jeshi la polisi limesahau majukumu yake na badala yake linategemea maagizo kutoka kwa wanasiasa?

Ninavyofahamu jeshi la polisi lina wajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zao na linalazimika kufanya response na initiations mahala ambapo wanaona usalama wa raia na mali zao upo kwenye mashaka.

Kuhojiwa na polisi ni jambo la kawaida ili wajiridhishe kama hakuna nia mbaya inayohatarisha usalama wa raia. Hivyo wanapoona sintofahamu ama kwa kujulishwa na raia au kwa intelejensia yao lazima wafanye response. Mojawapo ni mahojiano na walengwa.

Kumchukua raia yeyote na kumhoji ni sehemu ya majukumu yao na sio lazima watumwe na mwanasiasa. Ni jambo la kawaida kuitwa au kushikiliwa na polisi kwa mahojiano ili wapate taarifa unazofahamu kuhusiana na shughuli za kiraia. Tuache negativity na jeshi letu la polisi.

ANGALIZO: Binafsi naona polisi wanatimiza majukumu yao. Kama kutakuwa na ukiukwaji wa haki za raia au uonevu mara baada ya kushikiliwa kwa mahojiano hapo polisi watakuwa wamekiuka miiko na kiapo cha kazi yao na hawana weledi. Ila kama ni mahojiano tu haina shida, maana taarifa wanazitoa kwetu wananchi kupitia mahojiano.
 
Kuna chuo kimoja Cha polisi , CCP nchini Tanzania ,picha zinarushwa nje ya nchi ,zikionyesha askari waliokwenda kozi siku za karibuni kulowekwa mwili mzima kwenye matope ndio usajiliwe kujiunga na kozi. IGP Hilo umeambiwa?
 
This is soft generation...Jitihada zinahitajika kuliokoa taifa.
 
Kuna chuo kimoja Cha polisi , CCP nchini Tanzania ,picha zinarushwa nje ya nchi ,zikionyesha askari waliokwenda kozi siku za karibuni kulowekwa mwili mzima kwenye matope ndio usajiliwe kujiunga na kozi. IGP Hilo umeambiwa?
Hk n ktu cha kawaida sana kwny majeshi yaaan n kama kumpa uji mtoto
 
Kwa sasa kinachofanyika ni kwamba kila mwenye Amri juu ya Idara yake hanaongea yeye tu bila kujali masilai mapana ya Taifa
Mfano
mdogo ni huyo IGP sirro hanatowa kauli zisizo na mashiko kama kiongozi mwenye mamlaka
Mama yupo fair sana ila kuna kikundi cha wendawazimu lengo lao ni kumuharbia kabsa utawala wake

Sent from my SM-J500H using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom