Nani anamjua Mgombea huyu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani anamjua Mgombea huyu?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kite Munganga, Oct 26, 2010.

 1. Kite Munganga

  Kite Munganga JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Nov 19, 2006
  Messages: 1,298
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 145
  Source: Gazeti la...Ukweli na uwazi

  Na Haruni Sanchawa
  KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Saidi Mwema na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Lewis Makame wamepelekewa picha za udhalilishaji unaodaiwa kufanywa na mgombea ubunge mmoja wa jimbo lililopo nyanda za juu kusini.

  Uchunguzi wa gazeti hili umebaini kuwa picha hizo zimepelekwa kwa viongozi hao na taasisi moja isiyo ya kiserikali iitwayo The Registered Trustees of the Social Political Development Trust (AFORD) na zinaonesha ‘mchezo mbaya’ wa ulawiti aliofanyiwa kijana mmoja mwenye asili ya kiasia anayeishi katika jimbo hilo la uchaguzi.

  Kwa mujibu wa nyaraka zilizopelekwa kwa vigogo hao wa serikali (nakala tunazo), kijana huyo (jina tunalihifadhi) anadaiwa alifanyiwa unyama huo na kundi la watu kwa zamu Desemba 12, 2008 kwenye nyumba ya mgombea ubunge huyo.

  “(jina lake) alijitahidi kuona sheria inachukua mkondo wake, (mtuhumiwa) alianza kumtishia kumuua mpaka kufikia uamuzi wa kujificha kwa kuhama mji na kwenda kuishi Mbeya ndiko alikokimbilia,” imesema sehemu ya barua hiyo.

  Uchunguzi wa taasisi hiyo unadai uligundua kuwa jitihada za mlalamikaji zilizimwa na mtuhumiwa kwa kushirikiana na watendaji wakuu wa dola ambao walihakikisha madai hayo hayafiki popote, na waraka huo unadai kuwa vigogo hao kwa sasa wamehamishiwa makao makuu ya Jeshi la polisi nchini.

  Waraka huo unaongeza kusema kuwa mtuhumiwa alizisambaza picha za tukio kwa marafiki wa mlalamikaji na taasisi hiyo imemtaka IGP Mwema kuchunguza tukio hilo na watendaji waliotajwa kushiriki katika kufanikisha tukio hilo lisichukuliwe hatua za kisheria.

  Aidha, taasisi hiyo imemuandikia barua Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Makame ikimtaarifu juu ya madai hayo na kumtaka iliondoe jina la mtuhumiwa katika orodha ya wagombea kwa madai kuwa amekosa sifa za kuwa mgombea.

  Waraka huo umedai licha ya kashfa hiyo, mgombea ubunge huyo anadaiwa kumtia mimba mwanafunzi wa shule moja katika jimbo leke (jina tunalihifadhi) wa kidato cha tatu na akaahidi kumuoa lakini sasa amemtelekeza.

  Taasisi hiyo imedai katika barua hiyo yenye kumbukumbu namba AFORD /20/10/V/2010 ya Oktoba 20, 2010 kuwa kashfa hiyo imefikishwa ngazi ya juu ya chama cha mgombea huyo kupitia barua ya kwenda kwa katibu mkuu wao yenye kumbukumbu namba Aford/1/10/2010 ya Oktoba 5, mwaka huu na kusainiwa na Mwenyekiti wa AFORD, Senator Julius Miselya.

  Gazeti hili lilimtafuta Senator Miselya na kumuuliza kama kweli amendika barua hizo ambapo alithibitisha kuwa amefanya hivyo.

  “Ukweli ni kwamba huyu bwana hafai kuwa kiongozi, nimepeleka barua kwa IGP Mwema, Jaji Makame na katibu mkuu wa chama chake, hana sifa za uongozi na inafaa sheria ichukue mkondo wake,” alisema Miselya.
   
 2. TUKUTUKU

  TUKUTUKU JF-Expert Member

  #2
  Oct 26, 2010
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 11,852
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Duh!hii kali!sheria na taratibu za uchaguzi zichukue mkondo wake!
   
Loading...