Nani anamfadhili mtu huyu?

BetaPyne

New Member
May 4, 2006
3
9
Jana (Juni mosi, 2020) majira ya saa 8 Mchana, gari aina ta Prado ya rangi ya kijivu T304 DHK likiwa na watu 6 ndani yake lilizuiliwa kwenye ‘Barrier’ ya mjini Lindi karibu na Shule ya Sekondari ya Lindi baada ya Polisi kupata ripoti kuwa gari hilo lilikuwa linakwenda kasi na kukataa kusimama kwenye vizuizi vyote vya Traffic.

Gari hilo lilizuiwa na Lorry lililokuwa na askari polisi wenye silaha. Wakaambiwa washuke wakiwa na mikono juu.

Wakashuka watu 6 wakachangamshwa kidogo kipolisi, wakarushwa kichura na kupelekwa pembeni. Watu hawa walikutwa na bastola 3. Wakajitambulisha wakiwa na Kiongozi wao ambaye ni ‘Mwanaharakati Huru’ akifuatana na vijana 4 kutoka idara nyeti, pamoja na dereva wao.

‪Walipoulizwa walikuwa wanakwenda wapi, waliwaambia maafisa wa Polisi kuwa walikuwa wanakwenda Ruangwa kwa Waziri Mkuu. Walipoambiwa kuwa mbona hayupo, wakadai wana kazi wanakwenda kufanya.‬

Nzi wetu aimefuatilia nyendo zao na kubaini hata ofisi ya PM haina taarifa zao!

Swali langu: Mwanaharakati huyu huru anatumiwa na nani? Nani anamlea? Tunalipeka wapi Taifa?
 
Isije ikawa kama sekeseke la wale mapolice wa USA walipomkamata FBI na kumfunga pingu....palikiwa pataam apo...
 
Kama alikua na vijana wa idara basi ni wazi anafadhiliwa na idara. Idara ina mwajiri mmoja tu, ambaye ni mkurugenzi mkuu wa idara.

Kama hana baraka zao wangesha mzima kitambo sana, hata kama angekua na baraka za mkuu wa nchi.
 
Back
Top Bottom