Wadau nani anaifahamu vizuri hii website ya kuuza na kununua kupitia mtandao nimepata bidhaa nimekuja nipate kujua zaidi kama kuna mtu amewahi kuitumia!!
Hua nanunua vitu vingi sana kupitia wao, wako poa sana... najua wasi wasi wako n pesa isije potea, Ukisha toa order yako utalipa baada ya kuipokea, na kama hujaridhika nayo unabadilishiwa.. shipping fee n 3,000... lile n kama soko, linakutansha mnunuz na muuzaji
Kaymu ni soko namba moja la mtaondaoni hapa Tanzania.
Kaymu inakuunganisha wewe mnunuzi na muuzaji, hauhitaji kwenda kuzunguka madukani kutafuta bidhaa zote unazipata ndani ya Kaymu. Kwanzia electronics, simu za mkononi, vifaa vua majumbani, nguo na viatu kwa wa wadada, wakaka na watoto zote unapata.
Malipo unaweza kufanya kupitia Tigo pesa, Mpesa au Airtel Money kwa wateja wa mikoani, ila kwa wateja wetu wa Dar unalipia pale unapopata mzigo.
Gharama za kukuletea mzigo zitaambatanishwa na bei ya bidhaa. Kwa Dar ni Tsh 3,000 na mikoani kama Pwani, Arusha, Morogoro, Tanga na Kilimanjaro ni Tsh 8,000 na kwa mikoa ya mbali kama Mbeya n.k bei ya usafirishaji ni Tsh 12,000.
Bidhaa huchukua siku 3-5 kwa wateja wa Dar es Salaam kupata mzigo. Na huchukua siku 5-7 kwa wale wa mikoani.
Kaymu pia ina page zao Facebook, Instagram na Twitter wacheki kupitia @KaymuTanzania/ KaymuTZ.
Pia kwa maelekezo zaidi waweza kuwapigia bure kwenye namba 0800710024 au tembelea website yao Online Shopping | Electronics, Laptops, Mobile Phones | Kaymu Tanzania .
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.