Ndugu wanajamii kheri ya sikukuu ya Idd-El Haj
Napenda kuungana na wananchi wengine wanaomwona mh. Lowassa ni mtetesi wa Wanyonge na kuwaelimisha wanaomtupia maneno machafu bila ushahidi na bila kueleza hao washirika wao wanaowaleta huku wamewafanyia nini watanzania? Kitu gani wamekifanya kinachopimika?
Pamoja na mengi mema aliyoyafanya mh. Lowassa, leo nitakumbushia mambo mawili makubwa ameyasimamia kadiri ya uwezo wake katika nafasi finyu aliyo nayo serikalini. Mnyonge mnyongeni, hali yake mpeni.
1. Shule za kata.
2. VICOBA
Nitajaribu kutoa maelezo katika hayo mawili kati ya mengi aliyoyafanya.
1. Mh. Lowassa aliweza kusimamia ujenz wa shule za sekondari katika kila kata, jambo ambalo limefanikiwa kwa asilimia zaidi ya mia pamoja na changamoto alizopata katika ku~implement wazo lake lakini shule za kata ZIMEOKOA WANYONGE WENGI.
2. VICOBA-hii ni benki ya vikundi vidogovidogo vinavyojihusisha na ujasiriamali. Mh. Lowassa katika uhamasishaji wake kuviunga mkono vicoba, kumemfanya apendwe na wanachama wa vikundi hivyo kwa namna anavyojitahidi kuvisaidia ili viweze kusongambele. Ikumbukwe zaidi ya asilimia 95 ya wanachama hao ni wale wenye kipato duni lakini wapo ambao maisha yao yamechanua kupitia vicoba. Binafsi alitushauri tuanzishe vicoba na leo hii hata mwaka haujaisha ila tupo mbali tofauti na maisha yetu ya awali na hajatupa hata shilingi moja bali ni wazo tu alitupa. HUYU NI MKOMBOZI WA WANYONGE.
Wafuasi wa SITTA, MEMBE, PINDA, JANUARY, WASSIRA, n.k, tuambieni hawa watu mnaojaribu kuwapenyeza kwetu kwa Nguvu kubwa hasa kutengeneza mikashifa, LEO TUSEME MAZURI, MAANA HAKUNA MWANADAMU ALIYEKAMILIKA. NAOMBA TUSEME VITU VINAVYOPIMIKA, VINAVYOONEKANA, VILIVYOFANYA NA HAO VIONGOZI AMBAO WAPO KATIKA NAFASI ZA JUU KABISA.
Hakika raisi anaetufaa ni yule anaejua mahitaji ya wananchi ambae ni mh. Lowassa only. Nawasilisha.