Nani anafaa kuwa Mwenyekiti badala ya Mbowe?

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Sep 30, 2011
18,300
33,917
Kuna shinikizo linaendelea ndani na nje ya CHADEMA kwamba pamoja na mazuri kadhaa aliyoyafanya Freeman Aikaeli Mbowe kama Mwenyekiti wa CHADEMA, umefika wakati sasa wa Mbowe kumwachia Mwanachama mwingine aendeshe chama.

Lakini pamoja na shinikizo hizo bado hakuna jina moja linaloonekana kuungwa mkono na wanachadema wengi kwamba mtu huyo anafaa kuendesha chama. Kuelekea jaribio la kumuua, Tundu Lissu alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wanatajwa sana kufaa kumrithi Mbowe.

Lakini siku za hivi Karibuni limeibuka kundi kubwa la watu wanaodai kwamba Lissu hana sifa za kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa badala yake aendelee kuwa kwenye nafasi yake ya Mwanasheria wa chama. Jee ni nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa badala ya Mbowe?

KUMBUKA: CCM wanataka Mbowe aondoke wakiwa na Malengo ya kuibomoa CHADEMA, wakati CHADEMA wanataka Mbowe aondoke ili wapate fikra mpya katika kuendesha chama chao.
 
Bado hatujaanza kufikiria hilo, ukifika wakati tutawajulisha
 
CRDB leo wanamlilia kimei abaki unadhani ni wajinga?

Ni kweli mbowe anaweza kuwa na mapungufu yake lakini still ni mtu sahihi kukiongoza chama mbadala wake mi bado simuoni!
Na akifa ina maana CRDB nayo itakufa?hii ndio shida ya mijitu minafiki anapotajwa mungu wao hukimbilia kutoa mifano ya hovyo takataka,CRDB ni taasisi kuna watu wengi tu wanaweza kufanya kazi ya Kimei,vivyo hivyo na Mbowe,hivyo tu ni Chadema ,je akipewa nchi si atafia madarakani.
 
mungu wa nani tena mkuu?

mi nimetoa maoni yangu km mtanzania na maneno yangu sio sheria wala kanuni!....
 
Kuna shinikizo linaendelea ndani na nje ya CHADEMA kwamba pamoja na mazuri kadhaa aliyoyafanya Freeman Aikaeli Mbowe kama Mwenyekiti wa CHADEMA, umefika wakati sasa wa Mbowe kumwachia Mwanachama mwingine aendeshe chama.

Lakini pamoja na shinikizo hizo bado hakuna jina moja linaloonekana kuungwa mkono na wanachadema wengi kwamba mtu huyo anafaa kuendesha chama. Kuelekea jaribio la kumuua, Tundu Lissu alikuwa ni mmoja wa watu waliokuwa wanatajwa sana kufaa kumrithi Mbowe.

Lakini siku za hivi Karibuni limeibuka kundi kubwa la watu wanaodai kwamba Lissu hana sifa za kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa badala yake aendelee kuwa kwenye nafasi yake ya Mwanasheria wa chama. Jee ni nani anafaa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa badala ya Mbowe?

KUMBUKA: CCM wanataka Mbowe aondoke wakiwa na Malengo ya kuibomoa CHADEMA, wakati CHADEMA wanataka Mbowe aondoke ili wapate fikra mpya katika kuendesha chama chao.
CCM KWA KUCOPY HAMJAMBO, HUU UZI UMEUANZISHA BAADA YA KUONA UZI ULIOANZISHWA UKIULIZIA KUWA NI NANA WA KUMRIDHI MAKONDA DAR
 
Wewe unajua misimamo yangu kuhusu CHADEMA? Halafu huo uzi wako wa kumrithi Makonda sijauona kwa ivo sijausoma pia.

Jifunze matumizi ya herufi KUBWA kwenye uandishi.
 
Kuna kuchanganya mambo kwa sasa ndani ya cdm linapokuja suala la Mbowe kutoka kwenye uenyekiti. Kuna sisi tunaotaka atoke kwa maana ya kukuza demokrasia kwani ni vyema kiongozi wa kuchaguliwa awe na ukomo wangalau 10yrs maximum. Na kuna shinikizo toka ccm na wengoneo wakitaka atoke kwani ni kikwazo kwao na matarajio yao.

Hali hizo mbili zinaoneka kuwa na nguvu kwenye kumpata mrithi wa Mbowe. Mimi kama mimi siamini kwenye uimara wa mtu bali uimara wa taasisi. Sasa iwapo hoja ya Mbowe kukaa madarakani kwa sababu eti cdm bado inamuhitaji ni hoja ya fedheha. Chama kina 20yrs+, kama hakijawa imara muda wote huo ni lini kitakuwa imara kiasi cha kupata mwenyekiti mpya? Vinginevyo watetezi wa hoja hii watuambie bado cdm ni chama dhaifu ndio maana walifikia tendo la aibu la kumpa Lowassa nafasi ya kugombea urais.

Hoja ya kwamba ccm wanataka Mbowe atoke ili iwe rahisi kuweka kibaraka huenda ni kweli, lakini unapokuwa na mshindani wako unategemea asikufanyie hila? Hata hivyo naona hoja hii pia inatumiwa na wanacdm wanaomwamini Mbowe kama kinga ya yeye kuendelea kuwa mwenyekiti. Sababu hii inapopewa nguvu na hata wanachadema wenyewe napata shaka sana. Halafu ni wakati sasa wa wanachama wa cdm kuhakikisha kifungu cha ukomo wa uenyekiti kinakuwepo. Kinyume na hapo hakuna chama cha demokrasia wala nini bali ni utapeli kama utapeli mwingine.
 
Chama kina 20yrs+, kama hakijawa imara muda wote huo ni lini kitakuwa imara kiasi cha kupata mwenyekiti mpya? Vinginevyo watetezi wa hoja hii watuambie bado cdm ni chama dhaifu ndio maana walifikia tendo la aibu la kumpa Lowassa nafasi ya kugombea urais.
Ndiyo maana kwenye ile hoja yangu nyingine nilisema tatizo ni Katiba ya CHADEMA ya Mwaka 2006.

Ili taasisi iwe imara huwa inalindwa na Katiba yake na si uimara wala utashi wa wanaoiongoza. Tatizo wanasiasa wa Kiafrika huwa hawapendi kuwa na taasisi Imara kwani kwao siasa ni Kazi. Hata CCM wenyeviti wao wasingekuwa pia ni Marais leo hii nadhani Jakaya angekuwa bado yupo madarakani ndani ya CCM.
 
Hili tatizo la ukomo wa uenyekiti wa cdm ni jambo lililopigiwa kelele sana, lakini halijatatuliwa mpaka leo! Hapo ndio najua hivi vyama vya siasa ni uhuni kama uhuni mwingine. Hali hii ndio imenifanya mimi kutokuwa mwanachama wa chama chochote zaidi ya kuwa mshabiki tu.

Niliwahi kufuatilia lile sakata la kina Zitto, Kitila nk. walikuwa na hoja na madhaifu waliyataja kwa kina. Ila kwa sababu za ushabiki hoja zao zikafumbiwa macho. Ukiachia Magufuli kuvibania vyama vya upinzani kutotamba, madhaifu waliyoyasema kina Zitto ndio yanayoigharimu cdm sasa. Na madhaifu hayo hayawezi kuondoka iwapo bado Mbowe ataendelea kuwa mwenyekiti. Hivi ndugu yangu Allen inakuingia akilini kweli cdm kuwa na ofisi ya makao makuu ya vile kwa hali na miaka iliyonayo? Halafu anatokea mtu anakuambia Mbowe bado anastahili kuwa mwenyekiti! Nenda kaangalie nyumba ya Mbowe kama inafanana na ile ofisi ambayo yeye ni mwenyekiti more than 15yrs. Mkuu kama kweli cdm inahitaji mabadiliko ianze na Mbowe, kinyume na hapo ccm itaendelea kutamba huku ikiwa dhaifu.
 
Mkuu kama kweli cdm inahitaji mabadiliko ianze na Mbowe, kinyume na hapo ccm itaendelea kutamba huku ikiwa dhaifu.
Kwanza nitofautiane na wewe kidogo kuwa si sahihi kudhani udhaifu wa CDM unatokana kutokuwepo kwa ukomo wa muda wa uongozi ndani ya chama, badala yake unatokana na jinsi CDM ilivyojengwa.

Duniani kote huwa hauwekwi ukomo wa muda kwenye vyama ili kujenga demokrasia ya ndani na nafasi ya minyukano ya fikra chamani. Kama ndani ya chama hakuna nafasi ya kuruhusu minyukano ya fikra basi kubadilisha uongozi huwa shida sana. Demokrat ya Marekani inakabiliwa na mjadala mzito wa ndani juu ya kubadili uongozi wa juu wa chama hicho na kuleta kizazi kipya cha uongozi kwenye Demokrat.

Nyumba ya Mbowe ni jambo binafsi na kwa uhakika tatizo la Ofisi Kuu ya CHADEMA kuwa vile ilivyo linatokana na kutokuwa na sheria za matumizi ya fedha (Financial Regulations) ndani ya chama chenyewe.

Wakati wa Slaa alikuwa anasema hoja si kujenga Ofisi bali kujenga fikra za wananchi, waliokuwa wanataka ujenzi wa Ofisi walionekana kama vile wako nyuma kifikra. Ni lazima CHADEMA wajue Ofisi pia ni Utambulisho wa chama.Kama walishindwa kujenga Ofisi enzi za Kikwete nadhani kwa hivi sasa ndiyo itakuwa shida zaidi.
 
Kwanza nikupongeze sana kwa kutofautina na mimi kwenye mitazamo kwani ndio afya ya mjadala ili isitafsiriwe tunashambulia mtu na sio kujenga. Kwa taarifa yako muelekeo wa chama au taasisi zetu nyingi waafrika huakisi mtazamo wa kiongozi wake mkuu. Mara nyingi uimara na udhaifu wake huumbatanisha na taasisi anayoingoza. Nenda kwenye taasisi yoyote uone kama hujakuta taswira ya kiongozi yoyote kama, mavazi, kabila, uchapa kazi, ushirikina nk. Taasisi hizo hata kama zina katiba nzuri ama mbaya vipi kwetu africa tabia ya kiongozi ndio huamua mambo ndani ya taasisi husika.

Parapgraph yako ya pili sikubaliani nayo hata kama duniani kote kwenye vyama hakuna ukomo wa uongozi eti kisa ukomo utaua fikra za mikinzano. Najiuliza ni kwa vipi ukomo wa uongozi utaua hoja fikirishi au kinzani? Allen kwanza sikubaliani ni hili la kusema kwenye vyama hakuna ukomo, hapa napaswa kuchunguza vyama mbalimbali duniani kuhusu ukomo, vinginevyo utanilisha matango pori nikikuchekea.

Nyumba ya Mbowe nafahamu vyema ni jambo binafsi, ila nimetolea mfano tena mara moja ili kukazia hoja yangu.

Ujenzi wa ofisi ya cdm ni kweli enzi za Slaa ilisemekana watu wanawekeza kwenye elimu ya uraia, na kwa wakati ule ilikuwa kweli kwani tuliona operesheni mbalimbali, mikutano ya hadhara, cdm ilizunguka nchi nzima na kufungua matawi huku ikiongeza wanachama lukuki. Je baada ya kuingia Magufuli akapiga marufuku shuguli za vyama vya siasa kufanya siasa nchi nzima hela zinafanya nini zisijenge ofisi mpya yenye hadhi? Hebu niweke vizuri kwenye hili ndugu yangu.
 
Back
Top Bottom