Nani anafaa kuwa man of the match kwenye game ya leo kati ya Tanzania na Uganda?

Bocco amestahili. Gadiel jana hakuwa uchochoro, kaupiga safi sana nae. Team work nmeiona jana kwa kweli daah
 
Kikosi kapanga Manara..alimuambia Amunike babu ndivyo anavyotaka..si unajua wapopo kwa ndumba
Acha porojo hizo. Basi hizo maneno sie hazituhusu kinachotuhusu kwa sasa ni kushangilia na kujiandaa na Afcon
 
Nilishauri siku za nyuma, nashukuru Mungu, Amunike amenisikia. Kombination ya Samatta-Msuva-Bocco inaweza kuipasua defence yoyote ya Africa. Hawa wote ni deadly strikers na wana vitu tofautitofauti sana. Kuna mabavu, kimo na nidhamu ya mchezo (Bocco), kasi na upambanaji (Msuva), na akili na ubunifu wa mpira (Samatta)

Man of the match, bila shaka ni John Rapahel Bocco. Michango mingine iliyotukuka kutoka kwa wachezaji wot walioanza isipokuwa Manula ambaye hakuwa na kazi sana golini. Alilindwa vizuri. Huree Tanzania
Nimependa uchambuzi wako. Vivaaa Taifa stars
 
Kweli mkuu.. wanakuja mwishoni kama vikojozi bhana.
Yote kwa yote EAST AFRICA NI ZAMU YETU
BURUNDI
KENYA
UGANDA
TANZANIA.
Hapo mpaka robo fainali nadhani ni burundi tu ndio watakuwepo maana wapo on fire

Sent using my iPhone using jamiiforum app
 
Tusimsahau kocha msaidizi Moroco .. Naamini ndie aliemshauri Amunike upangaji wa kikosi...Maana ule ukuta kule nyuma ulikuwa ni balaa..Tofauti na siku ya Lesotho.
 
Back
Top Bottom