Nani amsaidie Hood

Nani amsaidie Hood

Hood wa sasa si wa enzi zileee; kila biashara huotji ubunifu na matangazo wafikiri cocacola hadi leo wanajitangaza simchezo kumaintain jina!!!!
Enzi hood ndio ilikuw gari yangu ya uhakika lakini si leo, hata dar moro hayupo!
Mara ya mwisho mwaka jana niliota safari ya ghafula nikapanda hapo mtawala kuelekea arusha bus imetoka mbeya na abiria saba tu nikaonea huruma sana ikabidi niulize kondakta akasema mfanyabiashara sababu amezoez kuwa barabarani hana budi hata kwa hasara inabidi aneendelee jenga imani kwa wateja!!! Mzee tulitoka saa kumi na moja tukafika same saa sita usiku tukalala hapo na mbeya express asubuhi radiator ikiamwaga maji yote safari ikaishia hapo ikabidi tufaulishwe!!!
 
Ukiona hivyo jua huyo kesha amua kuachana na hiyo biashara kwaiyo anajitoa barabarani pole pole anawekeza kwingine.Alafu unapoangalia uchakavu wa bus usisahau na tochi barabarani.
 
Yaan tena mtu katoka arusha anathubutu kupanda hood huo n uwendawazim wa kiwango cha lami wakat kuna gar za kupita dom zinaitafuta mbeya saa nne Au tano tena pamoja na vts hii ya sasa

Kulikua hakuna gari lolote isipokua hood siku hiyo
 
Yaani Moro Kwenda Mbeya night unapanda bus tena hood, hapo ni Mwendo wa I.T hapo Shell unazikuta I.T za kutosha.
 
Hizi gari sijui Hood alizipata wapi, na ni kama amefunga nazo mkataba wa kufa na kuzikana. Wenzake kadir muda unavyoenda huuza mabasi chakavu moja moja na ku replace mapya moja moja, lakin yeye kang'ang'ania tu mikangafu yake miaka nenda miaka rudi.

Bus ziko toka enzi za Plate Number za TZA mpaka leo anazo tu.
Hood sidhani kama anafanya tena biashara ya mabasi.Itakuwa walishagawana wanafamilia sidhani kama Mzee Hood ana mpango wa kuendelea na biashara
 
Hivi huko hakunaga dar lux?!!...sisi wa route ya dar-arusha-nairobi ni raha mustarehe kabisa hayo mambo ya kupanda vyuma chakavu tulishasahau miaka kadhaa nyuma
 
Back
Top Bottom