fugees
JF-Expert Member
- Aug 13, 2012
- 2,868
- 884
Habarini wanajamvi. Leo nikiwa Morogoro nikiwa nikitafuta usafiri wa kuelekea Mbeya (ili sikukuu hii ikalike huko kwa wanyakyusa) usafiri pekee niliona kama mkombozi wa safari yangu ni Hood.
Mida ya saa mbili usiku naliona busi la Hood hapa Msamvu, mpiga debe mmoja ananiambia bro huo ndio usafiri wa mwisho huwezi pata mwingine otherwise upande IT, nikaona isiwe tabu basi ngoja niwahi siti. Kama wasemavyo waungwana kuwa Mungu si athumani hatimaye nikapata siti na kulipia nauli ya kuelekea Mbeya.
Busi likaondoka Msamvu saa mbili na nusu kuelekea ofisi zao pale mtawala, mara kondakta anasema wajameni tutumie dakika kumi tu kuchimba dawa, basi abiria wengi wakashuka na kufanya hivyo nikiwamo mimi. Baada ya kuingia ndani yaani ofisi za Hood kuchimba dawa naona Hood yule wa miaka ya 2004 - 2007 kachoka sana yaani vyoo vyenyewe ni bora mara tano ya vyoo vya jera Keko au Segerea.
Ingawa sifikii levo za kiuchumi na Hood lakini niliona huruma sana na nikawaza sana namna biashara za watu zinakufa. Ikiwa saa tatu tunaondoka Morogoro kuelekea Mbeya busi hilo la arusha mbeya nikapata taarifa kuwa gari hilo limetoka Arusha saa kumi na mbili na kuingia Moro saa mbili.
Nilishikwa na wasi sana na kuna baadhi ya abiria waasema tutafika Mbeya saa kumi kesho duh nilitahamaki nikasema bora ningepanda IT. Kwa kweli safari imekua ya hofu gari ni bovu sana yaani gali inatembea kama mtu. So ile ndoto yangu ya kuwahi Mbeya saa ikakatika pale na nikawa sina hamu ya kufika muda huo tena.
Ila kikubwa nilichokiona Hood ananafasi kubwa ya kibiashara hususani ya mabasi hapa Morogoro maana kwa jina la Hood bado ni brand kubwa kwenye biashara ya usafirishaji
USAIDIZI
Hood anahitaji muwekezaji mwingine anunue brandi na kufanya biashara yake kwa jina hilo kwa maana brandi bado ipo vizuri. Ikumbukwe wapinzani wa kibiashara katika usafirishaji hapa morogoro ni abood na bm ila ninauhakika kama hoodi angekua na muwekezaji mpya basi hoodi na abood ndio wangekua wachuanaji pekee.
Kimsingi Hood amepotea sana kwenye biashara ya usafirishaji, kwa maana sidhani hata kama anamabasi matatu barabarani.
Hivyo kama wafanyabiashara kama bile Newforce wangeweza nunua au share brand na Hood hapa Morogoro na Tanzania kwa ujumla Hood bado angekua juu katika biashara hii ya usafirishaji.
Ni haya tu wadau.