Nani Ampokee Kikwete KIJITI?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,230
Hapa JF na kwingineko kuna watu wanaamini kwamba JK nchi imemshinda. Tuambiane basi kama leo JK akiamua kubwaga manyanga tunataka nani achukue kijiti kutoka kwa JK. Na tunataka huyo mtu ashirikiane na kina nani kuendesha nchi? Kulaumu bila kutoa suluhisho ni UZANDIKI!!
 
Nchi iwekwe chini ya UN kwa mkataba maalum wa uangalizi kama inawezekana kuunda utaratibu wa namna hii, halafu kila kipindi cha miaka kadhaa anachaguliwa UN Commissioner atakayeiendesha nchi.
Mkataba huo upige marufuku Mtanzania yeyote kuteuliwa kuwa Commissioner.
 
Hakuna wattu makini kwani hata hao wanaojiita wapinzani wanashindwa kuongoza hata taasisi zao za kifamilia Taznaia wataiweza? warekebishe vyama vyao kwanza
 
Tatizo ni kwamba uwezekano wa jamaa ku step down kabla ya wakati haupo.Kwa sababu kuna namna kama tatu za kuidondosha serikali,na zote sioni kama zinaweza ku function;
1.Kumtoa kupita NGUVU YA UMMA.Hii haiwezekani kwa sasa nguvu ya umma bado haijakomaa kwa kiwango hicho.Usisahau wa TZ wengi bado waoga wa mabomu na mapoyoyo.
2.Kupitia Bunge.Huko nako haiwezekani maana mkuu akihisi dalili mbaya tu anawahonga jamaa na nyongeza ya POSHO wananyamaza.
3.Kupitia mapinduzi ya kijeshi.Hilo nalo ndoto ya mchana maana upoyoyo upo hadi jeshini.
Labda watu wapige sala na maombi aachie mwenyewe kabla ya muda wake.
 
Hapa JF na kwingineko kuna watu wanaamini kwamba JK nchi imemshinda. Tuambiane basi kama leo JK akiamua kubwaga manyanga tunataka nani achukue kijiti kutoka kwa JK. Na tunataka huyo mtu ashirikiane na kina nani kuendesha nchi? Kulaumu bila kutoa suluhisho ni UZANDIKI!!
Mimi mrdash1 nitashirikiana na wana JF wote
 
Nchi iwekwe chini ya UN kwa mkataba maalum wa uangalizi kama inawezekana kuunda utaratibu wa namna hii, halafu kila kipindi cha miaka kadhaa anachaguliwa UN Commissioner atakayeiendesha nchi.
Mkataba huo upige marufuku Mtanzania yeyote kuteuliwa kuwa Commissioner.

Good idea,kulingana na nchi ilivyomshinda kuiendesha hii inaweza kuwa viable option in the short run.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom