Nani aliyemnyonga kamanda wa Polisi Zanzibar?

Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,356
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,356 2,000
Hatuachi Kujiuliza: Nani walio mnyonga Camander Aziz Juma?

Asalamu aleikum ndugu zangu wazanzibari na watanganyika wa ndani na nje ya Zanzibar na Tanganyika. Ama mimi nimefika hapa na masikitiko makubwa sana ya kifo cha Camander Azizi Juma aliekuwa Mkuu wa Polisi Zanzibar. Innalillah Wainailahi Rajiun.

Camander Azizizi Juma alifariki Ghafla siku ya Alhamisi ya tarehe 6.Juni 2019 na kifo chake kimeacha masuali mengi yakujiuliza kwa sisi Wazanzibari au Watanganyika ambao hutetea HAKI na kukataa kuburuzwa na watawala waliopo madarakani.

Kamander Azizi licha yakuwa yeye alikuwa ni mkuu wa polisi lakini aliwahi kusomea Sheria lkatika masomo yake ya juu na kazi zake inasemekana alikuwa akifanya kwakutumia sheria zaidi kuliko Utashi wa Kisiasa na chuki zinazofanywa na Polisi wa Tanganyika na Zanzibar.

Kabla yakuendelea na mkasa huu wa mauti ya kijana wa Kizanzibari ambae aliwahi kuwa mkuu wa Polisi Zanzibar naalishika nafasi hio kwa miaka 4-5 kama sijakosea kabla yakuhamishiwa Tanganyika.

Katika kipindi chake cha uongozi hapa Zanzibar, ile piga piga ya Polic-CCM na kamata kamata ya Wazanzibari wasiokuwa na hatia nyakati za usiku zilipungua. Watu waliokuwa karibu nae wanatueleza kwamba alikerwa sana na Ukamataji wa Mashekhe wa Uwamsho na kupelekwa Bara. Kamander Azizi alikuwa ni msaidizi AG -kama PR kule Bara. Alikukamata nafasi hio hadi alipo kufa siku ya tarehe 6. Juni 2019 hapo nyumbani kwake Kibweni.

Marehemu kamander Aziz,i baba yake ni mtu kutoka Kaskazini Unguja na Mama yake marehemu ni mtu wa Ngwachani Pemba. Marehemu alilelewa katika maadili mazuri ya kiungwana ambayo yalimfunza mambo mengi ya Dini na Culture zetu za Kizanzibari. Family ya marehemu ni watu waliokuwa wenye heshma, kujitambua kama wao ni Wazanzibari na upendo miongoni mwa jamii za kizanzibari.

Sio hivo tu pia, marehemu Azizi alikuwa ni mtu aliekuwa amesomea Sheria sana na kazi zake zote alizokuwa akifanya alikuwa mara nyingi anafuata sheria kuliko kuchukua utashi wa kisiasa kama wanavofanywa Polisi wengine. Kwa upande mwengine tunaweza kumuweka katika kundi la Polisi waliokuwa wasomi na wasiotaka kuburuzwa buruzwa.

Kwanini tuwe na Conspiracy Theory juu ya kifo Chake?

Wakati wa Uongozi wa Kamander Aziz inasemekana kulikuwa na fitna kubwa na majungu yakipikwa ndani ya uongozi wake.

Kabla ya yeye kushika nafasi hio ya ukuu wa Polisi Zanzibar nafasi hio ilikuwa ikishikiliwa na Kamander Mussa umaarufu (Mussa Meno au Ronaldinho). Kutokana na habari ziliotufikia, inasemekana marehemu Azizi alikuwa akipingana na kamander Mussa Juma katika uendeshaji wao wa nafasi hio nyeti.

Nitawarudisha nyuma kidogo kwenye historia ya Mashekhe waliokamatwa Zanzibar ili niwape picha halisi ya kutofahamiana baina ya Kamander Azizi na kamander Mussa Meno. Inasemekana mwaka wa 2014-15 kulikuwa na mashekhe wengi wakikamatwa ovyo nakuwekewa ndani bila sababu zozote zile. Kuna siku Shekhe mmoja alikamatwa na askari polisi msikitini wakati akiwa anatoa Hutba. Shekhe huyu tunasikia hakuwa na kosa lolote lile, na wafuasi wake waliwahi kupigiana simu na kuzifukuza gari hizo 2 za polisi waliovalia kivita hadi walikomficha Shekhe yule.

Polisi hao kwanza walimkimbiza shekhe huyo sehemu za Mazizini na walipoona watu wameshakuwa wengi sana na bado wengine wanaitana ndipo polisi walipoamua kumchukua Shekhe huyo hadi Madema. Wafuasi wa Shekhe huyu walizifuata gari hizi hadi Madema na kuanza kuzongea katika kituo nakuwataka polisi wamuachie shekhe wao.

Inasemekana Amri ya ukamatwaji wa Shekhe huyo haujulikani unatoka wapi, ila wazanzibari wengi walihisi kwamba polic-CCM walifanya hivo kwa lengo lao walitaka lifanyike zogo na wapate sababu ya kupiga watu.

Kitendo chakukusanyika watu pale Madema kilimkera mkereketwa Mussa Juma ambae alikuwa ni Mkuu wa Polisi Zanzibar na marehemu Azizi alikuwa kama msaidizi na mkuu wa kituo cha Madema. Kwa habari tulizozipata na baadhi ya polisi waliokuwepo kituoni siku hiyo, walithibitisha kwamba kamander Azizi alipokea simu kutoka kwa Mussa Juma na kumuamrisha atoe Gari 4 zenye polisi wenye silaha ili wawatawanye watu hao kwa nguvu na mabomu ya washa washa.

Mzozo ulitokea hapo kwani Kamander Azizi alikataa kata kata kutoa gari 4 za Polisi wenye Silaha za moto, na alifika mbali kwakumwambia Mkuu wa Polisi kama unataka mimi nifanye hivo basi lete maelezo hayo kwa maandishi na sio kwa simu.

Pia alisikika akimueleza kwamba ni nani alietowa Amri yakukamatwa kwa Shehe huyu msikitini na kumleta Madema wakati mimi kama ni mkuu wa kituo cha Madema sina habari hio? …..

Hivo marehemu Azizi alimwambia Mussa Juma kwamba, yeye kama mkuu wa Kituo atahakikisha wananchi hao hawaleti madhara katika kituo hicho na si vyenginevo. Baadae marehemu Azizi alipandishwa cheo cha Mussa Juma na Mussa akahamishiwa Tanganyika na kupewa fupa jengine angongone. Hapo ndipo Sakata la fitna za Upemba na Uunguja, Ukaskazini na Ukusini zikaanza hapo na kuwiva hadi zikenda kupakuliwa Tanganyika kwa Mabwana zetu.

Inasemekana baada ya hapo Kuna kundi la Wahadimu wa Kusini walifurahishwa na kitendo hicho cha Azizi kuvuliwa Ukuu wa Polisi Zanzibar. Lakini haikufika muda mrefu Mkuu wa Polisi Tanganyika alimwiota bara na kumteuwa kuwa kama Msaidizi wake au Spoke person. Wazanzibari wale waliokuwa kundi la Mussa Juma hawakufurahishwa na uteuzi huo.

Kulitokea nini Siku ya Kifo Chake?

Marehemu Azizi alikuwa Zanzibar Kibweni siku ya kifo chake alhamisi ya tarehe 6.Juni 2019 ambayo ilikuwa ni sku ya pili ya Eid El Fitri.

Inasemrkana marehemu Azizi alikuwa Bara lakini alikuja nyumbani kwa ajili ya skukuu.

Mazingira ya nyuma ya nyumba ya marehemu kuna miti miti mingi aliopanda kwa ajili ya upepo. Habari zilizotufikia siku ya Alhamisi usiku saa mbili marehemu alikwenda kusali Isha na baadae aliporudi nyumbani kwake watu walisikia kama miti hio inakamatwa kamatwa majani kana kwamba kuna watu wanajaribu kupita ndani ya uwanja wa nyumba yake.

Marehemu alifikiria ni Wizi hivo alichukua tochi yake nakwenda kuangalia nje kama kulikuwa na watu au laa. Baada ya muda wa dakika kupita bila ya yeye kurudi wala kusikia kelele yoyote ile ndio family ilikwenda nje kumuangalia kwavile waliona kimyaa na yeye hakurudi ndani.

Lakini walipotafuta tafuta na kumwita hawakuona kitu wakadhani kwamba baada ya incident ile iliomtoa nje labda aliekuwa maeneo ya jirani kwavile ana uhusiano mzuri na jirani zake.

Baada ya masaa mawili kupita hajarudi ndani ndio family yake wakaanza kuingia wasi wasi na kupiga simu kwa majirani wa pale mtaani nakuuuliza. Ndipo wakatoka nje nakuanza kumwita nakumtafuta kwa tochi wakaona mwili wake ukininginia juu ya mti mmoja katika miti hiyo iliokuwa nyuma ya nyumba yake. Inasemekana marehemu alikuwa amefungwa mikono nyuma na (Ati) madaktari waliomchunguza wanasema kwamba shingoni kwake alikuwa na alama za mikono kamwa alikabwa Kibi kwanza kabla yakuwekwa kitanzi.

Wazanzibari wengi tuliosikia kifo chake tulisikitika sana na wale tulio ijuwa family yake hatukuweza kupata picha kama Azizi anaweza kujitundika mwenyewe. Ila kifo chake kinaambatana na utata wa Cheo chake alichokuwa nacho na asili yake anakotoka pamoja na Dini. Hakika Jeshi la Polisi Bara hawataki Zanzibar wawe na watu wazuri waliosoma katika nyadhifa za Polisi. Wao wanachotaka ni kuwaona Watu kama Kamander Mussa Juma ambae anaburuzwa.

Pili Azizi hakuwa kijana aliekuwa amehadaika na vyeo au cheo. Ni mtu alikuwa na kinaa pamoja na kujiamini na lile alilokuwa akilifanya. Kamander Azizizi anaambiwa kajinyonga mwenyewe. Lakini mtu aliejinyonga hawezi kujifunga kamba kwa nyuma.

Siku ya maziko yake tulitarajia Mkuu wa Polisi SIRO ahudhurie maziko yake lakini chakusikitisha ni Askari wachache sana wenye vyeo vya juu walihudhuria maziko yake.

Hata hivo Kwentu Sisi Wazanzibari haikutushuhulisha sana kwani wenyewe Tulitosha kwenda kumzika alhamdulilah . Allah amlaze mahali pema peponi, na kama amedhulumiwa basi Kamander Azizi atakuwa amekufa shahidi.

Watu wasiojulikana Sasa wameanza Stile mpya za Assacination na sio ile tulioifahamu katika kipindi cha nyuma cha tokea Utawala huu wa awamu ya tano kukaa madarakani.

Tukumbuke kwamba kuna watu wengi wasio hatia tayari wamepotea na wengine kushambuliwa kwa Risasi mchana kweupe na Serikali ya Magufuli imekaa kimyaa. Tunajuwa kwamba Polic-CCM wanatumika katika mauwaji na utekaji wa Watu wasio na hatia kwa vile tuu wanapingana na Utawala uliokuwepo.

Tunajuwa Kwamba bado kuna njama nyengine nyingi za utekwaji na Mauwaji unaandaliwa kwa ajili ya Viongozi wapizanni pamoja na wana sheria waliokuwa wamekataa kunyamazishwa.

Hata hivo Sisi Wazanzibari tunatakiwa tujiulize. Kwanini kifo cha mtu kama huyu kiwe kimyaa?

Kwanini hatuwezi kusema na kukemea. Inaonyesha kwamba sisi tumekuwa Wafu kiasi ya kwamba hata tuone maovu yanatendeka tunanyamaza kimyaa.

Tujuwe lilomfika mwezio leo huenda litakufika wewe kesho.

CHANZO: MZALENDO.NET
 
K

kantalambaz

JF-Expert Member
Joined
Dec 24, 2017
Messages
1,333
Points
1,500
K

kantalambaz

JF-Expert Member
Joined Dec 24, 2017
1,333 1,500
Ukiendelea na uzushi wa hivi jela inakuhusu kwa matumizi mabaya ya mtandao.
 
M

Mine eyes

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2016
Messages
3,956
Points
2,000
M

Mine eyes

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2016
3,956 2,000
Aisee shetani kaamua ,yaani wasiojulikana wamefika mpaka Zanzibar .
Zanzibar wapo miaka yote ..hili ni geni kwa bara!
Huku si ajabu..tena yapo mengi yanafanyika...
Ndio maana wazenj wanajenga chuki na watanganyika..wanamaumivu...
na majeraha mengi....
 
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,356
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,356 2,000
Umeandika umbea tuu ulioota ndotoni. Siri ya kifo cha marehemu anaijua marehemu mwenyewe. Sababu ulizoweka hazina msingi wala uzito wowote wa kuchukua uhai wa mtu. Zaidi unajaribu kufanua uchochezi tuuu. Fanya kazi acha umbea.
uko Lumumba ?? Ulishatoa mchango wa mafuta ya mwenge ??
 
D

Deceiver

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2018
Messages
1,598
Points
2,000
D

Deceiver

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2018
1,598 2,000
Taarifa hii ni ya kupuuzwa kwaa kiasi fulani.

Jamaa alijinyonga.hata familia inalijua hilo.

Kufungwa kamba ni jambo linasemekana tu ili kumtoa katika fedheha ya kujinyonga lakini ukweli hamna kamaba wala nini.

Mtu kama yule akamatwe afungwe kamba,akabwe alafu asipige kelele tu awe kimya tu..?

Kusema kwamba nyuma ya nyumba kulikuwa na hzo kama watu wanasisika wakikamata majani ni uongo tu wa kutaka kuwatoa watu kwenye reli kwamba jamaa alijinyonga.lakini inasemwa kwamba huwenda hicho kilichosikika ni ile purukubshani zake mwenyewe akijaribu kujinasua baada ya kujitundika na kupiga kelele ni ngumu hivyo lazima apapatike kwanza na hizo papara huwenda ndo walizosikia watu wakasema labda wavamizi

ALAMA za vidole zilizokutwa ni alama za vidole vyake mwenyewe ambayo alikuwa akijikamata kwa lengo la kujipapatua na kujitoa katika kitanzi baada ya kujitundika.

Ushahidi wote unaonesha kwamba alijinyonga,haiwezekani mtu kaama yule avamiwe alafu awe kimya tu uongo huo.

Sema wazanzibari kwa fitina siwawezi,wao kuitupia bara kila kitu sio ajabu sana.

sirro hakufika kwa sababu jamaa alijinyonga na kwamujibu wa jeshi mtu akijinyonga amedhalilisha jeshi na hastahiki kuzikwa kwa heshima.

Kwa chep chake jamaa sirro ilikuwa aje kabisa na timu maalum ya viongozi wa polisi wapige gwaride la heshima na timu hiyo iliandaliwa kabisa,lakini ilipothibitika kwamba kajinyonga mwenyewe kitu hicho kiliahirishwa moja kwa moja kutokana na kujinyonga kwakwe.

Viongozi waliokuja msibani walikuwa wao binafsi tu sio kiniaba ya kazi na chep cha marehemu,hyo ypte ni kutokana na kujinyonga kwake ni fedheha kwa jeshi na hata kidini pia aliyejinyonga ni kama kaua hvyo anakuwa kama kafanya uasi na anakosa baadhi ya stahiki zake.

Huwenda alirogwa mpaka ikapelekea kujinyonga,kama alirogwa basi dhambi ni za huyo aliyeroga.

Kama hakurogwa basi malipo yake yapo kwa Mola subhaana.
Uchawi ungekuwepo visiwani. CUF wangeshawaroga CCM kitambo sana. Albadr nayo ingekuwepo basi masheikh wa uamsho wangekua wako huru tena majumbani mwao
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,703
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,703 2,000
Mbona mkiambiwa alijiua mnapanick sana..haiwezekani au?

Jamaa alijiua.

Wewe una ushahidi gani kwamba ameuliwa?

Mimi nafahamu kwa mazingira ya kwake sio rahisi watu kumuua kimya kimya alafu wapande ukuta waondoke na yeyr asipige kelele kabisa.

Ukuta wa nyumba yake sio wa kuparamis kirahisi rahisi,na wala hakuna ushahidi wowote wa kuonesha kwamba ameuwawa.

Kama angrkuwa ameuwawa angechezewa paredi la heshima kwa mujibu wa cheo chakee.
Hivi wewe unaushahidi gani wakua alijiua?
 
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,356
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,356 2,000
Si nafasi yangu kumhukumu yoyote yule, ila....

Hakuna muislam yeyote tena ambae ni askari polisi wa hapa Zanzibar (mzanzibar) ambae atabaki msafi huku anajua kabisa kwamba masheikh wameonewa na wanaonewa.

Nasikitika kufkiria kwamba familia ya the so called kamanda azizi itayapitia mabaya zaidi kuliko wanayoyapitia familia za kina farid na wenzao. Maana at least uamsho familia zao kuna watu wanazihudumia kwa kila kitu ila yeye ndio imetoka hivyo.

Hata hao waliokuwa wakimtuma kina sirro msibani hawakufika😀😀😀😀

Allah SW anasema sura 4:9

Na wachelee wale ambao lau kuwa na wao wangeli acha nyuma yao watoto wanyonge wangeli wakhofia. Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme maneno yaliyo sawa.

Ikiwa huyo Marehemu alikuwa ni mcha Mungu na msema ukweli, Allah ametoa uhakikisho wa maisha ya hiyo familia yake wakati yeye ameshatangulia.

Allahu Aalam
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,703
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,703 2,000
Kumbe una majibu yako ?Nilikuuliza hivi Lukuvi anapoiambia Zanzibar Sisi tunajeshi , Sisi ni Nani ?? Unaleta hadithi nyingi
Anaposema sisi kama anawakilisha serikali au watangakia ndo umenijibu hapo..?

Hujanijibu maswali langu,maswali yangu yapo waazi kabisa naomba kujuzwaa na wewe mzanzibari msafi...

Hujanijibu nilichouliza..

Nani anawalazimisha wazenji kuwa watanganyika...?

Ili uwe mtanganyika uwe una sifa zipi na tabia zipi kiasi kwamba ifike hatua isemwe kwamba huyu sasa ni mtanganyika rasmi..?

Lukuvi kusema "sisi tuna jeshi " ndo hapo kalazimisha vipi wazanzibari kuwa watanganyika,mbona hakuna uhusiano..?

Maswali yangu hujajibu mkuu,watu kama ninyi mtume kawasema vibaya sana na mafikio yenu juu ya ubaguzi na ukabila ni mabaya sana.

دعوهااااااااا......
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,703
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,703 2,000
Jamaa kajiuwa hilo lipo wazi.na ndio maana hakuchezewa paredi la heshima la mazishi..
Uchawi ungekuwepo visiwani. CUF wangeshawaroga CCM kitambo sana. Albadr nayo ingekuwepo basi masheikh wa uamsho wangekua wako huru tena majumbani mwao
 
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,356
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,356 2,000
Anaposema sisi kama anawakilisha serikali au watangakia ndo umenijibu hapo..?

Hujanijibu maswali langu,maswali yangu yapo waazi kabisa naomba kujuzwaa na wewe mzanzibari msafi...

Hujanijibu nilichouliza..

Nani anawalazimisha wazenji kuwa watanganyika...?

Ili uwe mtanganyika uwe una sifa zipi na tabia zipi kiasi kwamba ifike hatua isemwe kwamba huyu sasa ni mtanganyika rasmi..?

Lukuvi kusema "sisi tuna jeshi " ndo hapo kalazimisha vipi wazanzibari kuwa watanganyika,mbona hakuna uhusiano..?

Maswali yangu hujajibu mkuu,watu kama ninyi mtume kawasema vibaya sana na mafikio yenu juu ya ubaguzi na ukabila ni mabaya sana.

دعوهااااااااا......
Unatafuta ubishi usio mashiko au umeshaujua ukweli lakini unajaribu kuficha ficha ?? Lukuvi kaongea SISI TANZANIA BARA TUNA JESHI

Ikiwa Tanzania bara wana jeshi jee hapo Zanzibar linafanya kitu gani ?? kama si Uvamizi ??
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,703
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,703 2,000
Wazenji wakati mwingine wana chuki za kijinga tu mkuu.
Mtu anaeema eti jamaa kauwawa na watanganyika alafu sababu zenyewe za kitoto kabisa.

Wakati jamaa kajiuwa mwenyewe kabisa na ndyo msna hakuchezewa paredi la mazishi kwa sababu jeshi linakataa na hata sirro hakwenda baada ya kuthibitika alijiuwa.

Wazenji baadhi yao wana bifu za kijingaa,jamaa alijiuwa mwenyewe kwenye mabanda yake ya kuku nyumbani kwake,alikuwa amejitundika na kamba iko shingoni.

Alijiandaa hasa na hiyo siku alojinyonga simu aliacha ndani,na kuna rafiki yake alikuwa na kawaida ya kupiga nae stori baada ya swala ya usku,lakini siku hiyo akamuambia hayuko sawa amuache aende zake
Sasa jee jamaa alijua kama kuna watu wanakuja kumuua mpaka akatae kupiga stori na rafiki yake kama kawaida yao..?

Na huyo rafiki yake ndo alipigiwa simu mwanzo baada ya kuwa jamaa haonekani,akawaambia "nilionsna nae akaniambia hayuko sawa leo nimuachee"

Walipopiga simu yake wakaona inaita ndani na hapo ndo wakaanza kumtafuta wakamkuta kwenye mabanda yake kajinyonga.

Kauwawa vipi asipige kelele?
Watu wanakuja mpaka wanaondoka wasisikie vishindo kwamba kuna mtu anakabwa huko?

Na huo ukuta wa nyumbani kwake umefika ukauona ulivyo mrefu..?

Kiufupi alijjiuwa mwenyewe
Zanzibar wapo miaka yote ..hili ni geni kwa bara!
Huku si ajabu..tena yapo mengi yanafanyika...
Ndio maana wazenj wanajenga chuki na watanganyika..wanamaumivu...
na majeraha mengi....
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,703
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,703 2,000
Kwani kusema kwake sisi tuna jeshi ina maana watanganyika wote wanashiriki na kuingia katika kauli hiyo?

Watanganyika wote ni wavamizi wa zanzibar kwa sababu eti amesema mtu fulani wa serikali maneno hayo?

Na vipi kama aliposema sisi alikusudia wao serikali ya tanganyika na sio watanganyika wote mpaka sisi raia ambao hatuna mamlaka yeyote wewe unaleta tafsiri ipi..?

Hujanijibu nilichouliza..

Huyo lukuvi aliposema hivyo ndio maana yake wazenji wote wawe watanganyika....?

Ili uwe mtanganyika uwe una sifa zipi na tabia zipi kiasi kwamba ifike hatua isemwe kwamba huyu sasa ni mtanganyika rasmi..?
Unatafuta ubishi usio mashiko au umeshaujua ukweli lakini unajaribu kuficha ficha ?? Lukuvi kaongea SISI TANZANIA BARA TUNA JESHI

Ikiwa Tanzania bara wana jeshi jee hapo Zanzibar linafanya kitu gani ?? kama si Uvamizi ??
 
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,356
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,356 2,000
Wazenji wakati mwingine wana chuki za kijinga tu mkuu.
Mtu anaeema eti jamaa kauwawa na watanganyika alafu sababu zenyewe za kitoto kabisa.

Wakati jamaa kajiuwa mwenyewe kabisa na ndyo msna hakuchezewa paredi la mazishi kwa sababu jeshi linakataa na hata sirro hakwenda baada ya kuthibitika alijiuwa.

Wazenji baadhi yao wana bifu za kijingaa,jamaa alijiuwa mwenyewe kwenye mabanda yake ya kuku nyumbani kwake,alikuwa amejitundika na kamba iko shingoni.

Alijiandaa hasa na hiyo siku alojinyonga simu aliacha ndani,na kuna rafiki yake alikuwa na kawaida ya kupiga nae stori baada ya swala ya usku,lakini siku hiyo akamuambia hayuko sawa amuache aende zake
Sasa jee jamaa alijua kama kuna watu wanakuja kumuua mpaka akatae kupiga stori na rafiki yake kama kawaida yao..?

Na huyo rafiki yake ndo alipigiwa simu mwanzo baada ya kuwa jamaa haonekani,akawaambia "nilionsna nae akaniambia hayuko sawa leo nimuachee"

Walipopiga simu yake wakaona inaita ndani na hapo ndo wakaanza kumtafuta wakamkuta kwenye mabanda yake kajinyonga.

Kauwawa vipi asipige kelele?
Watu wanakuja mpaka wanaondoka wasisikie vishindo kwamba kuna mtu anakabwa huko?

Na huo ukuta wa nyumbani kwake umefika ukauona ulivyo mrefu..?

Kiufupi alijjiuwa mwenyewe
Naona unatuongezea chumvi ya rafiki ambazo labda ulisahau kutuambia. Kuna Ex Diplomat wa Ufaransa alikuwa akiishi Zanzibar pamoja na mke wake , aliuliwa nyumbani nyumbani mwake yeye na mke wake pamoja na mbwa wao na hawakuonekana zaidi ya miezi 3 , utaniambia kwa nini hawakupiga kelele wala mbwa kubweka .Mpaka ulipofanywa uchunguzi ndio ikagundulikana kuwa waliuliwa na kutumbukizwa kisimani
 
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,356
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,356 2,000
Kwani kusema kwake sisi tuna jeshi ina maana watanganyika wote wanashiriki na kuingia katika kauli hiyo?

Watanganyika wote ni wavamizi wa zanzibar kwa sababu eti amesema mtu fulani wa serikali maneno hayo?

Na vipi kama aliposema sisi alikusudia wao serikali ya tanganyika na sio watanganyika wote mpaka sisi raia ambao hatuna mamlaka yeyote wewe unaleta tafsiri ipi..?

Hujanijibu nilichouliza..

Huyo lukuvi aliposema hivyo ndio maana yake wazenji wote wawe watanganyika....?

Ili uwe mtanganyika uwe una sifa zipi na tabia zipi kiasi kwamba ifike hatua isemwe kwamba huyu sasa ni mtanganyika rasmi..?
KIMBIA LAKINI KAONGEA HIVI

Lukuvi kaongea SISI TANZANIA BARA TUNA JESHI maneno hayo anaiambia ZANZIBAR

Maneno haya uliyoandika , mimi sijayasema , unanipakazia

" Watanganyika wote ni wavamizi wa zanzibar kwa sababu eti amesema mtu fulani wa serikali maneno hayo?"
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,703
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,703 2,000
KIMBIA LAKINI KAONGEA HIVI

Lukuvi kaongea SISI TANZANIA BARA TUNA JESHI
Hujanijibu nilichouliza..

Nani anawalazimisha wazenji kuwa watanganyika...?

Kusema kwake tanzania bara tuna jeshi ina maana wewe unawajumuisha watanganyika wote mpaka wale wasiokuwa na mamlaka na chochote serikalini wewe unawajumuisha ni katika wavamizi...?

Kati ya jeshi wa tanzania bara na raia wa tanzania bara wepi wanakuja kuvamia zanzibar...?

Mpaka mimi niliekuja zanzibar kwa shughuli za uvuvi naivamia zanzibar sio...?

Ili uwe mtanganyika uwe una sifa zipi na tabia zipi kiasi kwamba ifike hatua isemwe kwamba huyu sasa ni mtanganyika rasmi..?
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,703
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,703 2,000
Bado hoja yako haikanushi kujiuwa kwa huyo jamaa kwa sababu mazingira kabla ya kujinyonga yapo wazi.

1.rafiki yake ambae alimhairisha siku wasipige stori na akasema hayuko sawa.

Je hapo ina maana alijua kuna watu wanakuja kumuuwa hivyo akawaandalia mazingira mazuri wampate kirahisi...?

Na ushahhidi wa rafiki yake upo kwa sababu alipigiwa simu.

Unaweza kuelewa ni kipi kilimsumbua siku hiyo mpaka akaghairisha stori na rafiki yake...?

Wewe ni mkabila mchafu ambae unastahiki kurudoshwa katika zama za ujaahiliyya.

Huko ndo unakostahiki kuwepo,sio katika jamii ya watu wastaarabu.
Naona unatuongezea chumvi ya rafiki ambazo labda ulisahau kutuambia. Kuna Ex Diplomat wa Ufaransa alikuwa akiishi Zanzibar pamoja na mke wake , aliuliwa nyumbani nyumbani mwake yeye na mke wake pamoja na mbwa wao na hawakuonekana zaidi ya miezi 3 , utaniambia kwa nini hawakupiga kelele wala mbwa kubweka .Mpaka ulipofanywa uchunguzi ndio ikagundulikana kuwa waliuliwa na kutumbukizwa kisimani
 
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2019
Messages
3,703
Points
2,000
safuher

safuher

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2019
3,703 2,000
Mkuu hilo mama ni jinga ni la kupuuzwa,nilikuwa namheshimu ila saivi namchukulia ni kama victim flani.
Faiza ukisoma hilo unaloita andiko kuna habari iliyothibitishwa hapo hata na familia? Au nawe unaingia ktk mkumbo waa kusikia sikia?
 
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,356
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,356 2,000
Hujanijibu nilichouliza..

Nani anawalazimisha wazenji kuwa watanganyika...?

Kusema kwake tanzania bara tuna jeshi ina maana wewe unawajumuisha watanganyika wote mpaka wale wasiokuwa na mamlaka na chochote serikalini wewe unawajumuisha ni katika wavamizi...?

Kati ya jeshi wa tanzania bara na raia wa tanzania bara wepi wanakuja kuvamia zanzibar...?

Mpaka mimi niliekuja zanzibar kwa shughuli za uvuvi naivamia zanzibar sio...?

Ili uwe mtanganyika uwe una sifa zipi na tabia zipi kiasi kwamba ifike hatua isemwe kwamba huyu sasa ni mtanganyika rasmi..?

Haya unayasema wewe kwa chuki zako

Mimi naongelea nini Lukuvi alichokisema wakati akimwakilisha Waziri Mkuu kanisani, na wewe yaelekea umeweka pamba masikioni m hutaki kusikia

Lukuvi amesema wazi kuwa TANZANIA BARA INA JESHI , sasa ikiwa anawaambia wazanzibari hapo utatafsiri mwenyewe haki hiyo unayo

Zaidi ya Yote watanganyika , wakenya na watu wa mataifa mengine wapo kabla ya uvamizi wa Januari 1964 na hakuna mtu aliyesema au kuthubutu kuwaita wavamizi.

Mimi ninapoongea wavamizi nakusudia mamlaka ya Tanganyika

Laanatullahi Nyerere aliivamia Zanzibar Januari 12 , 1964 na kumkamata Waziri Mkuu wake MUHAMMED SHAMTE aliyechaguliwa na wananchi , PAMOJA NA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI NA KUWAPELEKA KATIKA MAJELA YA TANGANYIKA, bila kuwafikisha mahakamani , hiyo hiyo Januari 1964.

Wakati wako jela Tanganyika mwezi wa Aprili tarehe 26 tukatangaziwa kuwa kuna muungano umezaliwa umepewa jina Tanzania. JEE HUO KAMA SI UVAMIZI TUITE KITU GANI ????
 
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,356
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,356 2,000
Bado hoja yako haikanushi kujiuwa kwa huyo jamaa kwa sababu mazingira kabla ya kujinyonga yapo wazi.

1.rafiki yake ambae alimhairisha siku wasipige stori na akasema hayuko sawa.

Je hapo ina maana alijua kuna watu wanakuja kumuuwa hivyo akawaandalia mazingira mazuri wampate kirahisi...?

Na ushahhidi wa rafiki yake upo kwa sababu alipigiwa simu.

Unaweza kuelewa ni kipi kilimsumbua siku hiyo mpaka akaghairisha stori na rafiki yake...?

Wewe ni mkabila mchafu ambae unastahiki kurudoshwa katika zama za ujaahiliyya.

Huko ndo unakostahiki kuwepo,sio katika jamii ya watu wastaarabu.

HEEEEEE KUMBE SIKU HIZI WAVUVI KUTOKA TANGANYIKA WANAJUA MPAKA MARAFIKI WA WAKUU WA POLISI WALIOKO ZANZIBAR, MAENDELEO :p:p:p
 
Forum statistics

Threads 1,325,709
Members 509,275
Posts 32,200,264
Top