Nani aliyemnyonga kamanda wa Polisi Zanzibar?

Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2008
Messages
22,417
Points
2,000
Gavana

Gavana

JF-Expert Member
Joined Jul 19, 2008
22,417 2,000
Hatuachi Kujiuliza: Nani walio mnyonga Camander Aziz Juma?

Asalamu aleikum ndugu zangu wazanzibari na watanganyika wa ndani na nje ya Zanzibar na Tanganyika. Ama mimi nimefika hapa na masikitiko makubwa sana ya kifo cha Camander Azizi Juma aliekuwa Mkuu wa Polisi Zanzibar. Innalillah Wainailahi Rajiun.

Camander Azizizi Juma alifariki Ghafla siku ya Alhamisi ya tarehe 6.Juni 2019 na kifo chake kimeacha masuali mengi yakujiuliza kwa sisi Wazanzibari au Watanganyika ambao hutetea HAKI na kukataa kuburuzwa na watawala waliopo madarakani.

Kamander Azizi licha yakuwa yeye alikuwa ni mkuu wa polisi lakini aliwahi kusomea Sheria lkatika masomo yake ya juu na kazi zake inasemekana alikuwa akifanya kwakutumia sheria zaidi kuliko Utashi wa Kisiasa na chuki zinazofanywa na Polisi wa Tanganyika na Zanzibar.

Kabla yakuendelea na mkasa huu wa mauti ya kijana wa Kizanzibari ambae aliwahi kuwa mkuu wa Polisi Zanzibar naalishika nafasi hio kwa miaka 4-5 kama sijakosea kabla yakuhamishiwa Tanganyika.

Katika kipindi chake cha uongozi hapa Zanzibar, ile piga piga ya Polic-CCM na kamata kamata ya Wazanzibari wasiokuwa na hatia nyakati za usiku zilipungua. Watu waliokuwa karibu nae wanatueleza kwamba alikerwa sana na Ukamataji wa Mashekhe wa Uwamsho na kupelekwa Bara. Kamander Azizi alikuwa ni msaidizi AG -kama PR kule Bara. Alikukamata nafasi hio hadi alipo kufa siku ya tarehe 6. Juni 2019 hapo nyumbani kwake Kibweni.

Marehemu kamander Aziz,i baba yake ni mtu kutoka Kaskazini Unguja na Mama yake marehemu ni mtu wa Ngwachani Pemba. Marehemu alilelewa katika maadili mazuri ya kiungwana ambayo yalimfunza mambo mengi ya Dini na Culture zetu za Kizanzibari. Family ya marehemu ni watu waliokuwa wenye heshma, kujitambua kama wao ni Wazanzibari na upendo miongoni mwa jamii za kizanzibari.

Sio hivo tu pia, marehemu Azizi alikuwa ni mtu aliekuwa amesomea Sheria sana na kazi zake zote alizokuwa akifanya alikuwa mara nyingi anafuata sheria kuliko kuchukua utashi wa kisiasa kama wanavofanywa Polisi wengine. Kwa upande mwengine tunaweza kumuweka katika kundi la Polisi waliokuwa wasomi na wasiotaka kuburuzwa buruzwa.

Kwanini tuwe na Conspiracy Theory juu ya kifo Chake?

Wakati wa Uongozi wa Kamander Aziz inasemekana kulikuwa na fitna kubwa na majungu yakipikwa ndani ya uongozi wake.

Kabla ya yeye kushika nafasi hio ya ukuu wa Polisi Zanzibar nafasi hio ilikuwa ikishikiliwa na Kamander Mussa umaarufu (Mussa Meno au Ronaldinho). Kutokana na habari ziliotufikia, inasemekana marehemu Azizi alikuwa akipingana na kamander Mussa Juma katika uendeshaji wao wa nafasi hio nyeti.

Nitawarudisha nyuma kidogo kwenye historia ya Mashekhe waliokamatwa Zanzibar ili niwape picha halisi ya kutofahamiana baina ya Kamander Azizi na kamander Mussa Meno. Inasemekana mwaka wa 2014-15 kulikuwa na mashekhe wengi wakikamatwa ovyo nakuwekewa ndani bila sababu zozote zile. Kuna siku Shekhe mmoja alikamatwa na askari polisi msikitini wakati akiwa anatoa Hutba. Shekhe huyu tunasikia hakuwa na kosa lolote lile, na wafuasi wake waliwahi kupigiana simu na kuzifukuza gari hizo 2 za polisi waliovalia kivita hadi walikomficha Shekhe yule.

Polisi hao kwanza walimkimbiza shekhe huyo sehemu za Mazizini na walipoona watu wameshakuwa wengi sana na bado wengine wanaitana ndipo polisi walipoamua kumchukua Shekhe huyo hadi Madema. Wafuasi wa Shekhe huyu walizifuata gari hizi hadi Madema na kuanza kuzongea katika kituo nakuwataka polisi wamuachie shekhe wao.

Inasemekana Amri ya ukamatwaji wa Shekhe huyo haujulikani unatoka wapi, ila wazanzibari wengi walihisi kwamba polic-CCM walifanya hivo kwa lengo lao walitaka lifanyike zogo na wapate sababu ya kupiga watu.


Kitendo chakukusanyika watu pale Madema kilimkera mkereketwa Mussa Juma ambae alikuwa ni Mkuu wa Polisi Zanzibar na marehemu Azizi alikuwa kama msaidizi na mkuu wa kituo cha Madema. Kwa habari tulizozipata na baadhi ya polisi waliokuwepo kituoni siku hiyo, walithibitisha kwamba kamander Azizi alipokea simu kutoka kwa Mussa Juma na kumuamrisha atoe Gari 4 zenye polisi wenye silaha ili wawatawanye watu hao kwa nguvu na mabomu ya washa washa.

Mzozo ulitokea hapo kwani Kamander Azizi alikataa kata kata kutoa gari 4 za Polisi wenye Silaha za moto, na alifika mbali kwakumwambia Mkuu wa Polisi kama unataka mimi nifanye hivo basi lete maelezo hayo kwa maandishi na sio kwa simu.

Pia alisikika akimueleza kwamba ni nani alietowa Amri yakukamatwa kwa Shehe huyu msikitini na kumleta Madema wakati mimi kama ni mkuu wa kituo cha Madema sina habari hio? …..

Hivo marehemu Azizi alimwambia Mussa Juma kwamba, yeye kama mkuu wa Kituo atahakikisha wananchi hao hawaleti madhara katika kituo hicho na si vyenginevo. Baadae marehemu Azizi alipandishwa cheo cha Mussa Juma na Mussa akahamishiwa Tanganyika na kupewa fupa jengine angongone. Hapo ndipo Sakata la fitna za Upemba na Uunguja, Ukaskazini na Ukusini zikaanza hapo na kuwiva hadi zikenda kupakuliwa Tanganyika kwa Mabwana zetu.

Inasemekana baada ya hapo Kuna kundi la Wahadimu wa Kusini walifurahishwa na kitendo hicho cha Azizi kuvuliwa Ukuu wa Polisi Zanzibar. Lakini haikufika muda mrefu Mkuu wa Polisi Tanganyika alimwiota bara na kumteuwa kuwa kama Msaidizi wake au Spoke person. Wazanzibari wale waliokuwa kundi la Mussa Juma hawakufurahishwa na uteuzi huo.

Kulitokea nini Siku ya Kifo Chake?

Marehemu Azizi alikuwa Zanzibar Kibweni siku ya kifo chake alhamisi ya tarehe 6.Juni 2019 ambayo ilikuwa ni sku ya pili ya Eid El Fitri.

Inasemrkana marehemu Azizi alikuwa Bara lakini alikuja nyumbani kwa ajili ya skukuu.

Mazingira ya nyuma ya nyumba ya marehemu kuna miti miti mingi aliopanda kwa ajili ya upepo. Habari zilizotufikia siku ya Alhamisi usiku saa mbili marehemu alikwenda kusali Isha na baadae aliporudi nyumbani kwake watu walisikia kama miti hio inakamatwa kamatwa majani kana kwamba kuna watu wanajaribu kupita ndani ya uwanja wa nyumba yake.

Marehemu alifikiria ni Wizi hivo alichukua tochi yake nakwenda kuangalia nje kama kulikuwa na watu au laa. Baada ya muda wa dakika kupita bila ya yeye kurudi wala kusikia kelele yoyote ile ndio family ilikwenda nje kumuangalia kwavile waliona kimyaa na yeye hakurudi ndani.

Lakini walipotafuta tafuta na kumwita hawakuona kitu wakadhani kwamba baada ya incident ile iliomtoa nje labda aliekuwa maeneo ya jirani kwavile ana uhusiano mzuri na jirani zake.

Baada ya masaa mawili kupita hajarudi ndani ndio family yake wakaanza kuingia wasi wasi na kupiga simu kwa majirani wa pale mtaani nakuuuliza. Ndipo wakatoka nje nakuanza kumwita nakumtafuta kwa tochi wakaona mwili wake ukininginia juu ya mti mmoja katika miti hiyo iliokuwa nyuma ya nyumba yake. Inasemekana marehemu alikuwa amefungwa mikono nyuma na (Ati) madaktari waliomchunguza wanasema kwamba shingoni kwake alikuwa na alama za mikono kamwa alikabwa Kibi kwanza kabla yakuwekwa kitanzi.

Wazanzibari wengi tuliosikia kifo chake tulisikitika sana na wale tulio ijuwa family yake hatukuweza kupata picha kama Azizi anaweza kujitundika mwenyewe. Ila kifo chake kinaambatana na utata wa Cheo chake alichokuwa nacho na asili yake anakotoka pamoja na Dini. Hakika Jeshi la Polisi Bara hawataki Zanzibar wawe na watu wazuri waliosoma katika nyadhifa za Polisi. Wao wanachotaka ni kuwaona Watu kama Kamander Mussa Juma ambae anaburuzwa.

Pili Azizi hakuwa kijana aliekuwa amehadaika na vyeo au cheo. Ni mtu alikuwa na kinaa pamoja na kujiamini na lile alilokuwa akilifanya. Kamander Azizizi anaambiwa kajinyonga mwenyewe. Lakini mtu aliejinyonga hawezi kujifunga kamba kwa nyuma.

Siku ya maziko yake tulitarajia Mkuu wa Polisi SIRO ahudhurie maziko yake lakini chakusikitisha ni Askari wachache sana wenye vyeo vya juu walihudhuria maziko yake.

Hata hivo Kwentu Sisi Wazanzibari haikutushuhulisha sana kwani wenyewe Tulitosha kwenda kumzika alhamdulilah . Allah amlaze mahali pema peponi, na kama amedhulumiwa basi Kamander Azizi atakuwa amekufa shahidi.

Watu wasiojulikana Sasa wameanza Stile mpya za Assacination na sio ile tulioifahamu katika kipindi cha nyuma cha tokea Utawala huu wa awamu ya tano kukaa madarakani.

Tukumbuke kwamba kuna watu wengi wasio hatia tayari wamepotea na wengine kushambuliwa kwa Risasi mchana kweupe na Serikali ya Magufuli imekaa kimyaa. Tunajuwa kwamba Polic-CCM wanatumika katika mauwaji na utekaji wa Watu wasio na hatia kwa vile tuu wanapingana na Utawala uliokuwepo.

Tunajuwa Kwamba bado kuna njama nyengine nyingi za utekwaji na Mauwaji unaandaliwa kwa ajili ya Viongozi wapizanni pamoja na wana sheria waliokuwa wamekataa kunyamazishwa.

Hata hivo Sisi Wazanzibari tunatakiwa tujiulize. Kwanini kifo cha mtu kama huyu kiwe kimyaa?

Kwanini hatuwezi kusema na kukemea. Inaonyesha kwamba sisi tumekuwa Wafu kiasi ya kwamba hata tuone maovu yanatendeka tunanyamaza kimyaa.

Tujuwe lilomfika mwezio leo huenda litakufika wewe kesho.

CHANZO: MZALENDO.NET
 
M

Mine eyes

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2016
Messages
3,968
Points
2,000
M

Mine eyes

JF-Expert Member
Joined Apr 11, 2016
3,968 2,000
Wazenji wakati mwingine wana chuki za kijinga tu mkuu.
Mtu anaeema eti jamaa kauwawa na watanganyika alafu sababu zenyewe za kitoto kabisa.

Wakati jamaa kajiuwa mwenyewe kabisa na ndyo msna hakuchezewa paredi la mazishi kwa sababu jeshi linakataa na hata sirro hakwenda baada ya kuthibitika alijiuwa.

Wazenji baadhi yao wana bifu za kijingaa,jamaa alijiuwa mwenyewe kwenye mabanda yake ya kuku nyumbani kwake,alikuwa amejitundika na kamba iko shingoni.

Alijiandaa hasa na hiyo siku alojinyonga simu aliacha ndani,na kuna rafiki yake alikuwa na kawaida ya kupiga nae stori baada ya swala ya usku,lakini siku hiyo akamuambia hayuko sawa amuache aende zake
Sasa jee jamaa alijua kama kuna watu wanakuja kumuua mpaka akatae kupiga stori na rafiki yake kama kawaida yao..?

Na huyo rafiki yake ndo alipigiwa simu mwanzo baada ya kuwa jamaa haonekani,akawaambia "nilionsna nae akaniambia hayuko sawa leo nimuachee"

Walipopiga simu yake wakaona inaita ndani na hapo ndo wakaanza kumtafuta wakamkuta kwenye mabanda yake kajinyonga.

Kauwawa vipi asipige kelele?
Watu wanakuja mpaka wanaondoka wasisikie vishindo kwamba kuna mtu anakabwa huko?

Na huo ukuta wa nyumbani kwake umefika ukauona ulivyo mrefu..?

Kiufupi alijjiuwa mwenyewe
Sipingani na mtizamo wako...

Labda mtoa mada ameelemea upande mmoja zaidi ila angalia pointi!
Wameshuhudia watu wa familia yake na wakasema walivyomuona kafungwa kamba mikono .hii ilikuwa kabla ya wewe kushuhudia na kuja kukanusha kwa uhakika!
Nadhani na wewe ni mmoja wa waliosikia...

Siungi mkono yote aliyosema mtoa mada ila na siko upande wowote na sitaki kubishana ila ukweli upo wazi...
Kwa mengi tu...
La muhimu ni kutoa vile vinavyotatiza... mengine ni dana dana!
Watanganyika zenj wapo wengi na .. ni vyema maana nchi ni moja.hata wapemba bara wapo wengi sana tu!
Muelewe mtoa mada kamaanisha nini...
 
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Messages
7,137
Points
2,000
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2017
7,137 2,000
Allah SW anasema sura 4:9

Na wachelee wale ambao lau kuwa na wao wangeli acha nyuma yao watoto wanyonge wangeli wakhofia. Basi nao wamche Mwenyezi Mungu, na waseme maneno yaliyo sawa.

Ikiwa huyo Marehemu alikuwa ni mcha Mungu na msema ukweli, Allah ametoa uhakikisho wa maisha ya hiyo familia yake wakati yeye ameshatangulia.

Allahu Aalam
Katika mjadala kama hii huwa siongei sanaaa, ndio kawaida yangu!

Anyway, tukumbuke tu mchuma janga hula na wakwao. Na pia dhulma haidumu.
 
Proved

Proved

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2018
Messages
5,123
Points
2,000
Proved

Proved

JF-Expert Member
Joined Sep 10, 2018
5,123 2,000
Taarifa hii ni ya kupuuzwa kwaa kiasi fulani.


Jamaa alijinyonga.hata familia inalijua hilo.

Kufungwa kamba ni jambo linasemekana tu ili kumtoa katika fedheha ya kujinyonga lakini ukweli hamna kamaba wala nini.

Mtu kama yule akamatwe afungwe kamba,akabwe alafu asipige kelele tu awe kimya tu..?

Kusema kwamba nyuma ya nyumba kulikuwa na hzo kama watu wanasisika wakikamata majani ni uongo tu wa kutaka kuwatoa watu kwenye reli kwamba jamaa alijinyonga.lakini inasemwa kwamba huwenda hicho kilichosikika ni ile purukubshani zake mwenyewe akijaribu kujinasua baada ya kujitundika na kupiga kelele ni ngumu hivyo lazima apapatike kwanza na hizo papara huwenda ndo walizosikia watu wakasema labda wavamizi

ALAMA za vidole zilizokutwa ni alama za vidole vyake mwenyewe ambayo alikuwa akijikamata kwa lengo la kujipapatua na kujitoa katika kitanzi baada ya kujitundika.

Ushahidi wote unaonesha kwamba alijinyonga,haiwezekani mtu kaama yule avamiwe alafu awe kimya tu uongo huo.

Sema wazanzibari kwa fitina siwawezi,wao kuitupia bara kila kitu sio ajabu sana.

sirro hakufika kwa sababu jamaa alijinyonga na kwamujibu wa jeshi mtu akijinyonga amedhalilisha jeshi na hastahiki kuzikwa kwa heshima.

Kwa chep chake jamaa sirro ilikuwa aje kabisa na timu maalum ya viongozi wa polisi wapige gwaride la heshima na timu hiyo iliandaliwa kabisa,lakini ilipothibitika kwamba kajinyonga mwenyewe kitu hicho kiliahirishwa moja kwa moja kutokana na kujinyonga kwakwe.

Viongozi waliokuja msibani walikuwa wao binafsi tu sio kiniaba ya kazi na chep cha marehemu,hyo ypte ni kutokana na kujinyonga kwake ni fedheha kwa jeshi na hata kidini pia aliyejinyonga ni kama kaua hvyo anakuwa kama kafanya uasi na anakosa baadhi ya stahiki zake.

Huwenda alirogwa mpaka ikapelekea kujinyonga,kama alirogwa basi dhambi ni za huyo aliyeroga.

Kama hakurogwa basi malipo yake yapo kwa Mola subhaana.
Dah!
 
D

dos.2020

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2009
Messages
2,399
Points
2,000
D

dos.2020

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2009
2,399 2,000
Mbona mkiambiwa alijiua mnapanick sana..haiwezekani au?

Jamaa alijiua.

Wewe una ushahidi gani kwamba ameuliwa?

Mimi nafahamu kwa mazingira ya kwake sio rahisi watu kumuua kimya kimya alafu wapande ukuta waondoke na yeyr asipige kelele kabisa.

Ukuta wa nyumba yake sio wa kuparamis kirahisi rahisi,na wala hakuna ushahidi wowote wa kuonesha kwamba ameuwawa.

Kama angrkuwa ameuwawa angechezewa paredi la heshima kwa mujibu wa cheo chakee.
Mkuu inaonekanwa unashindwa kufahamu hoja za watu kabisa. Wanaoushutumiwa kumuua ndio hao viongozi wake waliotuaminisha kama kajiua ili kuondoa utata wa kifo chake kwenye jamii. Sasa hilo Paredi atapigiwa vipi? na wao ndio wanataka tuamini kua amejiua?

Uhalisia unaendelea kubaki kua Kamanda Azizi alikua hakubaliki kwenye System ya CCM, na amekua akipingwa vita vya chinichini kwa miaka mingi sana tu na Wanasiasa wa CCM kwa ile hali yake ya kutokubali kupelekeshwa na CCM. Amekua akifanya kazi yake kama Askari Polisi na si Policcm kama walivo kina Sirro na Mussa Njino
 
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Messages
7,137
Points
2,000
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2017
7,137 2,000
Mkuu inaonekanwa unashindwa kufahamu hoja za watu kabisa. Wanaoushutumiwa kumuua ndio hao viongozi wake waliotuaminisha kama kajiua ili kuondoa utata wa kifo chake kwenye jamii. Sasa hilo Paredi atapigiwa vipi? na wao ndio wanataka tuamini kua amejiua?

Uhalisia unaendelea kubaki kua Kamanda Azizi alikua hakubaliki kwenye System ya CCM, na amekua akipingwa vita vya chinichini kwa miaka mingi sana tu na Wanasiasa wa CCM kwa ile hali yake ya kutokubali kupelekeshwa na CCM. Amekua akifanya kazi yake kama Askari Polisi na si Policcm kama walivo kina Sirro na Mussa Njino
Mkuu wewe ni mzanzibar na Gavana ni mzanzibar ambae ana uchungu na nchi yake. Huyo jamaa mnaebishana nae ni mamluki anaeishi Zanzibar na hajui lolote kuhusu Zanzibar.

Mimi nimempuuza muda sana maana nimemfuatilia nikamjua, na mbwa ukishamjua jina hakusumbui tena
 
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2017
Messages
7,137
Points
2,000
Relief Mirzska

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Joined Jun 13, 2017
7,137 2,000
Nashukuru Mungu kwa kuniepusha na kazi hii ya kinanga
Nilikuwa napenda kuwa askari (mwanajeshi) wakati nipo mdogo kwa kuamini kwamba ntakuwa natetea watu.

Baba yangu akaniambia sitakuwa na radhi zake nkienda kwenye kazi hizo.

Nkaachana nazo kabisa na Leo najionea namna ambavyo hizo kazi zina laana
 

Forum statistics

Threads 1,326,837
Members 509,593
Posts 32,236,901
Top