Nani aliyefanya haya yafuatayo?

Nani aliyefanya haya yafuatayo?

Hoja ni vimejengwa kwa muda kiasi gani? Bila shaka ni miaka zaidi ya 50.

Halafu zimetumika fedha kiasi gani ukilinganisha na ubora wa miradi hiyo? Ufisadi uliokithiri, Ufadhili na mikopo.

Wakati wa Magufuli hakuna ufisadi, mikopo wala ufadhili. Hicho ndo tunajivunia. Hatua zinachukuliwa waziwazi.
Huyu ndiye kawazidi udisadi wenzie wote waliotangulia. Hujui kuwa kuna Tsh 2.4 Trillion haionekani imetumikaje kutokana na hoja za CAG?.
Lazima muvae miwani ya mbao ambayo hamuoni anavyo vuruga mfumo ili kujipatia rushwa. Amenunua ndege bila kufuata sheria za manunuzi ili apate 10%.

Amehamishia shughuli za ATCL toka Wizara ya uchukuzi kwenda Ikulu ili CAG asihoji na ametunga sheria ya madini inayo mzuia CAG kukagua shughuli za madini.

Kama huwezi kuyaona haya kuwa ni systemic grand instututional corruption utakuwa ni mlemavu wa akili. Hatuna dawa kwa kilema hicho
 
1. Ujenzi wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam?
2. Ujenzi wa Barabara ya Dar mpaka Moro?
3. Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa JNIA?
4. Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa KIA?
5. Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Mwanza?
6. Ujenzi wa barabara ya Chalinze hadi Segera?
7. Ujenzi wa Chuo Cha Taaluma za Kijeshi- Monduli?
8. Ujenzi wa Jengo Jipya la Bunge-Dodoma?
9. Ujenzi wa Barabara ya Moro-Dodoma?
10. Ujenzi wa Bandari ya Tanga?
11. Ujenzi wa bandari ya DSM/
12. Ujenzi wa barabara ya Moro-Iringa?
13. Ujenzi wa bandari ya Mtwara?
14. Ujenzi wa uwanja wa ndege wa Songwe?
15. Ujenzi wa Uwanja wa ndege wa Arusha?
16. Ujenzi wa Daraja la Mkapa?
17. Ujenzi wa Chuo kikuu cha Dodoma?
18. Ujenzi wa uwanja wa mpira wa Uhuru
19. Ujenzi wa Chuo kikuu cha kilimo Sokoine?
20. Ujenzi wa Chuo kikuu cha Mzumbe?
21. Ujenzi wa hospitali ya AMANA?
22. Ujenzi wa Hospitali ya Muhimbili?
23. Ujenzi wa Hospitali ya Mwananyamala?
24. Ujenzi wa Hospitali ya Temeke?
25. Ujenzi wa Hospitali ya Tumbi?
26. Ujenzi ya Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya nyanda za juu kusini?
27. Ujenzi wa Hospitali ya Benjamen-Mkapa- DODOMA?
28. Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mawenzi-Kilimanjaro?
29. Ujenzi wa Barabara ya Arusha-BABATI, MAKUYUNI-KARATU, KARATU-NGORONGORO?
30. UJENZI WA HOSPITALI YA SEKOU TOURE -MWANZA?
31. ujenzi wa MOUNT-MERU HOSPITAL YA MKOA WA ARUSHA/
32. UJENZI WA DODOMA GENERAL HOSPITAL?
33. UJENZI WA MLOGANZILA HOSPITAL?
34. UJENZI WA BARABARA YA DAR-MTWARA?
35. UJE NZI WA HOSPITALI YA MKOA WA TANGA- BOMBO?
36. UJENZI WA CHUO KIKUU CHA ARDHI?
37. UJENZI WA IFM?
38. UJENZI WA MWALIMU NYERERE MEMORIAL ACADEMY?
39. UJENZI WA VYUO VYA WALIMU KILA KANDA NA MIKOA?
40. UJENZI WA BARABARA YA DODOMA-IRINGA?
41. UJENZI WA BARABARA YA ARUSHA-NAMANGA?
42. UJENZI WA BARABARA YA SEGERA-TANGA?
43. UJENZI WA BARABARA YA DODOMABABATI?
44. UJENZI WA UWANJA WA NDEGE WA DODOMA, IRINGA, BUKOBA ETC.
45. UJENZI WA HOSPITALI YA MKOA WA LINDI-SOKOINE?
46. UJENZI WA HOSPITALI YA MKOA WA MBEYA-MBEYA RUFAA?
47. UJENZI WZA HOSPITALI YA MKOA WA KIGOMA-MAWENI?
48. UJENZI WA HOSPITALI YA MKOA WA SINGIDA?
49. UANZISHWAJI WA BARAZA LA TAIFA LA MITIHANI?
Duh!! halafu yoote haya yalifanyika na watumishi waliongezewa mishahara yao kila mwaka bila tatizo lolote kuliko yanayotokea sasa.
 
50. Ujenzi wa chuo cha Jeshi- Msata?
51. Ujenzi wa Chuo cha polisi-CCP-MOSHI?
52. Ujenzi wa shule za msingi kwa kila kijiji?
53. Ujenzi wa shule ya sekondari za O-level kwa kila kata?
54. Ujenzi wa shule za sekondari za A- level kwa kila Tarafa na Wilaya?
55. Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha la Mtera?
56. Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Kihansi?
57. Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Nyumba ya Mungu?
58. Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Kidatu?
59. Ujenzi wa Bwawa la kuzalisha umeme la Hale?
60. Ujenzi wa Mtambo wa kuzalisha umeme wa gesi pale UMEME PARK-UBUNGO SIO SONGAS.
61. Ujenzi wa kiwanda cha cement cha Twiga cement?
62. Ujenzi wa kiwanda cha nguo cha urafiki?
63. Ujenzi wa kambi ya mafunzo ya kijeshi-Dodoma?
64. Ujenzi wa reli ya TAZARA?
65. Ujenzi wa bomba la Mafuta- TAZAMA?
66. Uanzishwaji wa TANESCO kama shirika la Umeme?
67. Ujenzi wa shirika la karakana ya Jeshi- Nyumbu?
68. Uanzishwaji na ujenzi wa vituo vikuu vya polisi kila mkoa na wilaya?
69. Ujenzi wa Kambi za JKT karibia kila mkoa-TANZANIA?
70. Ujenzi wa Majengo ya Mahakama za hakimu mkazi kila mkoa?
71. Ujenzi wa majengo ya mahakama kuu kila kanda?
72. uanzishwaji wa sarafu yetu baada ya bank ya EAC kuvunjika 1966?
73. Uanzishwaji wa bank kuu ya Tanzaznia?
74. Uanzishwaji wa Range za TAIFA?
75. Ujenzi wa Barabara ya SIngida-tabora?
76. Ujenzi wa barabara ya Nzega- MWANZA?
77. Ujenzi wa barabara ya Mwanza-Musoma-SIRARI?
Halafu unasikia Mzee Mwinyi akijishusha na kumsifia jiwe eti amefanya mengi kuliko waliyofanya wao wanne ukiwaweka pamoja. Huu ni upuuzi wa kupitiliza
Kwa mara ya kwanza mnakiri kwa vinywa vywenu kuwa. Toka chama cha mapinduzi kiiongoze serikali kuna mengi kimeyafanya aksanteni sanaa
 
Eti nikitoka hakuna wa kuyaendeleza, ndege, standard gauge stiegersgorge, Hivi Nyerere, Mwinyi, Mkapa, Kikwete waliyoanzisha yaliendelezwa na nani? Nahaya anayoyazindua kila siku yalianzishwa na nani?
 
Halafu unasikia Mzee Mwinyi akijishusha na kumsifia jiwe eti amefanya mengi kuliko waliyofanya wao wanne ukiwaweka pamoja. Huu ni upuuzi wa kupitiliza
Mwinyi na Mama Maria Nyerere siyo wa kuhojiwa mara kwa mara.
 
Back
Top Bottom