Nani aliimba huu wimbo....mtu chake apendacho

lokiyo

JF-Expert Member
Joined
Dec 17, 2010
Posts
1,953
Reaction score
884
Wakuu nataka nani au ni bendi gani iliimba huu wimbo wa mapenzi haya kificho yanapoingia moyoni...Mtu chake apendacho, hakina hila machoni, huridhika kuwa nacho japo hakina thamani:sleepy:
 
Gurumo na bitchuka..ngoja wenye mambo yao waje wakupe data zaidi
 
Wakuu nataka nani au ni bendi gani iliimba huu wimbo wa mapenzi haya kificho yanapoingia moyoni...Mtu chake apendacho, hakina hila machoni, huridhika kuwa nacho japo hakina thamani:sleepy:

Mwimbo huu kauimba mdada anaitwa Miriam Mwinjuma wa Jahazi Modern Taarab.
Wimbo unaitwa ***** ***** mchokoe pweza.
"Mtu chake apendacho hakina hila machoni,hukiganda hikohiko hata mumfanyie nini"
 
We unaonekana ni kizazi cha dot com. Wimbo huo asili yake ni wimbo wa dansi. Uliimbwa na Sikinde DDC Mlimani park. Gurumo ana shairi lake lasema'mapenzi hayana kificho,yaingiapo rohoni mwangu,mwenye mapenzi haoniii,ingawa macho anayoooo... Huyo wa taarab kakopy na ku paste juzijuzi tu hapa.
 
Nitake radhi, kwa umri wangu wa miaka 54 unaniita wa dotcom!!!!
Nitake radhi nakwambia ewe kijana Swat
 
Last edited by a moderator:

Akikutaka radhi ntamshangaa sana, kama kweli wewe sio kizazi cha dot com iweje utoe comment ya kuwa huo wimbo ni wa taarabu. Wote wa mwaka 47 wanajua origin ya wimbo huo ni Sikinde na mwimbaji ni Hassan Bichuka na Muhidin Gurumo "The late". Wewe mtake radhi mrusha uzi huu kwa kujaribu kupotosha ukweli
 
Mbona wavamia masusu kwa mambo yasokuhusu mkuu?
Au usiku wa leo ulinikamia?
Mtoa uzi aliposema hajauona YouTube ndo nami nikajaribu kusema labda ndo ule wa Jahazi.
Simtaki radhi maana sijapotosha ila nimeuweka mwingine unaofanana nao.
 
Nitake radhi, kwa umri wangu wa miaka 54 unaniita wa dotcom!!!!
Nitake radhi nakwambia ewe kijana Swat

Mkuu nikiri sijui umri wako. Lakini mazingira ya comment yako yameonesha wewe hata kama una miaka 54 si mfuatiliaji miziki mbalimbali. Ungekuwa mfuatiliaji ungegundua wimbo huo upo toka miaka ya 80's. Enzi za Radio Tanzania.Hiyo taarabu imetungwa mwishoni mwa mwaka jana 2013,au mwanzoni mwaka huu 2014!. Ndio mana nikahisi wewe ni dot.com.
 
Last edited by a moderator:
Wimbo Mzuri sana bichuka alilia kuna siku alipokuwa anafanya mahojiano na gamba hizi nazo ijumaa radio one.
 
Mwimbo huu kauimba mdada anaitwa Miriam Mwinjuma wa Jahazi Modern Taarab.
Wimbo unaitwa ***** ***** mchokoe pweza.
"Mtu chake apendacho hakina hila machoni,hukiganda hikohiko hata mumfanyie nini"

Nakuaminia Shem!!
 
Mkuu nikiri sijui umri wako. Lakini mazingira ya comment yako yameonesha wewe hata kama una miaka 54 si mfuatiliaji miziki mbalimbali. Ungekuwa mfuatiliaji ungegundua wimbo huo upo toka miaka ya 80's. Enzi za Radio Tanzania.Hiyo taarabu imetungwa mwishoni mwa mwaka jana 2013,au mwanzoni mwaka huu 2014!. Ndio mana nikahisi wewe ni dot.com.

Nimekusamehe.
Unajua nini mkuu, mie si mtu wa kuzifuatilia hizi nyimbo saaana, mie zangu ni za akina Mayaula Mayoni, Papa Wemba, Bilekompasi, Loketto....halafu nilikuwa napenda sana kuruka majoka enzi za Bilicanas kwa Mbowe....kwenye viunga vya akina marehemu mzee kikofia.
 
We unaonekana ni kizazi cha dot com. Wimbo huo asili yake ni wimbo wa dansi. Uliimbwa na Sikinde DDC Mlimani park. Gurumo ana shairi lake lasema'mapenzi hayana kificho,yaingiapo rohoni mwangu,mwenye mapenzi haoniii,ingawa macho anayoooo... Huyo wa taarab kakopy na ku paste juzijuzi tu hapa.

mhhhjj aiseee umekula chumvi nyingi
 
Nimekusamehe.
Unajua nini mkuu, mie si mtu wa kuzifuatilia hizi nyimbo saaana, mie zangu ni za akina Mayaula Mayoni, Papa Wemba, Bilekompasi, Loketto....halafu nilikuwa napenda sana kuruka majoka enzi za Bilicanas kwa Mbowe....kwenye viunga vya akina marehemu mzee kikofia.

Nashukuru kwa kunisamehe.Ila tena umefanya kosa jingine. Bilicanas imeanza kuitwa hivyo juzijuzi. Zamani wakati sisi tukiingia ilikua ikiitwa Mbowe Club. Itabidi nikutafute nikusimulie mengi ya zamani ha ha ha!
 
Huoni nimetaja kwa Mbowe mkuu?
hakuna shida mkuu.
Nipo na nimejaa tele.
sijajua ulipo ila kama uko Dar, baadae tungeenda bonanza Leaders Club.
 
Wakuu nataka nani au ni bendi gani iliimba huu wimbo wa mapenzi haya kificho yanapoingia moyoni...Mtu chake apendacho, hakina hila machoni, huridhika kuwa nacho japo hakina thamani:sleepy:

Mapenzi hayana kificho yaingiapo moyoni, mwenye mapenzi haoni ingawa macho anayo
 
Back
Top Bottom