Nani alaumiwe?

Mkeshaji

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2011
Posts
4,258
Reaction score
1,418
Heri ya mwaka mpya wanabodi,
Nilikuwa safarini kuelekea mikoa ya kusini kwa mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka.
Nikiwa katikati ya safari niliona giza limeshaanza kuingia hivyo nikaona nitafute nyumba ya wageni nipumzike usiku huo ili siku iliyofuata nimalizie kipande cha safari iliyobaki. Basi nikafanikiwa kupata chumba katika mojawapo ya nyumba za wageni mahali hapo.

Nikiwa nimejipumzisha chumbani majira ya saa 6 hivi usiku nikasikia kitu kama zogo hivi (nje ya chumba changu lakini ndani ya guest). Ikabidi nitoke. Pale kwenye korido niliwakuta watu wanne: jamaa wawili wanaume wa miaka kati ya 40-45 ambao sikuwafahamu, binti mmoja apata miaka 15-17 hivi pia sikumfahamu, na wa nne alikuwa dada muhudumu wa ile guest ambaye ana chumba chake mle ndani.
Sasa baada ya kudadisi na kufuatilia ndiyo nikagundua ilikuwa hivi:

Wale jamaa wawili walikuwa na safari ya kibiashara kwenda mikoa hiyo ya kusini. Mmoja kati ya hao jamaa ameoa dada wa kutoka mikoa hiyo ya kusini. Sasa kwa kuwa huyu jamaa alikuwa anaelekea huko nyumbani kwa mkewe (japo kibiashara) basi mkewe akamkabidhi mdogo wake wa kike (yaani shemeji yake huyu jamaa sasa, ambaye ndo yule mwenye miaka 15-17) ampeleke nyumbani kijijini kwani shule zilikuwa zimefungwa.

Walipofika hapo waliamua kulala (kwa sababu wanazozijua wao). Sasa huyu jamaa aliyekabidhiwa binti akachukua chumba kimoja na akawa anamwambia yule binti naye akalale huko kwani yeye hakuwa na hela ya kukodi chumba kingine. Na hicho chumba kilikuwa ni singo (Kumbuka mimi nilifika hapo baada yao na nilipata chumba na bado vingine vilikuwepo). Binti akawa anagoma. Jamaa akalazimisha sana, lakini binti akashikilia msimamo. Jamaa akamwambia binti kama hutaki basi utalala hapo hapo nje mimi sina hela ya kukodi chumba kingine.

Basi binti akajikunyata hapo uani huku analia. Ndipo muhudumu wa guest katika mishe mishe zake akamkuta. Kumuuliza vipi, binti akamwelezea A-Z. Muhudumu akamwamsha yule jamaa mwingine sasa na kumwelezea hiyo ishu. Basi jamaa akampaka yule jamaa kinoma (Hawa jamaa wanatokea mikoa ya kanda ya ziwa na walikuwa wanaongea kilugha lakini niliweza kubaini japo kwa lugha ya picha). Ndo hilo zogo lililoniamsha.

Yule jamaa mwingine (siyo shemeji wa binti) ikabidi atoe hela kumkodia binti chumba, ndo binti akaenda kulala. Saa hiyo ilikuwa yapata saa nane kasoro usiku. Ilibidi tumsihi huyu jamaa mwingine a-take care ya binti maana kwa hali ile tulihisi kama chui kapewa kazi ya kumpeleka mbuzi malishoni.

Asubuhi yake mi niliamka mapema sana ili kuendelea na safari yangu. Kilichojili huko nyuma sikujua, japo nilibaki najiuliza: Nani alaumiwe?

True story.
 
Nani alaumiwe kwa lipi? ndani ya hadithi yako hata wewe tunaweza kukulaumu. Jaribu kuweka swali vizuri mjadala uwe wa mlengo mmoja.
 
Nani alaumiwe kwa lipi? ndani ya hadithi yako hata wewe tunaweza kukulaumu. Jaribu kuweka swali vizuri mjadala uwe wa mlengo mmoja.

Daddy me nahisi anauliza nani alaumiwe kati ya mke ( dada wa yule binti) au mume (shemeji wa yule binti).......
 
Mambo ya shemeji hayoo! Anataka kula kuku na mayai, yaani hapa siyo nani alaumiwe bali ni funzo kwmb lo wanaume hawaaniki hata kidogo!!!(Baadhi)
 
Nani alaumiwe kwa lipi? ndani ya hadithi yako hata wewe tunaweza kukulaumu. Jaribu kuweka swali vizuri mjadala uwe wa mlengo mmoja.
Sasa mi nilaumiwe kwa lipi hapo?
Na ni kwa nini mjadala uwe wa upande mmoja? Nadhani ni vema kuuacha wide hivi.
 
Daddy me nahisi anauliza nani alaumiwe kati ya mke ( dada wa yule binti) au mume (shemeji wa yule binti).......
Yes indeed. Lakini kwa anayesema mi napaswa kulaumiwa, basi ni vema akatoa sababu.
 
Daddy me nahisi anauliza nani alaumiwe kati ya mke ( dada wa yule binti) au mume (shemeji wa yule binti).......

okay daughter thanks....
tukijikita katika perception hiyo basi wa kulaumiwa ni huyo mwanaume, tokea lini mwanaume tena mfanyabiashara ukashindwa kumlipia shemejiyo sehemu ya kulala.
Kama hakupewa hela ya malazi kwa nini hakugoma kuondoka na huyo binti.
Huyo jamaa ni mkware tu alikua anajitengenezea mazingira ya kumgegeda shemjiye, usheitwan tu ulimjaa.
 
Alaumiwe huyo mume wa mtu aso haya wala asojua vibaya, ye kupewa tu binti amsindikiize imekua nongwa, angepewa mtoto wa kike mdogo huyo angekua kashamuharibu vibaya
 
Sasa mi nilaumiwe kwa lipi hapo?
Na ni kwa nini mjadala uwe wa upande mmoja? Nadhani ni vema kuuacha wide hivi.

eenh afadhali umekuja mkuu...ishu ni hivi, huyo binti ni chini ya miaka 18, kisheria huyo bado ni mtoto. Watoto hulindwa na haki za msingi ambazo kisheria kila mtu anapaswa kuzingatia. Ulichoshuhudia wewe ni kuona haki hiyo inatenguliwa na wewe kutochukua hatua yoyote walau hata kuvishirikisha vyombo vya usalama.
Nikuulize swali, sasa hivi umeleta taarifa JF...je unadhani imemsaidia vipi yule binti???
 
Alaumiwe huyo mume wa mtu aso haya wala asojua vibaya, ye kupewa tu binti amsindikiize imekua nongwa, angepewa mtoto wa kike mdogo huyo angekua kashamuharibu vibaya
Hata huyo aliopewa pia mbona naye alikuwa ni mdogo tu. Nadhani huyu jamaa alikuwa anammendea huy mtoto tangu huko home sema hapa alipata upenyo tu. Na huenda yeye ndo alilazimisha kumsindikiza yule binti kwao.
 
Wewe sasa naona unanichenjia!
Kiufupi yule jamaa mwingine alishajikomit kuhandle hiyo ishu. na kwa kuwa mimi nilikuwa na tite schedule nikaona basi ni jambo la busara kuiacha hiyo ishu kwa jamaa yule kwani nilimwona ni muungwana tofauti na mwenziye.

Kumsaidia au kutomsaidia yuele binti is another ishu, lakini kwa kuileta hapa nina uhakika itakuwa imeisaidia jamii hii, wewe ukiwa mmoja wapo na balozi katika hili.
 
Hata huyo aliopewa pia mbona naye alikuwa ni mdogo tu. Nadhani huyu jamaa alikuwa anammendea huy mtoto tangu huko home sema hapa alipata upenyo tu. Na huenda yeye ndo alilazimisha kumsindikiza yule binti kwao.

atlist huyo anaufahamu hadi ameweza kukataa pata picha angekua 5 years old
 
atlist huyo anaufahamu hadi ameweza kukataa pata picha angekua 5 years old
True.
Sasa hapa kuna somo jingine.

Je ninyi wanawake, waume zenu wapo hivyo mnavyowaamini?
 
hapo alaumiwe huyu dogo kwanini kama angekuwa anania mbaya nae angepiga kelele jamaa angekula miaka 30 fasta kwa kosa la kubaka ila kutokana dada anampenda dadake akaamua kupotezea kiivo..
 

Sio kuwa nakunanga bali najaribu kukufanya ufikirie nje ya box pia...
Leo hii hebu fikiria unakutana na gazeti ukurasa wa mbele kabisa unaona picha ya yule binti kabakwa na huyo shemeji yake....najua moyoni utajuta kwa kuwa kuna hatua ulisita kuichukua.
 
True.
Sasa hapa kuna somo jingine.

Je ninyi wanawake, waume zenu wapo hivyo mnavyowaamini?

u cant generelize kua wapo hivyo bt as long as huyo mume ni mtu mzima decision anayo mwenyewe na kuepuka tamaa zake
 
hapo alaumiwe huyu dogo kwanini kama angekuwa anania mbaya nae angepiga kelele jamaa angekula miaka 30 fasta kwa kosa la kubaka ila kutokana dada anampenda dadake akaamua kupotezea kiivo..

we nawe, apigie makelele koridoni makubwa, bint hata rum hajatinga hizo kelel angempigia nani sasa
 
hapo alaumiwe huyu dogo kwanini kama angekuwa anania mbaya nae angepiga kelele jamaa angekula miaka 30 fasta kwa kosa la kubaka ila kutokana dada anampenda dadake akaamua kupotezea kiivo..
Kweli mkuu.

Wapo watu/mabinti ambao wananyanyaswa lakini kwa kuogopa ama kuvunja uhusiano wa upande fulani au kubadilishiwa kubao pindi watakapovujisha ishu basi huamua kukaa kimya huku wakiendelea kuathirika.

Haya mambo hata majumbani yamejaa sana.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…