Hapo cha kwanza kabisa ni wazazi kushindwa kutimiza wajibu wao wa kulea, kutoa matumizi nk kutokana na maisha kuwa magumu kwa sasa. Unakuta mzazi anaondoka asubuhi kwenda kutafuta riziki, akirudi anapitia kwenye kahawa, bar, mchepuko nk kurudi nyumbani saa 6 usiku watoto wote wamekwisha lala, sasa hapo watoto wakianza tabia mbaya siyo rahisi kugundua na kuchukua hatua.