Nani ajibu maswali ya moto shuleni

Rwey

Senior Member
Jul 11, 2008
121
23
Matukia ya shule za bweni kuungua moto yanazidi kuongezeka nchini, jambo linalotia wasiwasi wazazi ambao wanapenda watoto wao wasome shule za bweni. Yapo matukio mengi ya shule kuungua; nikukumbushe kidogo tu matukio ambayo yameshatokea mwaka huu na kuripotiwa na vyombo vya habari:

‘Bweni la wasichana katika Shule ya Sekondari Mkalamo, wilayani Korogwe limeteketea tena kwa moto pamoja na mali zote za wanafunzi zilizokuwamo. Lilikuwa tukio la pili kutokea shuleni hapo. ‘Mabweni ya shule ya Sekondari ya wasichana ya Bigwa inayomilikiwa na Masista wa Kanisa Katoliki Jimbo la Morogoro yateketea kwa moto’.

‘Shule ya Sekondari ya Binti Mussa iliyopo katika Kata ya Kiwalani yateketea kwa moto uliosababishwa na hitilafu za umeme’. 'Sekondari ya Mawenzi yaungua moto’, ‘Mabweni ya wavulana katika shule ya sekondari ya Kikatiti wilayani Arumeru mkoani Arusha yameteketea kwa moto na kusababishara hasara ya mamilioni ya fedha’.

Yapo matukio mengi ya namna hiyo na ya wiki chache zilizopita ni Machame ambayo mabweni yake yaliungua moto na Lugoba ambayo nayo moto umeunguza mabweni mara mbili. Nimelazimika kutoa mifano hiyo michache angalau msomaji uone namna gani maisha ya watoto wetu wanaosoma katika shule za bweni yalivyo hatarini.

Kuna mambo mengi ya kujiuliza, kwa nini matukio hayo ya moto shule hizo madarasa hayaungui? Kwa nini ni mabweni tu ndiyo yanayoungua? Naamini ni maswali ambayo kwa haraka hayawezi kupata majibu. Kutokana na matukio ya namna hii hofu kubwa imeanza kutanda hasa kwa wanafunzi wenyewe ndiyo maana nasema kwamba kuna haja ya kuchukua hatua za kutokomeza hali hiyo.

Haifurahishi hata kidogo kwa mwanafunzi ambaye anatakiwa asome kwenye mazingira ya utulivu anapokuwa na hofu ya kuzuka moto ambao unahatarisha maisha yake. Ni matukio ambayo yamekuwa yanatokea mara kwa mara, lakini katika siku za hivi karibuni yameongezeka. Nani anahusika na hali hiyo na makusudi yake ni nini?

Wanandugu naomba tuzungumzie hili suala..
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom