Samahani sana kama ntakuhudhi,
haya ni maoni yangu toka moyoni na sikushawishiwa na mtu yoyote:
Nikili kwamba mimi ni Mwanachama hai wa CCM na si utani. Chama nilikipenda toka moyoni, Ila kwa kwa sasa nabwaga manyanga Rasmi mimi si mwanachama tena wa CCM. Nilijiunga na CCM Mwaka 1999 nikiwa Form 4 hapo jijini DSM tena kwa Moyo mmoja kwa kadi No.1267...., tena kutokana na Mapenzi yangu ya dhati kwa Mwl. JK NYERERE. Na alipokufa nilisikitika sana tena sana, nakumbuka kipindi hicho nilikuwa najiandaa na Mitiana ya Form 4 na tena nilikuwa naumwa typhod kali sana na kidogo iniue! Ila nilijikongoja toka kitandani mpaka pale maeneo ya sanyansi enzi hizo pakijulikana Maji machafu kushuudia mwili wa mwalimu JK NYERERE ukipitishwa hapo. Kiukweli nililia sana na nkazidiwa na kukimbizwa hospital baada ya kuzidiwa ghafla na jua kali lililokuwa limenichapa. Nashukuru mungu aliniepusha na kifo.
SABABU ZA KUTOKA CCM:
1. Jana nimepata tena mshutuko wa ajabu baada ya kusikia kuwa chama changu (CCM) kilihusika katika kifo cha Mshawishi wangu wa kujiunga na CCM (JK NYERERE), kweli nimeumia sana.
2. Hii imepelekea nianze kuanimi maneno ya wapinzani kuwa CCM ni chama cha wauaji, achilia mbalil maswala ya UFISADI, maana Tanzania bila ufisadi haiwezekani, ndo maana kila mtu ni fisadi katika ofisi yake, na hakuna anayeweza kulipinga, maana bila ufisadi hakuna hata mmoja nayeweza kujenga kwa kutumia mishahara yetu. Nisingependa kuegemea katika swala la ufisadi.
3. Hii imenipele niamini kuwa chanzo cha vifo vya watu mbali mbali ndani ya CCM ni Mkono wa CCM wenyewe! Ntatoa mifano Hai:-
(a) Kifo cha Kigoma Malima, Utata Mtupu mpaka leo..........Mhusika ni CCM
(a) Kifo cha Kombe, Utata Mtupu mpaka leo......................Mhusika ni CCM
(b) Kifo cha Sokoine, Utata mtupu mpaka leo....................Mhusika ni CCM
(c) Kifo cha Daudi Balal, Utata Mtupi mpaka leo...................Mhusika ni CCM
(d) Kifo cha Amina Chifupa Utata mtupu mpaka leo............Mhusika ni CCM
(e) Kifo cha Aman Abeid karume Utata mtupu mpaka leo....Mhusika ni CCM
(f) Kifo cha Omary Ally Juma Utata mtupu mpaka leo ........Mhusika ni CCM
(g) Kifo cha JK NYERERE nacho leo wanasema ...................Mhusika ni CCM
Na sasa kuna maneno mengine juu ya ugonjwa wa Dr. Mwakyembe na Prof Mwandosya kuwa chanzo ni CCM, Jamani kwanini niendelee kuwa mwanachama wa chama hiki? Tafadhali wana CCM Mliokuwa wenzangu nipeni ushawishi wa kutosha wa kwanini nibaki katika hiki chama na Wapinzani nipeni sela zenye mashiko ya kujiunga na chama chenu la sivyo nakaa bila kuwa mwanachama wa chama chochote katika maisha yangu yote kuanzia leo.
KAPT. KOMBA ALIPATA WAPI TAARIFA MPAKA KUTUNGA NYIMBO ZA MAOMBOLEZO ALBAM NZIMA NA KUIREKODI, ALIJUAJE KAMA JK NYERERE ATAKUFA? PIA NINA WASI WASI NA KAPT KOMBA ALIJUA MPANGO MZIMA WA KIFO CHA UYU MZEE WETU WA TAIFA.
"NIMEUMIA SANA NA HABARI HII YA MKAPA KUHUSIKA KATIKA KIFO CHA JK.NYERERE NA IMENITOA RASMI CCM"
"MUNGU MLAZE PEMA MWL. JK NYERERE NA TUNAMPENDA SANA, WOTE WALIOHUSIKA WATAHUKUMIWA HAPA HAPA DUNIANI NA UMPE NGUVU MAMA MARIA NYERERE NA FAMILIA YAKE ASIDANGANYIKE KUUKANA HUU UKWELI MAANA WATAMWANDAMA SANA KUPITIA TBC ILI AYAKANE NA KUMKANA V. NYERERE KUWA SI MWANA FAMILA NA AMEKURUPUKA"
"NA MPAKA SASA HAJAKANUSHA"
MyTake:
Changia bila kutukana.