Nane Nane ilivyo sasa ni tukio la kisiasa zaidi, wala halina nia ya kuboresha Kilimo. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nane Nane ilivyo sasa ni tukio la kisiasa zaidi, wala halina nia ya kuboresha Kilimo.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Jul 17, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tangu sherehe za Nane Nane zimeanzishwa ni muda mrefu sana sasa.Nitakuwa mwongo nikisema nakumbuka mwaka zilipoanzishwa rasmi,kwa kweli sikumbuki.Wana JF nisaidieni.Lakini swali la msingi ni hili: Hivi kweli sherehe za Nane Nane zinaweza kuchangia kuboresha kilimo chetu?Kwangu mimi jibu ni hapana.

  Kwa nini jibu hapana.Kuna sababu kuu mbili au tatu za msingi nionazo mimi.Moja ni kwamba ni wakulima wachache sana wanaohudhuria sherehe hizi.Wengi wanaokwenda kule ni wakazi wa mijini ambao kusema kweli sio wakulima hasa.Hawa sherehe za Nane Nane ni sehemu ya burudani tu,kutembea na kuona Simba,vichwa vya watu visivyo na viwiliwili vikiongea,kununua bidhaa n.k..Nia hasa sio kuona na hatimaye kuboresha Kilimo!

  Pili,serikali haichukulii maanani sherehe hizi hasa.Hii inanikumbusha slogan ya "KILIMO KWANZA." Hii yote ni mikakati ya kisiasa tu ambayo inakusudia kupata political gains zaidi kuliko kupata maendeleo halisi ya wanachi.Kwa hiyo fedha zinazotengwa zinakuwa kidogo mno, kiasi kwamba maandalizi yake yanakuwa hafifu sana.Katika hali hiyo, haiwezekani kabisa kupata matokea yanayokusudiwa.

  Ushauri wangu kwa serikali ni kwamba,kama ina nia ya dhati ya kuboresha Kilimo,basi itadhmini impact ya sikukuu ya Nane Nane katika kuboresha Kilimo mpaka kufikia sasa,kwa vile ni muda mrefu sasa umepita tangu ianzishwe.Kama ikionekana hakuna impact yeyote, ni vema ikafanya utafiti wa kina kujua kwa nini hakuna impact, ili iangalie uwezekano wa kuiboresha na hatimaye impact inayo kusudiwa ipatikane.Na ikionekana kwamba hakuna uwezekano wa kuiboresha ili malengo yaliyo kusudiwa yafikiwe,basi ni vema ikasitishwa,kuliko kufanya mambo ambayo hayana faida, yanayopelekea kupoteza fedha za wanachi bure.
   
 2. Sanjara Honey

  Sanjara Honey Member

  #2
  Jul 17, 2009
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 63
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 15
  Kama hiyo 8-8 iko kisiasa, jindae kushiriki/kuhudhuria Tanzania honey Expo ambayo iko kibiashara zaidi.

  Gonga hapa Tanzania Honey Expo

  [​IMG]
   
Loading...