Nancy Pelosi: Kumzuia Tramp kuanzisha vita na Iran ni kwa maslahi ya Marekani

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
May 31, 2018
8,638
16,568
Pelosi: Kumzuia Trump kuanzisha vita dhidi ya Iran ni kwa maslahi ya Wamarekani

Feb 14, 2020 12:01 UTC

[https://media]

Spika wa Bunge la Wawakilishi katika Kongresi ya Marekani, Nancy Pelosi, ametoa taarifa baada ya kupitishwa azimio la Baraza la Seneti la kumuwekea vizingiti rais wa nchi hiyo kuhusu kuanzisha vita dhidi ya Iran.

Katika taarifa yake, Pelosi amesema: "Bara la Seneti kwa kupitisha azimio kuhusu uwezo wa kuanzisha vita, limeungana na Baraza la Wawakilishi na limetekeleza majukumu yetu kama Kongresi ya Marekani kwa lengo la kulinda usalama wa watu wa Marekani."

Pelosi ameongeza kuwa: "Uamuzi huo ambao unaweka vizingiti kuhusu kuanzisha uhasama na Iran bila kushauriana na Kongresi pia utalinda maisha ya wanajeshi, wanadiplomaisa na maafisa wengine wa Marekani."

Pelosi amesema hivi sasa zaidi ya wanajeshi 100 wa Marekani wamepata majeraha mabaya ya ubongo baada ya Iran kuvurumisha makombora katika kituo cha jeshi la Marekani cha Ainul Assad nchini Iraq lakini Donald Trump anasema kilichowasibu wanajeshi wa Marekani ni maumivu ya kichwa tu.

[https://media]Baraza la Seneti

Spika wa Baraza la Wawakilishi la Marekani amesema Trump anapaswa kusikiliza matakwa ya Kongresi na watu wa Marekani kwani Marekani na dunia haiwezi kustahamili vita tena.

Siku ya Alhamisi Baraza Seneti la Marekani lilipitisha azimio la kupunguza uwezo wa Trump kuanzisha vita dhidi ya Iran. Azimio hilo lilipitishwa kwa kura 55 za ndio huku wajumbe 45 wakilipinga.

4bv5b5623496721kkdd_800C450.jpeg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Natamani speaker wa bunge "NDUGAI" angekua na akili/uthubutu/nguvu/mtazamo/weredi hata nusu tu ya huyu "BI-DADA NANCY".

Nchi hii tungefika mbali sana, rais asingefanya mambo anavyotaka yeye na wala serikali isingefanya kazi kwa inavyojisikia.
 
Huyu mama ni pro Hillary Clinton - ni wale ambao hawa amini kwamba Trump alishibda kiti cha Urais ki halali - yeye na genge lake wanatafuta kila sababu za kujenga hoja zenye lengo la kumuondoa madarakani Trump hata kabla ya term yake kwisha, wako well organised kweli kweli.
 
Trump sio mjinga mpaka aanzishe Vita na Iran maana anajua madhara yake yatakuwa makubwa Sana.

Hilo azimio lilopitishwa ni njama ya Pelosi na genge lake kumhujumu Trump.
 
Huyu mama ni pro Hillary Clinton - ni wale ambao hawa amini kwamba Trump alishibda kiti cha Urais ki halali - yeye na genge lake wanatafuta kila sababu za kujenga hoja zenye lengo la kumuondoa madarakani Trump hata kabla ya term yake kwisha, wako well organised kweli kweli.
Kuanzisha vita bila sababu za msingi na jazba ni sawa?
 
On the contrary, kama Hillary Rodham Clinton angeshinda kiti cha Urais hivi sasa Dunia ingekuwa in mid WW3, alikuwa na hidden agenda ya kushambulia Urusi kwa kushtukiza tangu akiwa Waziri wa mambo ya nje wakati wa utawala wa Obama.

FYI, Dunia sasa hiko safer regardless ya Trump kuonekana ni mtu bellicose and war monger - deep down hayuko hivyo maneno mengi anayo yasema ni maigizo tu hana nia ya kuanzisha vita na Taifa lolote unlike Hillary and like mind.
 
Hidden Agenda Yakuishambulia URUSI ?!

Ulimaanisha RUSSIA Ipi kwanza MKUU ?!...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hidden Agenda Yakuishambulia URUSI ?!

Ulimaanisha RUSSIA Ipi kwanza MKUU ?!...

Sent using Jamii Forums mobile app

Mkuu sizungumzi vitu vyakubuni hapa, jaribu kutumia search engines mtandaoni kuhusu barua za siri ambazo Hillary Clinton alizisambaza kwenye Balozi za USA wakati akiwani Waziri wa mambo ya nje wa Taifa lake - barua zilikuwa na lengo la kuwatayarisha mabalozi wasije kushituka USA ikishambulia Urusi kwa kushtukiza - ukweli ndio huo, we unafikiri kwa nini kwenye kampein Clinton alikazania kuisingizia Urusi kwa mambo chungu mzima ambayo later yamekuja kuwa proven kwamba ni uongo na uzushi mtupu.

Kwa nini Trump alipo shinda kiti cha Urais Obama alitumia miezi michache ya mwisho wa utawala wake kutimua Wafanya kazi wa Balozi za Urusi huko Merikani wapatao 30 na family zao, kufunga Balozi ndogo za Warusi huko East na West Coast of USA - Obama na Clinton walitaka Trump apate wakati ngumu kuwa na maelewano mazuri na Serikali ya Putin baada ya kuona long term plan yao ya kushambulia Urusi kwa kushtukiza haitawezekana while Trump akiwa ofisini, narudia kusema mama huyo ni hatari sana kwa amani ya Dunia, anawatumikia owners wa Military Industrial Complex na Benki Kubwa nchini humo, hao ndio ufahidika sana kuuza silaha wakati wa vita.
 
On the contrary, kama Hillary Rodham Clinton angeshinda kiti cha Urais hivi sasa Dunia ingekuwa in mid WW3, alikuwa na hidden agenda ya kushambulia Urusi kwa kushtukiza tangu akiwa Waziri wa mambo ya nje wakati wa utawala wa Obama.

FYI, Dunia sasa hiko safer regardless ya Trump kuonekana ni mtu bellicose and war monger - deep down hayuko hivyo maneno mengi anayo yasema ni maigizo tu hana nia ya kuanzisha vita na Taifa lolote unlike Hillary and like mind.
Unazungumza kwa facts au hisia? Clinton siyo rais na maamuzi ya Trump ndiyo yanayoakisi msimamo wa Marekani. Mfano wa yaliyojiri karibuni dhidi ya Iran.Wenye "vision" wameona akiachwa bila kizuizi ataleta balaa.
 
Mkuu napingana na hio hidden agenda ambayo Walikua Nayo Kina Hillary
Mkuu sizungumzi vitu vyakubuni hapa, jaribu kutumia search engines mtandaoni kuhusu barua za siri ambazo Hillary Clinton alizisambaza kwenye Balozi za USA wakati akiwani Waziri wa mambo ya nje wa Taifa lake - barua zilikuwa na lengo la kuwatayarisha mabalozi wasije kushituka USA ikishambulia Urusi kwa kushtukiza - ukweli ndio huo, we unafikiri kwa nini kwenye kampein Clinton alikazania kuisingizia Urusi kwa mambo chungu mzima ambayo later yamekuja kuwa proven kwamba ni uongo na uzushi mtupu.

Kwa nini Trump alipo shinda kiti cha Urais Obama alitumia miezi michache ya mwisho wa utawala wake kutimua Wafanya kazi wa Balozi za Urusi huko Merikani wapatao 30 na family zao, kufunga Balozi ndogo za Warusi huko East na West Coast of USA - Obama na Clinton walitaka Trump apate wakati ngumu kuwa na maelewano mazuri na Serikali ya Putin baada ya kuona long term plan yao ya kushambulia Urusi kwa kushtukiza haitawezekana while Trump akiwa ofisini, narudia kusema mama huyo ni hatari sana kwa amani ya Dunia, anawatumikia owners wa Military Industrial Complex na Benki Kubwa nchini humo, hao ndio ufahidika sana kuuza silaha wakati wa vita.
Nikwamba Hilo Suala Hakuna Nakama Lilikuwamo Sio Ndani Ya Hii Miaka Na Hao Balozi Walokimbizwa RUSSIA Nakmbka Walikimbizwa Na Warusi Wenyewe Baada Ya Jambo Kama Hilo Kutokea Kwa Upande Wa US Dhidi Yawanadiplomasia Wa RUSSIA Waliopo DC

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom