Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 578
- 2,614
Unajua kuwa nanasi ndiyo tunda pekee duniani lenye vimeng’enya vya bromelain?
Huchukua zaidi ya asilimia 90 ya vimeng’enya vyote vinavyopatikana kwenye nanasi.
Vimeng’enya hivi vinavyotumika katika kuvunja protini mwili huwa na faida nyingi kwa afya. Baadhi ya faida hizo ni-
Chanzo: Afyainfo
Huchukua zaidi ya asilimia 90 ya vimeng’enya vyote vinavyopatikana kwenye nanasi.
Vimeng’enya hivi vinavyotumika katika kuvunja protini mwili huwa na faida nyingi kwa afya. Baadhi ya faida hizo ni-
- Husaidia kutibu changamoto za mfumo wa upumuaji kwa kupambana na maambukizi ya bakteria na virusi. Huondoa mafua.
- Husaidia kuondoa maumivu mwilini hasa yale yanayotokea kwenye maungio ya mifupa, kuvimba kwa tishu pamoja na baridi yabisi (Rheumatoid arthritis)
- Hupambana na aina mbalimbali za uvimbe joto (inflammation) mwilini.
- Huzuia kuongezeka kwa shinikizo kubwa la damu, kiharusi, shambulio la moyo pamoja na kuzuia kuganda kwa damu kwenye mishipa.
- Hutibu tatizo la pumu ya mfumo wa hewa.
- Hudhibiti ukuaji na usambaaji wa seli zinazosababisha saratani.
- Hupambana na aina mbaya za bakteria hasa wale wanaosababisha magonywa ya kinywa, uzazi na mfumo wa chakula.
- Hutibu vidonda vinavyosababishwa kuungua moto kwa kuondoa tishu mfu.
- Hutumiwa viwandani kwenye kuandaa nyama. Hulainisha nyama hizi ili zifae kwa matumizi ya kawaida ya binadamu.
Chanzo: Afyainfo