Sodoku
JF-Expert Member
- Feb 3, 2016
- 1,260
- 2,863
Nilimwambia jamaa yangu Mmoja Sophia Simba hawezi kwenda upinzani na kama akienda basi muda si mrefu angepata ugonjwa wa moyo na pengine kufariki. Kuhama CCM ni jambo gumu sana kuliko wengi wanavyodhani. Ni gumu sana kuliko kutoka kwenye ulokole kwenda kujiunga na harakati za shetani.
Ni wachache ambao wanajua nini wanafanya au wanataka wanaweza hama CCM. Ukihama CCM kama una biashara yako itakufa, kama una kampuni yako itakufa, kama ulikuwa umeajiriwa serikalini utapoteza kazi(uwezekano huo mkubwa upo) kwa ngazi aliyokuwa amefikia Sophia Simba asingeweza kuhama CCM nami simshauri.
Najua wapinzani wamekuwa wakichukua kila anayetoka au kufukuzwa ccm lakini katika hili kuna jambo la kujifunza.Kuna watu wa kutoka au kufukuzwa ccm waacheni. Hawana tija katika vyama vyenu. Hawa ni watu ambao kimwili wanakuwa upinzani ila kiroho wapo CCM. Maslahi waliyokuwa wanayapata ccm ni zaidi kiasi kwamba wanakuwa upinzani kwa ajili ya status tu lakini kimaslah ni ngumu sana. CCM kulikuwa na shughuli nyingi za kufanya vyeo ni vingi ambavyo vina maslah, kuna tender nyingi wanaweza pata. Kuna biashara nyingi sana wanaweza fanya wakiwa huko.
Na kwa wafanyabiashara ili wawe salama inabidi wawe ccm hii ni kauli ambayo imeshawah semwa mara kadha na viongozi wa juu wa CCM. hivyo hili si jambo dogo. Unapaswa kuwa msafi ili uweze kuhama CCM. Kama huna usafi hautadumu upinzani. Utakumbuka maziwa na asali uliyokuwa ukilamba miaka hiyo ccm utarudi tu siku moja. Na hapo utapata nafasi ya kuwatukana wapinzani ili ushangiliwe CCM.
Sophia Simba hana ujasili wa kuhama CCM msimlaumu. Sidhani kama anapenda afe maskini au aangushe kila alichosimamisha kupitia CCM?
Msidhani hajui anajua sana. Mwacheni aendelee kuwa mwana CCM moyoni hata kama wenyewe wamemkataa.