Namuonea sana Huruma Spika kwani Kijana Kipenzi anatumika Kummaliza ili Mama awe Spika 2020

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,568
108,910
Spika umechelewa sana Kuusoma huu Mchezo ambao ulipangwa na Kuratibiwa vizuri kabisa dhidi yako ili Uchafuke, watafutwe Watu Mitandaoni na Kwingineko Wakuchafue huku Kampeni za chini chini kwa hao unaowasimamia na kuwaongoza Bungeni zikiendelea ili huko pia Uchafuke na hatimaye sababu ipatikane na mwakani uonekane hufai kisha Mwanadada ambaye ndiyo Kipenzi kwa Kukikalia hicho Kiti chako awe hapo kisha Mipango mingine ya Kiukatili na Kukomoana iendelee.

Nakuonea mno Huruma Spika kwani pamoja na Ukongwe na Ujanja wako wote ulishindwa Kuushtukia huu Mchezo ambao tena ulianza Kusukwa dhidi yako muda mrefu huku huyo Mtu anayedhani ni Rafiki yako, anakupenda na kukubali ndiyo akiwa anakumaliza kama ambavyo imekuwa kawaida yake Kuwamaliza wengine hasa Kisiasa na Kimamlaka.

Kuna Kipindi huko nyuma nakumbuka Watu wenye nia njema tu nawe huku wengi Wao wakiwa wanatoka Upinzani walikuonya na hadi kukuambia kuwa endelea kuwa Neutral hapo Bungeni kwani Wewe unatumika tu pasipo Wewe kujua na kwamba ipo Siku Malengo ya hao wanaokutumia yakitimia basi utaundiwa Zengwe huku Kikundi cha Watu kutoka huko huko Upande wako uliko Kisiasa kikitumika katika Kukuangamiza Jambo ambalo sasa linaelekea Kutimia.

Ili mpango utimie akatafutwa Mtu ambaye hagusiki nchini na Kipenzi pia ili awe anakuchokoza na kukupandisha Jazba mara kwa mara ili uhamaki na utoke katika Reli kama Spika na uanze Majibizano nae kisha Hadhi yako ishuke na kwa hali iliyopo sasa ni kweli Hadhi yako imeshuka na inaendelea tu Kushuka.

Ni jana tu katika Muendelezo wa Mkakati wa Kukumaliza huyo Kijana amezua tena Jambo lingine la Kuihusisha Taasisi yako ya Bunge ambayo Wewe ndiye Kiongozi wake Mkuu kwamba imehusika na Ulaji wa Kifisadi wa Hela za Michango kwa Timu ya Taifa Stars huko Misri huku lengo Kuu la huyo Kijana likiwa ni lile lile tu la Kukumaliza na Kukuchafua huku aliyemtuma akiwa amepumzika zake tu Kwao Jirani za Ziwa lenye Jina la Malkia wa Uingereza.

Pole sana Spika ila nadhani sasa ile Laana ya Mbunge Mgonjwa inaanza Kukutafuna na bado hujachelewa kwenda Kumuomba Radhi. Wewe ulidhani kwa Uonevu wako dhidi yake hadi Kumkomoa utakuwa ndiyo unapendwa na aliyepumzika sasa Ziwani na leo anampokea Mla Mirungi kutoka hapo Jirani kumbe ulikuwa unatumika tu kwa Maslahi yake / yao na sasa wameshaona umekuwa Tambala la Dekio ( huna thamani tena Kwao ) wameamua Kukuundia Zengwe ili Uchafuke sana na uonekane hufai kwa lolote wala chochote kile.

Ushauri wangu tu Kwako najua kuwa tayari huyo Kipenzi ameshakuharibia hasa katika hili Suala zima la Taifa Stars na Pesa ya Michango iliyopotea Kifisadi huku Taasisi yako ya Bunge pamoja na Wabunge wako wakihushwa na Ulaji huo na Wewe sasa ili umkomoe na uweze Kummaliza vyema huyo Kipenzi ( japo najua umeshachelewa ) na Wewe ibua Ufisadi wake wa Pesa za Michango kama Tsh Milioni 500 ambazo zilichangwa mbele ya Mama Ushungi Daima kwa Timu ambapo kuna taarifa kwamba zilizowafikia Wachezaji ni kama tu Tsh Milioni 200 na zingine huyo Kipenzi na Wapambe wake wamekula na ili Kuwazuga Wachezaji alipokuwa nao huko Misri akajifanya kuwafanyia Shopping za hapa na pale na Kuonekana kweli ana Uchungu nao wakati Kiuhalisia kumbe amewapiga ( amewaibia ) sana tu.

Spika wangu sijui utakuwa Mgeni wa nani tena.
 
Wakimaliza kututeka wataanza kutekana wao kwa wao na kutafunana

Mi enzi hizo nipo mbinguni nawasubiria pale mlangoni kuwa direct mlango wa kwenda kule kwa baba yao shetan !

Ntakua nacheka kinoma , kama huyo ndugai ntamwambia bwana malaika gabriel aniachien yaani ni mwendo wa kichura chura mpaka motoni !

Ntakachomfanya bashite , i reserve my comment

Hahaha !
 
Wakimaliza kututeka wataanza kutekana wao kwa wao na kutafunana

Mi enzi hizo nipo mbinguni nawasubiria pale mlangoni kuwa direct mlango wa kwenda kule kwa baba yao shetan !

Ntakua nacheka kinoma

Hahaha !
Nami ntakua mitaa hyo hyo nagongea msuba huku nikiwacheka kwa dharau maana tuliwaambia wakikosa nyama wataanza kulana wenyewe kwa wenyewe
 
Mbunge Mjeruhiwa ana Laana Kali na mbaya sana ambayo sasa ndiyo inamtafuna vizuri mno Spika.
Walichomfanya lissu kiliniumiza

Ila Katika maisha yetu, kama ilivyo kwenye nguo, upo ule uzi unaojitokeza na kukera ambao ukikosea kuufumua au kuuvuta nguo nzima huraruka, au sweta zima hufumuka na kugeuka uzi. Somo hapa ni kuwa hasira na nguvu hazitatui kila tatizo".
 
Spika Ndugai siyo maji baridi,ni ngangali kweli kweli.
Jaribu kumzunguka muone kipigo kitakatifu.
 
Back
Top Bottom