yaani dunia ya leo zawadi kanga nimemwambie amrudishie na ampige kibuti
natalia mpenzi,
naomba nikusaidie uelewa kidogo kuhusu
maana ya zawadi na hasa katika mahusiano ya mapenzi.
zawadi ni jinsi au njia ya kuonyesha kuguswa na thamani ya umpendaye na kumpatia kitu ambacho unaamini katika matumizi yake ataendelea kukukumbuka na kulienzi penzi/pendo lako la thamani kwake... Zawadi ya aina yoyote na thamani yoyote hutosha kufikisha ujumbe huo mzito kwa mwenza aliyepewa zawadi hiyo.
Zawadi nzuri katika mapenzi ni zile zinazogusa maisha ya mwenza wako ikiwezekana kila siku ili azidi kukuweka moyoni mwake na kulithamin penzi la aliyempatia zawadi hiyo.
Zipo pia zawadi ndogondogo zinazoweza kumgusa muhusika kwa muda mfupi tu..say tunda kama apple, ice cream, chocolate dinner ya pamoja etc.
Zipo zawadi ndogo pia ila zaweza kumgusa muhusika kwa muda mrefu. Eg. Taulo la kuogea, khanga, kitenge, chupi, miwani, perfumes, mswaki, simu za mkononi, viatu, handkerchief, pen, make-up set na nyinginezo chungu nzima.
Zawadi huwa na thamani pia ikilinganishwa na umbali au hata juhudi zilizotumika kuipata zawadi hiyo..say umerudi toka safari nchini congo ukaleta kitenge, umefanya kazi kwa muda mrefu na kurudi na zawadi kwa pesa uliyoitumia kununulia zawadi imetokana na extra efforts.
Zawadi za vitu kama pesa hata iwe ni mamilioni ya pesa huwa vinasahaulika kwa haraka sana kwa muhusika kwa vile hujikuta akitumia kwa matumizi anayoona yeye ni ya kawaida ikilinganishwa na kitu kidogo alicholetewa na mpenziwe.
Natumai nimekusaidia katika somo hili dogo...
naomba pia usijaribu kuuvunja uhusiano wa cousin wako.