Namuona Kikwete Ndani ya Magufuli

Namuona Kikwete Ndani ya Magufuli

Yani kila kitu hadi wabebwe waandishi wa habari.
Duh, sasa hapa naona mnazidi kumponda 'mwokozi' wetu a.k.a chaguo la Mungu. Ina maana unataka kusema kwamba akiona waandishi hawapo ndipo anapiga simu mwenyewe pawa brekifasti!?
 
Kwani Kikwete si kaanza kuchukiwa na wachache pale 'urafiki wa kutokutana barabarani' ulivoyeyuka tu! Bado anapendwa sana tu na Watanzania!
mkuu hawa nyumbu hawawezi kukuelewa. hawajiulizi tu hata alipokuwa anaaga pale uwanja wa Taifa watu walizizima kwa furaha na huzuni kumuaga huyo jamaa. yeye anafikiri wakiandika humu mitandaoni na kile kigazeti cha jamhuri ndo ishara kuwa Kikwete anachukiwa na watanzania. aibu yao.
 
Nafikiri ndio huko Mombasa mnapodanganyana
 
Huu utamaduni hata Mwinyi ulimkumba
aliitwa 'mzee Ruksa' kama kumtukana....
Mkapa alipoingia aliagiza picha Mwinyi iondolewe haraka hata Picha yake haijawa tayari..
na yeye Kikwete alivyoingia akashangaa anaandamwa..
Magufuli asipoangalia atakuja kuandamwa asiamini
Watu wana matarajio ila yanayeyukaga. Uzuri watz watulivu kama kobe!!ukimgusa anarudisha kichwa ndani ya jumba. Hili linatumika vibaya.wanajua vichwa vitarudi ndani kama kobe! Bado ni mapema sijajua tuko sahihi au la...ila kama safari hii haitakuwa nzuri. Kobe atauma.
 
PIGA picha. Vuta hisia na kumbukumbu. Unakumbuka nini katika wakati kama huu, miaka 10 iliyopita? Mimi nakumbuka machache, yaliyotangulia na yaliyofuata baadaye.

Miaka 10 baada ya kuahidiwa “maisha bora kwa kila Mtanzania” yakashindikana, sasa watu wanazungumzia “Tanzania Mpya” ya Magufuli

Yupo wapi Kikwete “rafiki wa vyombo vya habari” aliyehitimisha miaka 10 ya utawala wake bila kuruhusu zitungwe sheria za kulinda taaluma ya habari, waandishi, wamiliki wa vyombo vya habari na watoa habari?

Rais Kikwete huyu tunayemzomea leo, tulimharibu wenyewe. Na sasa tunamzomea wenyewe. Ni malipo ya “urafiki wa mashaka.”

Rais Magufuli wa leo hatofautiani na Rais Kikwete wa Machi 2006. Wote wanajua jinsi ya kucheza na hisia za wananchi.

Kikwete tuliyemlea, aliyelewa sifa zetu, akafanya atakavyo, ameacha shida zinasotesa wananchi. Wanasema amewaachia shida. Wanalia. Rais Magufuli anatumbua majipu yake, yeye “anatumbua raha” alizojiandalia kwa miaka 10 mfululizo.

Na wakati wananchi wanashangilia utumbuaji wa majipu unaofanywa na rais, hawana muda wa kutafakari, ni akina nani wanateuliwa kuziba nafasi

Rais Magufuli si “rafiki wa vyombo vya habari” lakini ana uhusiano mzuri na baadhi yetu, na ameanza kujifunza jinsi ya kuishi na vyombo vya habari na waandishi ili wasimtumbue jipu.

Na kwa wengine, Rais Magufuli hachekicheki kama Kikwete. Anafura. Anachukia. Anaamuru.

Hakika, hii siyo Tanzania tunayotaka kujenga. Nchi ya waoga. Nchi ya wanafiki. Nchi ya kujipendekeza. Nchi ya kukubali bila kuhoji. Nchi itakayoangamia kwa ukimya wetu.
@Mwahabari: nikupe pongezi kwa kutoa changamoto kwa wana JF kwa hoja zako nzito lakini tatanishi.

Nzito kwa msingi kwamba unataka wanajamvi tumtathmini Magufuli uwezo wake katika muda mfupi kwa kumlinganisha na aliyemtangulia.

Hoja tatanishi kwa msingi kwamba unazungumzia watu na matukio na siyo masuala yanayochangia uchumi wa nchi hii usikue pamoja na utajiri asilia uliopo. Hapa nina maana ya sera na mikakati iliyopo ya maendeleo.

Pamoja na pongezi na hoja pingamizi zangu zifuatazo, umeibua mjadala mwafaka. Je,

1) Tujadili viongozi kwa matendo yao kama ulivyofanya (rejea baadhi ya nukuu za mada yako)!

2) Tujadili uongozi wa nchi hii tangu kupata uhuru kwa sera na mikakati ya watawala (hukuligusia)!!

3) Tujadili kudumaa kwa maendeleo ya nchi tajiri kwa sababu ya wananchi waoga (hoja yako)!!!

Tufanyeje kuondokana na hali uliyoielezea kwenye mada yako (angalizo ya nukuu)?

Kwa mtazamo wangu tunakosa uongozi bora (tujadili tafsiri ya 'uongozi bora' kwa kurejea viongozi waliopita wamefanya nini kwa Taifa hili) ili dhana ya Baba wa Taifa kuhusu maendeleo iwe na nafasi katika kujipanga kufikia kwenye nchi ya asali: watu, ardhi, siasa safi ba uongozi bora.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
 
Ungenisoma vizuri ungenielewa
 
PIGA picha. Vuta hisia na kumbukumbu. Unakumbuka nini katika wakati kama huu, miaka 10 iliyopita? Mimi nakumbuka machache, yaliyotangulia na yaliyofuata baadaye. Nyakati zinashindana na kupingana; lakini zinafanana, anaandika Ansbert Ngurumo.

Nakumbuka nyakati za kushangilia “ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya.” Ni shangilio la kaulimbiu. Naoanisha hilo na hili la sasa: “Hapa Kazi Tu!”

Nakumbuka enzi za Rais Jakaya Kikwete kuitwa “chaguo la Mungu?” Wengine walimwita “Tumaini lililorejea.” Wapo waliomuita, “Mkombozi mpya wa Tanzania.”

Wakati wakimwita Kikwete mkombozi, mtangulizi wake, Rais Benjamin Mkapa, alipewa majina yote mabaya. Mbabe. Katili. Mwizi. Aliambiwa ameharibu nchi. Hakuwa mtu wa watu.

Naona kama tumerudi nyuma miaka 10. Chaguo la Mungu sasa linapewa sifa za kijambazi, na huyu mpya, John Magufuli anaitwa “mpenzi wa Mungu.”

Kikwete aliyeshangiliwa na kusifiwa, sasa anazomewa na watu wale wale waliomsifu na kumtukuza. Wapo wanaodiriki kusema amekuwa mbaya kuliko Mkapa.

Miaka 10 baada ya kuahidiwa “maisha bora kwa kila Mtanzania” yakashindikana, sasa watu wanazungumzia “Tanzania Mpya” ya Rais Magufuli.

“Tanzania yenye neema inawezekana” ya Kikwete imetoweka ghafla. Hatujiulizi wanakotoa kaulimbiu tamu zinazoteka wananchi kwa muda, halafu zikawatesa baadaye.

Watu wale wale, mambo yale yale. Hatujifunzi. Hatukui. Hatuendelei kwa sababu hatutumii fikra bali hisia. Ndiyo maana tunadanganywa kirahisi.

Namkumbuka, Gado, mchora katuni mmoja katika magazeti ya Nation, Kenya. Alichora waandishi wa Tanzania wakiwa wanalamba viatu vya Rais Kikwete.

Tafsiri yake ilikuwa pana. Ilikera watawala na waandishi. Lakini ujumbe ulikuwa umefika, kwamba vyombo vyetu vya habari, badala ya kumhoji rais, vilimtukuza.

Leo tukitazama nyuma, tunajivuna kwa kazi tuliyofanya kumdekeza na kumfikisha Kikwete hapo alipo leo?

Yupo wapi Kikwete “rafiki wa vyombo vya habari” aliyehitimisha miaka 10 ya utawala wake bila kuruhusu zitungwe sheria za kulinda taaluma ya habari, waandishi, wamiliki wa vyombo vya habari na watoa habari?

Kwa sababu ya “urafiki huo” wakosoaji kadhaa wa serikali – waandishi na wanaharakati wengine, waliumizwa, waliteswa, na wengine waliuawa. Tuligawanyika ilipofika zamu yetu kujadili mateso na dhuluma hizi. Tulilewa madaraka yasiyo yetu.

Hayo ndiyo malipo ya mapokezi ya shangwe tuliyompa. Miaka mitano ya kwanza ya “ari mpya, nguvu mpya na kazi mpya” ilizaa miaka mitano mingine ya “ari zaidi, nguvu zaidi, na kasi zaidi.” Tuliona lakini hatukutafakari. Hatukushtuka!

Rais Kikwete huyu tunayemzomea leo, tulimharibu wenyewe. Na sasa tunamzomea wenyewe. Ni malipo ya “urafiki wa mashaka.”

Alipoanza ziara za kushtukiza katika ofisi na idara za serikali, tuliona ni mapinduzi makubwa sana. Alipopeleka wateule wake katika semina elekezi, halafu akawahutubia mwanzo hadi mwisho, tulisifu ubunifu mpya wa utendaji.

Hatukuhoji Kikwete amepata wapi maarifa ya ghafla anayojaribu kupandikiza kwa wasaidizi wake. Hatukuhoji alipata wapi uadilifu wa ghafla uliotufanya tumuone tofauti na mfumo wake.

Tulidanganywa na tabasamu lake. Tulimezwa na nguvu yake ya kuteka na kutumia vyombo vya habari kuimba sifa zake.

Hata vichwa vya habari vilibadilika. “Kikwete, we acha tu! Haijawahi kutokea.” Tulivyo wasahaulifu, Rais Magufuli naye alipoanza ziara za kushtukiza, tukarejea kule kule.

Rais Magufuli alipofuta semina elekezi, tukamuona shujaa, wakati sisi ndio tulishangilia semina hizo zilipoasisiwa na Kikwete miaka 10 iliyopita.

Kama vile Rais Kikwete alivyojaribu kujijenga kwa kumbomoa Mkapa, huyu naye anajijenga kwa kumbomoa Kikwete.

Ndiyo “majipu” haya yanayotumbuliwa. Ni “majipu” ya Kikwete. Ni “majipu” tuliyosababisha wenyewe kwa kushangilia matendo, kauli na vituko vya Kikwete.

Ni “majipu” ya makofi na vifijo vyetu. “Majipu” haya yanayotumbulia ni salamu kutoka juu. Ni dhihaka isiyo kifani kwamba chaguo la Mungu linatumbuliwa majipu!

Tunaponzwa na ukasuku wa “kuimbaimba” kaulimbiu za watawala.

Rais Magufuli wa leo hatofautiani na Rais Kikwete wa Machi 2006. Wote wanajua jinsi ya kucheza na hisia za wananchi.

Huyu anazungumza lugha ya wananchi waliokata tamaa. Anatoa matumaini mapya kwa wananchi maskini wanaokerwa na utajiri wa wengine, na walioaminishwa kwamba utajiri huo, kama usingekuwa mikononi mwa hao wachache, ungekuwa kwa maskini hao.

Wananchi wanashangilia jinsi anavyotumbua majipu kwa sababu aliyetanguliwa aliyalea. Lakini naye anasahau kwamba anajenga msingi wa yeye kutumbuliwa baadaye.

Kikwete tuliyemlea, aliyelewa sifa zetu, akafanya atakavyo, ameacha shida zinasotesa wananchi. Wanasema amewaachia shida. Wanalia. Rais Magufuli anatumbua majipu yake, yeye “anatumbua raha” alizojiandalia kwa miaka 10 mfululizo.

Na wakati wananchi wanashangilia utumbuaji wa majipu unaofanywa na rais, hawana muda wa kutafakari, ni akina nani wanateuliwa kuziba nafasi za wanaotumbuliwa.

Je, tunawajua na kuwaamini wanaoingizwa kuzina nafasi za waliotumbuliwa majipu? Mbona wengi wao ni watu waliokuwa karibu sana na Magufuli huko alikotoka? Mbona na huko kuna majipu mengi waliyosababisha kabla ya kuondolewa?

Yawezekana utumbuaji huu wa majipu ni fursa ya Magufuli kuchomoa watu wa Rais Kikwete na kuchomeka watu wake kwenye serikali?

Rais Magufuli si “rafiki wa vyombo vya habari” lakini ana uhusiano mzuri na baadhi yetu, na ameanza kujifunza jinsi ya kuishi na vyombo vya habari na waandishi ili wasimtumbue jipu.

Anajaribu kujenga kundi la watetezi wake. Ameshapata genge la washangiliaji. Anajaribu kugawa makundi ya wakosoaji. Nia yake ni moja. Aachwe apumue. Afanye atakalo. Tutajadiliana baada ya miaka mitano.

Na kwa wengine, Rais Magufuli hachekicheki kama Kikwete. Anafura. Anachukia. Anaamuru.

Mtu mmoja amesema, “kama mliumizwa na rais anayetabasamu, kwa huyu mtauawa wengi. Punguzeni makali. Huyu ni mkali.”

Sikiliza kauli na ahadi zake mbele ya majaji na mahakimu. Rejea hotuba yake bungeni kuhusu mustakabali wa katiba mpya. Jikumbushe hotuba yake ya Singida kuhusu vyama vya siasa.

Hakika, hii siyo Tanzania tunayotaka kujenga. Nchi ya waoga. Nchi ya wanafiki. Nchi ya kujipendekeza. Nchi ya kukubali bila kuhoji. Nchi itakayoangamia kwa ukimya wetu.

Naweza nikasema sijakutana na andiko lenye mashiko na lililoandikwa kwa utaalamu mkubwa kama hili tangu mwaka huu uanze! hizi ndizo akili kubwa tunazozitaka! kama ilivyo ada mazombi ya kukosoa andiko kama hili huwa hayakosekani na yashavamia kote!

Naanza kuamini kuwa kula vizuri na kulala vizuri kunamfanya mtu awe smart hata anapotoa au kupinga hoja! mizombi inayopinga huu uzi kula vizuri ni shida, kulala vizuri ni shida, yaani ni stress kibaao! na sio kosa lao ni CCM imewafikisha hapa! kama mnabisha hebu ikaneni CCM muone kama akili zenu hazitakuwa bright kama za mwandishi.
 
mwanzo wakati nakutana na huu uzi nikaona kama vile ni mreeeefu, nkakata tamaa, sikusoma hata sentensi moja, nikascroll chini, nikasema hapana hebu nisome, nilipoanza kuusoma sikutamani uishe!

ila kiukweli watanzania walio wengi wameendelea kuwa wajinga, sijui watapona lini

EE MWENYEZI MUNGU TUHURUMIE SISI WATANZANIA
 
Ngurumo yuko sawa, nakumbuka kipindi cha kwanza cha JK, BWM alikuwa mafichoni, hakudiriki kujitokeza kwenye hadhara kuhofia kuzomewa!. Leo yale yale taliyomkuta BWM yanamkuta JK.
Watanzania wana mzuka wa serikali mpya, Mzuka ukishaisha, watagundua kuwa bei ya unga, mchele, mafuta iko palepale hapo ndipo Honeymoon kwa utawala mpya itakapokwisha.
Thamani ya shilingi Kwa dola bado inazidi kushuka , wananchi wa kipato cha chini wanataabika sana mzunguko wa pesa upo vibaya sana hakuna unafuu wowote.
 
mwanzo wakati nakutana na huu uzi nikaona kama vile ni mreeeefu, nkakata tamaa, sikusoma hata sentensi moja, nikascroll chini, nikasema hapana hebu nisome, nilipoanza kuusoma sikutamani uishe!

ila kiukweli watanzania walio wengi wameendelea kuwa wajinga, sijui watapona lini

EE MWENYEZI MUNGU TUHURUMIE SISI WATANZANIA
hakuna unafuu wowote bali wajanja wachache wamejinufaisha kupitia Majipu , Yaani wenye dhamana wanawafuatilia watu wa TRA wenye Utajiri mkubwa Kama wa Gasper Mhina kisha wanapewa Rushwa wanatulia huku wajanja wakiweka nyumba na mali zao Kwa majina ya Ndugu na marafiki . Magufuli anajituma kutumbua Majipu huku anaowataja wao wamejichumia Rishwa Kwa mgongo wake.
 
PIGA picha. Vuta hisia na kumbukumbu. Unakumbuka nini katika wakati kama huu, miaka 10 iliyopita? Mimi nakumbuka machache, yaliyotangulia na yaliyofuata baadaye. Nyakati zinashindana na kupingana; lakini zinafanana, anaandika Ansbert Ngurumo.

Nakumbuka nyakati za kushangilia “ari mpya, nguvu mpya, kasi mpya.” Ni shangilio la kaulimbiu. Naoanisha hilo na hili la sasa: “Hapa Kazi Tu!”

Nakumbuka enzi za Rais Jakaya Kikwete kuitwa “chaguo la Mungu?” Wengine walimwita “Tumaini lililorejea.” Wapo waliomuita, “Mkombozi mpya wa Tanzania.”

Wakati wakimwita Kikwete mkombozi, mtangulizi wake, Rais Benjamin Mkapa, alipewa majina yote mabaya. Mbabe. Katili. Mwizi. Aliambiwa ameharibu nchi. Hakuwa mtu wa watu.

Naona kama tumerudi nyuma miaka 10. Chaguo la Mungu sasa linapewa sifa za kijambazi, na huyu mpya, John Magufuli anaitwa “mpenzi wa Mungu.”

Kikwete aliyeshangiliwa na kusifiwa, sasa anazomewa na watu wale wale waliomsifu na kumtukuza. Wapo wanaodiriki kusema amekuwa mbaya kuliko Mkapa.

Miaka 10 baada ya kuahidiwa “maisha bora kwa kila Mtanzania” yakashindikana, sasa watu wanazungumzia “Tanzania Mpya” ya Rais Magufuli.

“Tanzania yenye neema inawezekana” ya Kikwete imetoweka ghafla. Hatujiulizi wanakotoa kaulimbiu tamu zinazoteka wananchi kwa muda, halafu zikawatesa baadaye.

Watu wale wale, mambo yale yale. Hatujifunzi. Hatukui. Hatuendelei kwa sababu hatutumii fikra bali hisia. Ndiyo maana tunadanganywa kirahisi.

Namkumbuka, Gado, mchora katuni mmoja katika magazeti ya Nation, Kenya. Alichora waandishi wa Tanzania wakiwa wanalamba viatu vya Rais Kikwete.

Tafsiri yake ilikuwa pana. Ilikera watawala na waandishi. Lakini ujumbe ulikuwa umefika, kwamba vyombo vyetu vya habari, badala ya kumhoji rais, vilimtukuza.

Leo tukitazama nyuma, tunajivuna kwa kazi tuliyofanya kumdekeza na kumfikisha Kikwete hapo alipo leo?

Yupo wapi Kikwete “rafiki wa vyombo vya habari” aliyehitimisha miaka 10 ya utawala wake bila kuruhusu zitungwe sheria za kulinda taaluma ya habari, waandishi, wamiliki wa vyombo vya habari na watoa habari?

Kwa sababu ya “urafiki huo” wakosoaji kadhaa wa serikali – waandishi na wanaharakati wengine, waliumizwa, waliteswa, na wengine waliuawa. Tuligawanyika ilipofika zamu yetu kujadili mateso na dhuluma hizi. Tulilewa madaraka yasiyo yetu.

Hayo ndiyo malipo ya mapokezi ya shangwe tuliyompa. Miaka mitano ya kwanza ya “ari mpya, nguvu mpya na kazi mpya” ilizaa miaka mitano mingine ya “ari zaidi, nguvu zaidi, na kasi zaidi.” Tuliona lakini hatukutafakari. Hatukushtuka!

Rais Kikwete huyu tunayemzomea leo, tulimharibu wenyewe. Na sasa tunamzomea wenyewe. Ni malipo ya “urafiki wa mashaka.”

Alipoanza ziara za kushtukiza katika ofisi na idara za serikali, tuliona ni mapinduzi makubwa sana. Alipopeleka wateule wake katika semina elekezi, halafu akawahutubia mwanzo hadi mwisho, tulisifu ubunifu mpya wa utendaji.

Hatukuhoji Kikwete amepata wapi maarifa ya ghafla anayojaribu kupandikiza kwa wasaidizi wake. Hatukuhoji alipata wapi uadilifu wa ghafla uliotufanya tumuone tofauti na mfumo wake.

Tulidanganywa na tabasamu lake. Tulimezwa na nguvu yake ya kuteka na kutumia vyombo vya habari kuimba sifa zake.

Hata vichwa vya habari vilibadilika. “Kikwete, we acha tu! Haijawahi kutokea.” Tulivyo wasahaulifu, Rais Magufuli naye alipoanza ziara za kushtukiza, tukarejea kule kule.

Rais Magufuli alipofuta semina elekezi, tukamuona shujaa, wakati sisi ndio tulishangilia semina hizo zilipoasisiwa na Kikwete miaka 10 iliyopita.

Kama vile Rais Kikwete alivyojaribu kujijenga kwa kumbomoa Mkapa, huyu naye anajijenga kwa kumbomoa Kikwete.

Ndiyo “majipu” haya yanayotumbuliwa. Ni “majipu” ya Kikwete. Ni “majipu” tuliyosababisha wenyewe kwa kushangilia matendo, kauli na vituko vya Kikwete.

Ni “majipu” ya makofi na vifijo vyetu. “Majipu” haya yanayotumbulia ni salamu kutoka juu. Ni dhihaka isiyo kifani kwamba chaguo la Mungu linatumbuliwa majipu!

Tunaponzwa na ukasuku wa “kuimbaimba” kaulimbiu za watawala.

Rais Magufuli wa leo hatofautiani na Rais Kikwete wa Machi 2006. Wote wanajua jinsi ya kucheza na hisia za wananchi.

Huyu anazungumza lugha ya wananchi waliokata tamaa. Anatoa matumaini mapya kwa wananchi maskini wanaokerwa na utajiri wa wengine, na walioaminishwa kwamba utajiri huo, kama usingekuwa mikononi mwa hao wachache, ungekuwa kwa maskini hao.

Wananchi wanashangilia jinsi anavyotumbua majipu kwa sababu aliyetanguliwa aliyalea. Lakini naye anasahau kwamba anajenga msingi wa yeye kutumbuliwa baadaye.

Kikwete tuliyemlea, aliyelewa sifa zetu, akafanya atakavyo, ameacha shida zinasotesa wananchi. Wanasema amewaachia shida. Wanalia. Rais Magufuli anatumbua majipu yake, yeye “anatumbua raha” alizojiandalia kwa miaka 10 mfululizo.

Na wakati wananchi wanashangilia utumbuaji wa majipu unaofanywa na rais, hawana muda wa kutafakari, ni akina nani wanateuliwa kuziba nafasi za wanaotumbuliwa.

Je, tunawajua na kuwaamini wanaoingizwa kuzina nafasi za waliotumbuliwa majipu? Mbona wengi wao ni watu waliokuwa karibu sana na Magufuli huko alikotoka? Mbona na huko kuna majipu mengi waliyosababisha kabla ya kuondolewa?

Yawezekana utumbuaji huu wa majipu ni fursa ya Magufuli kuchomoa watu wa Rais Kikwete na kuchomeka watu wake kwenye serikali?

Rais Magufuli si “rafiki wa vyombo vya habari” lakini ana uhusiano mzuri na baadhi yetu, na ameanza kujifunza jinsi ya kuishi na vyombo vya habari na waandishi ili wasimtumbue jipu.

Anajaribu kujenga kundi la watetezi wake. Ameshapata genge la washangiliaji. Anajaribu kugawa makundi ya wakosoaji. Nia yake ni moja. Aachwe apumue. Afanye atakalo. Tutajadiliana baada ya miaka mitano.

Na kwa wengine, Rais Magufuli hachekicheki kama Kikwete. Anafura. Anachukia. Anaamuru.

Mtu mmoja amesema, “kama mliumizwa na rais anayetabasamu, kwa huyu mtauawa wengi. Punguzeni makali. Huyu ni mkali.”

Sikiliza kauli na ahadi zake mbele ya majaji na mahakimu. Rejea hotuba yake bungeni kuhusu mustakabali wa katiba mpya. Jikumbushe hotuba yake ya Singida kuhusu vyama vya siasa.

Hakika, hii siyo Tanzania tunayotaka kujenga. Nchi ya waoga. Nchi ya wanafiki. Nchi ya kujipendekeza. Nchi ya kukubali bila kuhoji. Nchi itakayoangamia kwa ukimya wetu.
Kuna afisa wa TRA Temeke anaitwa Gasper Mhina huyo ni Tajiri kuliko Masamaki , ana majumba kibao Tanga kwao, Arusha , Dodoma na Dsm ambapo nyumba nyingi zipo Kwa majina ya Ndugu zake . Magufuli kamshindwa aliwatuma vyombo vyake vyote wamedunda, wengine Sasa wamekuwa watumwa wake wanampatia Taarifa zote na kumfundisha jinsi ya kuficha Mali na kukesha Kwa Sangoma aliopewa na January Makamba baada ya kufadhili ccm Uchaguzi uliopita na Uchaguzi wa Zanzibar , Tambua kuwa Majipu mengine yanalelewa na kulindwa huku vijipu vidogo vikiandamwa.
 
Back
Top Bottom