Namtafuta wangu wa maisha

Adam4eva

Member
Feb 14, 2017
7
2
Salaam, wana JF

Kwa mara nyingine tena naleta mbele yenu maombi yangu nikiwa naamini kwa moyo wangu wote kuwa lipo jibu miongoni mwenu. Haja ya moyo wangu ni kumpata binti au mwanamke ambaye analandana nami ili tuweze kufunga ndoa na kuishi pamoja. Wasifu wangu kwa ufupi ni kama ifuatavyo:-

· Miaka 43
· Elimu ya chuo kikuu
· Nimeajiriwa
· Mkristo niliyeokoka
· Nina watoto 3 ambao nataka niendelee kuishi nao katika ndoa yangu mpya
· Mimi ni mweusi, umbo la kati (si mnene, si mwemba)
· Raia wa Tanzania

Natafuta binti / mwanamke ambaye hakosi sifa zifuatazo:-

· Mkristo aliyeokoka au ambaye yuko tayari kuokoka
· Awe tayari kuwalea watoto nilionao tayari bila ubaguzi wa aina yoyote ile

Sifa zingine za ziada (lakini si za lazima) ni pamoja na hizi zifuatazo:-

· Awe ameajiriwa au kama sivyo awe mjasiriamali anayeipenda kazi yake
· Awe na miaka 22 – 29.
· Elimu ya kidato cha nne na kuendelea.
· Awe mweupe au maji ya kunde

Siyo rahisi kuwa na sifa zote. Cha muhimu ni kuwa, aliye na nia ya dhati anitumie private message (PM).
 
Mungu akujaalie upate mke atakaekua kivuli wakati wa jua, na mwamvuli wakati wa mvua
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom