Namtafuta 'Mbunge' Muslim Hassanal | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namtafuta 'Mbunge' Muslim Hassanal

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Asha Abdala, Dec 3, 2009.

 1. A

  Asha Abdala JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 21, 2007
  Messages: 1,134
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Baada ya Kafulila kuondoka chamani kwenda kwenye NCCR Mageuzi ambayo Mbunge wa Kigoma Kaskazini na Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe aliwahi kukitaja humu kwamba kilipewa fedha za EPA kuhujumu majimbo ambayo CHADEMA ilikuwa na nguvu mwaka 2005, nimejikuta nakumbukia uchaguzi wa mwaka 2005.

  Nakumbuka mwaka huo palikuwa na mgombea mdogo kuliko wote alitoka mara moja tu katika gazeti moja la kila wiki, na baada ya uchaguzi sijamsikia tena mara kwa mara. Huyu kijana picha yake niliyoiona gazetini ilikuwa handsome sana, natamani nimuone uso kwa uso!.

  Hivi karibuni nilisoma akitajwa kwenye gazeti la Hoja takribani mwezi mmoja kabla ya Kafulila kutimka mwenywe CHADEMA. Gazeti hilo lilimnukuu Kafulila akisema kwamba kuna makundi ndani ya CHADEMA ambayo yamesababisha chama kugawanyika hata kwenye kuteua wagombea. Habari hiyo ilimnukuu Kafulila akisema kwamba hali hiyo imedhihirika katika jimbo la Kigoma Kusini. Alisema kwamba kuna Kambi ya Zitto, ambayo inamtaka yeye awe mgombea, kambi ambayo ni ya vijana wengi nchi nzima na inawakilisha kundi la watanzania wa kawaida.

  Kafulila alinukuliwa akisema kwamba kundi la pili ni kambi ya Mbowe na Dr Slaa ambayo ni ya wazee na matajiri ambayo ina mtaka mjumbe wa bodi ya wadhamini wa chama hicho kijana Muslim Hassanal ndio awe mbunge wa jimbo hilo.

  Kafulila aliendelea kusema kundi hilo, ndio limemfadhili Muslim kwenda Kigoma kutimiza moja ya ahadi zake za mwaka 2005 aliyoitoa kwamba atahakikisha kila zahanati inapata magodoro, achaguliwe au asichaguliwe. Inadaiwa kwamba Muslim ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara vijana alitoa ahadi katika sekta mbalimbali ambazo zote alisema hata akishindwa ubunge angezitimiza kabla ya uchaguzi ujao.

  Madai hayo yalijitokeza kabla ya uchaguzi wa serikali za mitaa, na Kafulila akadai pia kuwa Muslim anafanya hivyo ili CHADEMA ikishinda Vijiji vya Kigoma Kusini ionekane yeye ndio amechangia.

  Nisaidieni jamani, namtafuta "Mbunge" Muslim Hassanal. Nimejaribu ku-google search habari pekee ambayo naona imemtaja ni http://www.habaritanzania.com/new/articles/3113/1/-Mawaziri-wa-Mkapa-wapeta-majimboni

  Niliposoma habari hii nikakumbuka jina la Kiffu aliyekuwa NCCR Mageuzi ambaye chama kule kilikuwa ni yeye na yeye ndio chama, matokeo yake uamuzi wake wa kuhama kwenda CCM mara baada ya uchaguzi ukakigawa chama hicho vipande vitatu. Kipande kimoja akaenda nacho CCM, kipande kingine kikaenda CHADEMA, kipande kimoja kilibaki NCCR; ndio hiki alichonacho Kafulila hivi sasa.

  Matokeo yake ni NCCR ambayo ilipata vijji vingi kuliko CHADEMA mwaka 2004, na kura nyingi kiasi kuliko CHADEMA mwaka 2005; kupata viti vichache na kura chache kuliko CHADEMA mwaka 2009. Hali ambayo imefanya rasmi CHADEMA kuwa chama mbadala wa CCM Kigoma Kusini badala ya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo kupitia NCCR kurejea CCM.

  'Mbunge' Muslim Hassan ni vizuri akajitokeza wakati huu kwa kuwa gazeti la Mwananchi ambalo awali lilikuwa linaipa nafasi CHADEMA kushinda Kigoma Kusini kupitia kwa Kafulila sasa limebadili Kauli yake na kuandika habari za kiuchambuzi kuwa NCCR Mageuzi ndio itayoshinda baada ya Kafulila kuhamia chama hicho.

  Tukiweza kumpata Muslim Hassanal, tutaweza kuwafanya Mwananchi wakawapambanisha na Kafulila; CHADEMA na NCCR ili watanzania tujue yupi hasa ni mbadala wa kweli wa CCM Kigoma Kusini na kote nchini.

  Asha
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Dada Asha,
  Good to see you back.
   
 3. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2009
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Hii inahitaji uchambuzi wa kina kwani itasaidia kutupa picha halisi.
   
 4. Mwita Maranya

  Mwita Maranya JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2009
  Joined: Jul 1, 2008
  Messages: 10,569
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145

  Dada Asha, unachokifanya hapa ni kumnadi Muslim kama mgombea wa kigoma kusini kama ambavyo kafulila anajinadi kugombea huko kigoma kusini.

  Hakuna sababu yoyote ya kuanza kulialia na gazeti la Mwananchi kwamba limekuwa linamnadi kafulila tangu ahamie NCCR kinyume na hapo awali ambapo walikuwa wanainadi chadema. Wao Mwananchi inawezekana kwa utafiti au uchunguzi wao wamegundua Kafulila ndiye yuko kwenye nafasi nzuri ya kushinda. Na kwa bandiko lako inaonekana dhahiri shahiri kwamba ni kweli uongozi wa CHADEMA umegawanyika juu ya mtu ambaye angekiwakilisha chama kwenye uchaguzi mkuu wa 2010 na huenda ndio sababu ya kafulila kuondoka, huenda amegundua akibaki CHADEMA hatopewa nafasi ya kugombea akaona bora aondoke mapema akajiandalie mazingira ya kuwa mgombea huko NCCR.

  Kama Muslim alitoa ahadai asizoweza kutekeleza wakati anagombea 2005 (maana inaonekana hakuwa na uwezo wa kifedha hadi wazee wa chama wameamua kumchangia wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa 2009) inaonekana aliwaongopea wana Kigoma na inawezekana kweli hao wazee wa CHADEMA wanaomuunga mkono waliamua kumpa msaada huo wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa ili wapate sababu ya kusema kwamba ndiye kafanikisha ushindi wa chama kwahiyo lazima agombee.

  Nadhani njia muafaka ilikuwa ni kuwapambanisha Muslim na kafulila kwa kufuata utaratibu wa chama kwa mujibu wa katiba yenu (kama mnaiheshimu) hatimaye mpate muwakilishi bora kwa maslahi ya chama chenu na demokrasia kwa ujumla.

  Halafu inaonekana kitu demokrasia ndani ya chama kinachojiita cha demokrasia na maendeleo bado ni utata mtupu. Kwahali hii hakuna sababu ya kumlaumu Kafulila kuamua kujiunga na NCCR, wacha ajaribu bahati yake huko kama ndiye anakubalika au la, wananchi wa kigoma kusini ndio wataamua.

  Cha msingi hapa ni kujiandaa kukabiliana na kafulila akiwa nje ya chadema kwakuwa ndani ya
  CHADEMA mmeweza kumdhibiti(maana hata uchaguzi wa vijana amelalamika kwamba ulifutwa kwa sababu wenye chama hawakutaka kafulila aongoze BAVICHA), kwahiyo lilifanyika zengwe ili uchaguzi ufutwe na ufanyike utaratibu wa kumdhibiti kafulila na kweli inaonekana kwa hilo wenye chama wamemuweza.

  Ni hayo tu!
   
 5. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #5
  Dec 3, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mheshimiwa

  haitwi Muslim Hassanal ni Muslim Ansarary.unamuona Handsome mbona wewe ni mwanamke ambaye jike/dume.

  Jamii ya waasia kutoa zawadi au sadaka ni jambo ambalo jadi yao, hayuko kwenye kampeni.
   
 6. E

  Eddie JF-Expert Member

  #6
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 28, 2008
  Messages: 516
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Asha you cant get over Zitto, kila uchao unatafuta bifu lisilo na tija.

  Dynamics za siasa zina change ndani ya muda mfupi, kama mwananchi waliona Chadema watashinda kutokana na tafiti zao, leo wakisema wanashinda NCCR imekuwa nongwa?

  Huyu Muslim kugombea ni haki yake kama ambavyo ww utakavyo gombea Kawe.

  Kuwa muwazi humtafuti Muslim bali unamtafuta Zitto na kwa mbinu hizi za kitoto umenowa!
   
 7. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #7
  Dec 6, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Achana na huyo mwanamke, ana lake jambo. Hivyo vigodoro alivyogawa Muslim kwenye zahanati mbalimbali kigoma ndio anaona ametimiza ahadi zake kweli kweli. Mbona hasemi kuhusu visima? Aache vizingizio vya serikali kutomjibu barua yake ya kutaka kuvichimba. Angeweza kuchimba hata bila kibali cha serikali. Mbona watu wanachimba makaburi na kuzikana?

  ........ndiyohiyo
   
Loading...