Bin Shaib
JF-Expert Member
- Aug 1, 2019
- 1,434
- 1,363
Wana jukwaa habari za Alhamis hii njema iliyo njema machoni pa Mungu ametuwezesha kuiona hatunabudi kumpa sifa na utukufu, [emoji122]
Maada yangu mimi ni kijana ambaye nimeishi maisha ya Mama pekee bila Baba mzazi ikiwa na maana kwamba toka nizaliwe sijawahi muona baba yangu na wala simfahamu.
Na mama yangu hajawahi kunionesha wala kushughulika kuhusu hili, kuna kipindi mambo yalikuwa yakibadilika nyumbani hadi namkumbuka baba najisemea labda kama baba angelikuwepo haya yote yangewezekana,
Nilikuwa nakaa nalia kwa kulalamika baba yangu kwanini mama alinificha ?.nilishangaa hadi mama nilikuwa nikimkosesha raha kabisa, basi kwa huruma ya kumhurimia mama nikawa njisemea tu poa kwa vile nisha kuwa hamna noma.
Ubini wa baba yangu naufahamu, majina yote matatu, kwa maana yapo kwenye cheti changu cha kuzaliwa.
Na nilimuuliza akasema haya ndo majina ya baba yako mzazi,
Majina ya baba ni:
#SHAIB HASSAN MUSSA
Siku moja mama alinieleza kisa chote kwamba :
Sijajua kuwa mahusiano yao kati ya baba na mama yalianza mwaka gani, Kwa maana mama alinambia wao walipotezana mwaka 1994 hapa mkoani Mwanza walikuwa wakifanya kazi kwenye kiwanda cha (plastics )cha kutengeneza vyombo vya bondo.
1994 walipotezana nikiwa tumboni nadhani mtakuwa mmenielewa.
Kwao baba ni mzaliwa wa Biharamulo lakini sijawahi kumtafuta baba yangu, natamani kumuona japo nimfahamu tu.
Mpaka sasa sijajua yupo wapi, je atakuwa Biharamulo, je, atakuwa Mwanza au atakuwa wapi???????
Wana jf ntampata baba yangu mzazi?
Je, nikitumia mitandao ya kijamii ntampata?
Mbarikiwe nyote.
[emoji2398]Bin Shaib Classic 2020.
Sent using Jamii Forums mobile app