Namsaidiaje?

Mkuu hapa inabidi uwe ngangari na kupiga marufuku uhusiano uliopo kati ya mkeo na huyo jamaa na una sababu za kutosha za kufikia uamuzi huo. Hata mawasiliano ya simu usiruhusu, kwenda kazini kwa mkeo marufuku kwa kifupi wakate mawasiliano ya aina yoyote na wakati huo huo uendelee kufuatilia kwa karibu ili kuhakikisha maamuzi yako yanafuatwa. Kama hutajali rudi hapa kutufahamisha maamuzi yako na yatakayojiri siku za usoni. Kila la heri katika kunusuru ndoa yako.
 
Ninakushauri umualike huyo jamaa na mkewe nyumbani kwako na mkeo akiwepo, then umwambie jamaa kuwa mkewe alikuja kushitaki juu ya mkeo kuwa karibu na mmewe, inavyoonekana wewe na mke wa jamaa hamfurahishwi na mienendo ya wawili hao hata kama wao na familia zao ni marafiki wakubwa kuna mambo mengine ukishaingia katika ndoa huwezi kuyaendekeza. Jadilini nyote wanne kwa pamoja muwekane wazi natumaini inaweza saidia. Mwisho kabisa You are the man of the house huna sababu yakuogopa kuuliza kituchochote kwa mkeo vinginevyo wewe pia utakuwa unachangia kubomoa nyumba yako ukiendelea kukaa kimya kwasababu mkeo ataona kila kitu unachukulia poa hivyo hata yeye hataogopa kuendeleza ukaribu na huyo rafiki yake. Wake up please before it is too late...
 


Mpwa suala la terms linakuja kwa kuwa tayari kuna thirdy part...

Nadhani mpwa hujawahi kukutana na situation ambapo mwanamke anakuwa dilemma...

Na vilevile hujawahi kutana na mwanamke ambaye anaishi nawe kwa kuwa tu mna ties zijulikanazo mbele ya jamii...

Bado mpwa nasisitiza kuandika, lazima kuwe na kikao kizito tena ikiwezekana jamaa awe na jambia pembeni...

Lazima mwanamke akiri kuwa anataka nini, hata Mungu alipoona wanadamu hatueleweki aliweka pande mbili...

Mtindo wa pande mbili ndio mtindo fair, ni mtindo wa uzani kama ifanyavyo mizani au sheria za mahakama...

Kama mwanamke atasema yupo tayari kuendelea na ndoa, basi kuanzia siku hiyo huyo kidume mwingine apigwe mkwara mzito na aelezwe kabisa akileta chokochoko yoyote kile kipanga kitahusika kutenganisha mirija ya hewa inayopita kwenye koromeo...
 
Pole sana mkuu

Mimi naona tayari mke wako keshaingia kwenye mahusiano na unatakiwa uyavuruge kwakumtumia mke wajamaa. Bahati nzuri umeshaweza oengea nahuyo shemeji kwahiyo mambie tu azidishe presha kwamumewe aache hata mawasiliano nawife wako ila usije ukajisahau mkawa karibu nashemeji hiyo noma

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
....Na hiyo laptop irudishe kwa mwenyewe haraka sana.
 

Dah, Thank u mkuu. @least i can take a piece of advice without my man of the house status being questioned
 
pole ndugu! kitu cha kwanza vunjeni mipaka! hiyo ,mliyo jiwekea maana inaonekana ndio chanzo sasa cha kuanza kuhisi utaumia muda au umeshaumia long time. Na kama kweli anakupenda atakubali kuivunja. Pili mwambie yeye sasa ni mke wa mtu na asifanye mambo kwa siri maana siri kwa wanandoa ndio anguko lao kubwa. Tatu naamini nyie mna wasimamizi wa ndoa mimi naamini wasimamizi wa ndoa ni walezi au wachungaji wenu wadogo sijui imani yenu. sisi katka ndoa yetu wamefanyika msaada mkubwa na kama kuna jambo lolote linaishia katika level ya wasimamizi tunaendelea. Nne inawezekana pande zote za watuhumiwa zimechoka ndoa zao wanaona sasa ni wakati wa kuwa close zaidi, yani mke wako kakuchoka pamoja na yote uliyosema na jamaa pia kamchoka wa kwake now the equition cannt balance! the solution ni kila mmoja kujinyofoa taaratibu kwenye ndoa yake! inawezekana mke wako hata hiyo raptop aliambiwa au alimwambia jamaa amletee zawadi! Yani mm sitaruhusu mke wangu aletewe zawadi na mtu ambaye mara zote I suspect him! sasa kaeni chini muongee kwa kina kuhusu issue zenu. Lililo kuu kuliko yote mkuu mwombe Yesu yeye amesema tumtwishe fadhaa zetu! kama wewe ni mtu wa imani.
 
hii experience nzuri, hivi inafanywa na house girls au wives?
 

Aank kumbe mpwa unataka mashahidi tu lakini nia ni kutoa ultimatum!!!

Mi ningeanza na wa ndani then kwa simu yake angepiga yeye na kumuambia mume wangu anataka kuzungumza na wewe then naye angesikia yake!!!

Yaani ningemkimbiza mwivi kimya kimya mpaka aelekee polisi mwenyewe
 
daaaaaaahhhh PetCash kwanza nikueleze thread yako imenimaliza nguvu,nimeiona nikaishiwa pozi maanke najaribu kujiweka under your shoes na kuona jinsi hali unavyokabili ni ngumu kiasi gani nabaki naumia mwenyewe ndani ya moyo.Pole sana kwa kuwa katika wakati mgumu.Naomba nikushauri haya yafuatayo labda yatasaidia kwa kiasi fulani:

1.tambua kwamba hilo ni tatizo tayari ndani ya ndoa na maisha yako kwa ujumla,so kinachotakiwa hapo ni kulikabili na sio kulikimbia kwani kukimbia matatizo yetu sio suluhisho hata kidogo.

2.huenda tokea mwanzoni mkeo na rafikiye walikuwa wamefikia hatua ya upenzi ila sema ndo hivyo tena labda walikuwa kidogo na maadili na wakaweza kujiwekea mipaka,na labda hawakuishia kuoana kwa heshima iliyokuwepo baina ya familia zao mbili(lakini mioyoni kila mmoja anatamani wangekuwa pamoja its possible)

3.No way mkuu hii ndo njia peke itakayomaliza mgogoro wako ulionao kichwani kwa sasa,usifikie mkataa wa fasta kuwa mkeo anampenda jamaa(japo hilo pia lawezekana pia)
a).anza kufanya uchunguzi wa chini chini(mkeo aisshtukie chochote)chunguza anatumia muda mwingi kiasi gani kuwasiliana na jamaa kwa maongesi ya simu au hata sms.

b).panga hata visafari vya uwongo ili ujue akibaki peke yake anautumia muda mwingi peke yake akiendelea na shughuli zake au anutumia kuwa pamoja na huyo mbeste wake kama kumtembela nyumbani ofisini na n.k.

c).tembelea ofisini kwake bila taarifa na bila yeye kujua na mara kwa mara ili ujue ikiwa jamaa anamtembela wife mara kwa mara na kwa minajili ipi na wife anampokeaje na analichukualiaje hilo(hapa ukigundua jamaa huwa anenda ofisini kwa wife often na wife anaona poa tu na wala hakutonyi kitu jaribu kumuuliza kiujanja aisishtukie kitu akikuambia ukweli pumua kidogo na ujue kuwa huenda kweli wenzetu uzungu untaka kuwaponza,ila aikpiga chenga tu oohh hapa huwa haji kabisa au mara moja moja shtuka washa taa nyekundu kichwani)

d).panga mlo wa jioni au outings yoyote mkiwa wote watatu au wanne(kama mke wa jamaa akirudi)huko utaona reaction itakoyoweza jitokeza baina yao(kwani penzi ni kikohozi,na hope we pia uliona baadhi ya ishara kutoka kwake kuwa amefall kwako na kukupa go ahead ya kumuaproah,tumia hizohizo pia kujua ana feel nini kwa mjamaa)

Mwisho mkuu ukishafanya utafiti wako na kugundua kuwa watu hao wanapendana,mchukue wife kaa naye chini na umuulize kwa upole bila kugomba mfanye ajihisi salama na huru,mweleze matokeo ya utafiti wako ukiwa na proof halafu usikie maoni yake(kama si msaliti na si mwongo ukimpa evindence za kutosha huenda akafunguka na kukueleza ya moyoni hasa akijua pote alipokuwa anapita ulipita pia hatakuwa na jinsi ya kudanganya soo ni obvious atakwambia ukweli ikiwa na feelings kwa huyo jamaa au la)akikwambia kuwa anahisia naye(japo hii si rahisia sana ila kama mmkeuwa mnaishi vizuri inawezekana na huenda akaanza na am sorry my husband najua hili sio jambo zuri kwako hata kidogo lakini naomba tu niwe muwazi kweli nilikuwa nampenda sana lakini hivi nina wewe simuwazi yeye tena na hata ukaribu niliokuwa nimeanza kuwa naye naufuta kama unakauumiza mwanzoni sikujua kuwa unaumia ila as long as umeniambia i promise i will be faithfull to you na nitapunguza ukaribu ili uwe na furaha)hii inawezeakana ikiwa tu mmekuwa mnaishi naye vizuri na ikiwa ana lepe la aibu na maadili fulani ndani yake,na kwa kuwa ulisema u were the first huenda hiyo pia ikamimpress kustick na wewe as inasemekana a woman will never forget the first man to make love with,ikitokea akakiri makosa yake na kuomba muendelee basi waweza mpa nafasi na kuzidisha upendo kwake,na ukiona najisahau na jamaa wake unamshtua then u go on.

Lakini kama ikitokea akakueleza ukweli kuwa anampenda jamaa sana na anahsi kuwa moyo wake haupo kwako tena mpe uhuru(inahitaji kujikaza kiume vinginevyo utajikuta hujui unachokiongea na mwishowe kuwa chizi)mwambie muende mahakamani mpeane talaka kila mtu ajijue,kama atavunja ndoa ya jamaa ili ye achukue nafasi au nini ni juu yake huku na we unatafuta ustaarabu mwingine(mkuu it's not easy lakini itakubidi ufanye hivyo kwani tofauti na hapo mtakuwa ndani ya ndoa kwa ajili ya mazoea na si mapenzi jambo ambalo halifai kwani ndoa inapaswa iunganishwe na mapenzi tu na si vinginevyo,na pia unaweza kujikuta umekuwa mtumwa wa mapeznizi unafanya mambo ili tu kumimpress wife asimfikirie jamaa).


Kiukweli mkuu uko kwenye verryyy hard situation mi mwenyewe inaniumiza kichwa :confused2: :confused2: :confused2: :confused2:,samahani kwa hotuba ndeeeeffffuuu ni kwa kuwa hata mi natapatapa kutafuta solution ya hilo janga,hope nitakuwa nimesaidia kwa kiasi fulani.
 
Last edited by a moderator:

Mpwa yote heri tu ili mradi huyu mwivi wa mali za watu ajue 'hakuna mtu anacheka na kima'...
 

You have said it all hapo kwenye bluu. Nahisi hapa kuna;

i) Breakdown of communication - Jamaa ameona laptop, hajauliza. Amegundua kwamba laptop mkewe aliletewa zawadi na rafiki yake na imeshasababisha mtafaruku mkubwa kwenye ndoa nyingine. Bado amekaa kimya. Wala hajauliza.

ii) Yaelekea huyu bwana anamuogopa mkewe, na pengine mkewe ana ''defensive mechanism'' ya kukimbilia ugomvi au kununa ili kukatisha mazungumzo pale anapoulizwa. Hilo nalo ni tatizo.
 
piga mkwara mzito halafu fatilia kwa siri kama bado wataendelea kuwasiliana...


kama ungekuwa unaweza kuwa na moyo wa chuma wa kuvumilia na kufanya ujasusi basi vumilia na fatilia huo ukaribu wao kimya kimya..hakikisha wife hajui kama unamfuatilia..ila angalia manake mwisho wa ujasusi usije kuishia jela bure
fanya ujasusi kwenye simu yake ili ujue mawasiliano yao yakoje...pia email km una access na mail yake chunguza,..

fatilia kila wakati wife anapokuwa hayupo hm au visit her in her office surprisingly several times

inawezekana wasiwe wapenzi lkn wanakaribia...

WEKA MIPAKA MIPYA NA HAKIKISHA WIFE ANATII
 
Nisikilize kwa makini:
Huyo sio kuwa ana culture za kizungu ila anaemitate uzungu, ujue wazungu walioendelea huwa wanapotaka kujifungua mtoto either wazazi wao au mke/wote kwa pamoja huomba rikizo hata pengine kuacha kazi na kuandaa muda wa kulea mtoto wao ambapo mtoto anapo kuwa karibu na wazazi hufundishwa kusema ukweli tu! mfano akiuliza hiki ni nini? hata kama ni papuchi huambiwa hii ni papuchi ila hauruhusiwi kutaja mbele ya watu!!!!!!! kwa hiyo hata anapo amua juu ya mahusiano kama wewe ni rafiki utabaki kuwa rafiki, kama ni boy friend hatakuonea haya popote kama ni mume utabaki kuwa mme tofauti na waigizaji wa huo utamaduni kama alivyo mke wako huwa ni waongo kwa kuwa hulelewa na wadada wa kazi ambao akimpiga humfundisha uongo toka anavyo jitetea sikumpiga analia mwenyewe sasa yule hujifunza kumbe ili usipigike hapa unajitetea kwa kudanganya naye akifanya kosa hajui kukiri na kuomba msamaha! Huyo mkeo una mahala pa kuanzia mwite mweleze uliyo yasikia mtake aseme ukweli na simama kama mwanaume mkanye huyo jamaa na onyesha hauko tiari kumuacha mkeo na yeye akiendelea utacho kifanya atajuta kumfahamu mkeo ila wasijue ni nini? Waonyeshe umekereka na uhusiano huo! Vunja vunja hicho ki lap top mbele yao na muonye mkeo kuwasiliana na jamaa na wewe acha mawasiliano na huyo ex wako! Simama kama mwanaume kwenye ndoa ilinde kwa nguvu zako zote!!!!!!!!!!!
 
Watu wengine mnazaliwaje bila wivu, hasira wala ujasiri!!!!!!!!!!! duh angekuwa anakodishwa huyo mke ninge kodi nikakaa naye japo wiki, huyo jamaa na mke mwenyewe wange kata mawasiliano toka day one nakutanishwa naye!!!!! na hata huko tusinge fika ini short asinge nipeleka kunitambulisha mtu wa hivyo!!!!!!!!!! Pole sana.
 
Hata kama hawajaanza, ila analea ugonjwa.

Mie ndio huu uzungu siuwezagi kabisa, sijui hugs nisizozielewa siwezi.

Ni bora kuwa muwazi kwa mwenza akazoea kabisa na kujua kipi kinakuumiza akifanya. Tatizo linakuja pale tunavumilia na kufa na tai shingoni, mwisho wa siku maumivu yanatuelemea.

 
Last edited by a moderator:
Mie nahisi social status ama class zinatofautiana. Mdada inaelekea kakulia mambo safi na uzungu, na kijana kakulia kawaida. Hizo status za walikotokea zimemfanya mme awe na inferiority complex.

Ndio maana anaona kitu kinamkwaza, bado anaogopa kumuuliza mkewe.

 
Kaka sijui ndoa yako ina miaka mingapi..inaonekana unamtreat mke wako kama yai,may be kwa sababu anatoka kwenye welloff family...kwenye ndoa mambo ya urafiki uliekuepo before you wed should stop Asap..urafiki gani wa kumkiss my gal eti uzungu..kwa nini yeye asije na gf wake amkiss kama he is fond of kissing...isitoshe jamaa anamletea mke wako gift! Anamletea laptop kama nani?hana wadogo zake awape hiyo laptop,kaka umezubaa mpaka mpaka mke wa mwizi wako ndio ndio anakuja kukushtua! Kaka ndoa haitaji uzungu huo,hata wazungu hawafanyi hivyo,kwa nini asiwatembelee kwako awape zawadi mbele ya mke wake na wewe ukiwepo? Hey bro wake up bhana story yako imeniuma sana,hata hao wazungu mnao waiga huwa wanatembeleana as family sio kupeana vijizawadi uchochori...Do this comrade,Mwambie wife umesikitishwa sana na tabia yake ya kutaka kuvunja ndoa ya jamaa,na amefanya hivyo kwa sababu amechukulia your sweetness for weakness,kuanzia leo hautaki mawasiliano aina yoyote btw them,hiyo laptop amrudishie tena mkiwa wote,mbele ya mke wa jamaa...on top of that mkanye mke wako,mwambie achague wewe au rafiki,weka miongozo kwenye ndoa yako,hawa mama zetu are weak ndugu yangu.be a man kaka dont be blinded by love.hata kama mkeo ndie bread winner be a man bhana
 
Hiyo mipaka ndo ilioharibu kila kitu,hapo dawa tumia mfumo dume ndo dawa,Angalie usiwe bushoke
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…