Nampenda sana Hoyce Temu, naipenda roho yake

Azarel

JF-Expert Member
Aug 25, 2016
28,414
39,490
Habarini Wadau,

Sio siri huwa ninampenda sana Hoyce Temu aliyekuwa Miss Tanzania nafikiri wa mwaka 1999.

Huyu dada amekuwa akionesha roho safi na upendo wa dhati kabisa kwa wasiojiweza na hasa watoto.

Katika kipindi chake cha "Mimi na Tanzania" Huwa anawashika, anawakumbatia na kuwajali watoto wenye matatizo makubwa kiafya kama vile ni wa kwake wa kuwazaa.

Pia huwa anasisitiza wachangiwe na kupatiwa misaada mbalimbali.

Mungu akutunze Dada Hoyce Temu na azidi kukupa moyo wa huruma.

AAMIN.
 
Ametenda jambo zuri sana kuonesha upendo kwa watoto na hata watu wengine wenye matatizo...

Hakika mwenye roho nzuri hulipwa thawabu!!

[HASHTAG]#RespectForHumanity[/HASHTAG]
Amen
 
Unaipenda kazi yake au unampenda yeye kivingine.?

Binafsi napenda kazi yake na hayo mengine unayoyawaza wewe pia. Mwanamke kujitambua, roho safi, ukarimu, uzuri ni ziada tu. Hoyce popote pale ulipo naomba uje unishike mkono au hata kunipa busu la shavu roho yangu ipone. Nimeoa lakini sina raha, nakuwaza wewe tu kila kukicha.
 
Ukiusikia upande wake wa pili ( Side B ) unaweza ukatamani umchukie Milele labda pengine hadi mtakapoona ama Jehanam au Paradiso.
Daah..kumbe na yeye ana mambo mengi tofauti na tunavyomfahamu wengi?
 
Habarini Wadau,

Sio siri huwa ninampenda sana Hoyce Temu aliyekuwa Miss Tanzania nafikiri wa mwaka 1999.

Huyu dada amekuwa akionesha roho safi na upendo wa dhati kabisa kwa wasiojiweza na hasa watoto.

Katika kipindi chake cha "Mimi na Tanzania" Huwa anawashika, anawakumbatia na kuwajali watoto wenye matatizo makubwa kiafya kama vile ni wakwake wa kuwazaa.

Pia huwa anasisitiza wachangiwe na kupatiwa misaada mbalimbali.

Sikuwahi kujua kuwa kuna wadada wa kichaga wana roho nzuri hivi kwajinsi wanavyosemwa humu.

Mungu akutunze Dada Hoyce Temu na azidi kukupa moyo wa huruma.

AAMIN.
Mtoa mada hicho kichwa kwenye avatar yako ni chako maana kila siku inakibadili
 
Back
Top Bottom