Nampenda mke wangu

Nampenda mke wangu

LELELU

Senior Member
Joined
Jan 29, 2018
Posts
167
Reaction score
259
NAMPENDA MKE WANGU..
sijuti japo dakika
kumpenda mwari yule
na kwao nilishafika
Kuchunguza pole pol

Nikapewa data zake
Tena kinagaubaga
Na sifa za waze wake
Hakika ndizo kaiga

tabia yake adimu
sijapata kuiona
Mwingi wa kutabasamu
Nyumbani atulizana

Nimedata na niqabu
baibui vazi lake
kafunzwa kwao adabu
kanifaa kuwa mke

Karidhia yangu hali
Sioni kwake kasumba
Basmati wake mwili
Umbo lake moja namba

mtaalamu jikoni
Kwa hili namuelewa
nakomba paka sahani
Nikizidi kunogewa

Mwenzenu nabembelezwa
Kwa uchovu wa kazini
kifuani natulizwa
Na maneno malaini

Mke wangu katulia
Wala sio mcharuko
Sie kiguu na njia
kucha haeshi vituko

*Chakula nala vizuri*
*Na Maneno ya mahaba*
*Matonge anahimili*
*Anakula na kushiba*

Hasira anadhibiti
si mtu wa kupayuka
Kumpiga haupati
Wala haombi talaka

Vyakula anavyopika
Sijawai kukinai
Anaziweza pirika
roho yangu yafurahi

Macho yake alegeza
Pindi nikimtazama
Haeshi kunikonyeza
Anipa yangu heshima

yarabi nijaalie
nidumu na huyu mwana
Riziki nifungulie
na tuzidi kupendana

..abu hafsa..
 
Heko kwako mtunzi
Mistari imewiva
Ujumbe tumeupata
Mola awe nanyi

[emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122] [emoji122]
 
NAMPENDA MKE WANGU..
sijuti japo dakika
kumpenda mwari yule
na kwao nilishafika
Kuchunguza pole pol

Nikapewa data zake
Tena kinagaubaga
Na sifa za waze wake
Hakika ndizo kaiga

tabia yake adimu
sijapata kuiona
Mwingi wa kutabasamu
Nyumbani atulizana

Nimedata na niqabu
baibui vazi lake
kafunzwa kwao adabu
kanifaa kuwa mke

Karidhia yangu hali
Sioni kwake kasumba
Basmati wake mwili
Umbo lake moja namba

mtaalamu jikoni
Kwa hili namuelewa
nakomba paka sahani
Nikizidi kunogewa

Mwenzenu nabembelezwa
Kwa uchovu wa kazini
kifuani natulizwa
Na maneno malaini

Mke wangu katulia
Wala sio mcharuko
Sie kiguu na njia
kucha haeshi vituko

*Chakula nala vizuri*
*Na Maneno ya mahaba*
*Matonge anahimili*
*Anakula na kushiba*

Hasira anadhibiti
si mtu wa kupayuka
Kumpiga haupati
Wala haombi talaka

Vyakula anavyopika
Sijawai kukinai
Anaziweza pirika
roho yangu yafurahi

Macho yake alegeza
Pindi nikimtazama
Haeshi kunikonyeza
Anipa yangu heshima

yarabi nijaalie
nidumu na huyu mwana
Riziki nifungulie
na tuzidi kupendana
Na mimi wacha nikajitafutie ujiko kwa mke wangu, nitamwambia nimetunga mie hahaha Asante mtunzi credit zikufikie
 
Kama hana chura,Uzi wako ni Outdated broda.
ahaha

tatizo kamsifu mkewe yeye kwa jinsi alivyo...

mungine atakuja atasema kama hana ajira hamna kitu...

sasa wewe anzisha yako ya chura
 
Back
Top Bottom