Nampenda ila kuwa na mahusiano nae naogopa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nampenda ila kuwa na mahusiano nae naogopa.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by HAMY-D, Sep 22, 2012.

 1. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Jamani wanajamvi naombeni mnishauri katika hili jambo, kama title inavyojieleza hapo, mwenzenu napata shida sana kuhusu huyu mtoto.

  Ni msichana ambae tupo nae darasani, kwa kipindi cha mwaka mzima sasa tumekuwa nae pamoja tukiishi kama marafiki wa karibu. Huyu msichana ni mrembo na anajulikana kila pembe ya hapa chuo kwa uzuri wake.

  Wasichana wenzake huwa wana mzungumzia kwa urembo wake huo na kwa upande wa wavulana ndio kabisaaa kila mmoja wetu ametubu kwa uzuri na urembo wake.

  Mioyo ya wavulana hapa chuoni huwa inatudunda kila mahala tunapomkuta amesimama au anapotembea, kwa ujumla mtoto anajua kuteka akili.

  Ametokea kuwa na mimi karibu sana na kwa kipindi kirefu huwa tunakaa pamoja. Mambo ambayo huwa tunaongea mara nyingi hayana mahusiano na masomo ingawa mara nyingi huwa tunapenda kufanyia mazungumzo yetu darasani na kwenye vimbweta(mawe yaliyoundwa kama dawati).

  Amekuwa akiniambia kila kitu kinachohusu maisha yake, kuanzia familia, watu aliokuwa nao kwenye mahusiano na ndoto zake.

  Mara kwa mara alikuwa ni mtu wa kuniangalia huku ana chekacheka, nikimuuliza vipi anabaki kusema "huh huh".

  Tatizo kubwa lililokuwa linanikabili ni idadi ya simu zilizokuwa zinaingia pindi nikiwa nae, yani ni kero.

  Simu nyingi zinazoingia utasikia ananieleza, huh huyu ni "cousin" mara huyu ni "gud friend of mine".

  Hapo hapo mara anaaga kwa kusema "je, naruhusiwa kwenda kumuona mtu fulani mara moja?".

  Jambo linalonishangaza ni kuwa busy sana kwa simu yake, huku akinisisitiza kuwa yeye ameachana na mtu wake ambae mimi namfahamu, huku akisema ajaumia kabisa na kuachana huko na huyo mtu wake.

  Sasa jamani naombeni ushauri wenu, huyu msichana kweli amekaa akilini mwangu, lakini naogopa kuanzisha nae mahusiano ya kimapenzi. Je, nipo sahihi?
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Utakufa kwa presha wewe....kimbia usiangalie nyuma. Ukiendelea utarudi JF na kilema cha akili
   
 3. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  asante mkuu kwa ushaur wako.
   
 4. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Okey...tena hao wanaopendwa na wengi (sio wote) huwa hawapendi kuwa kwenye umiliki wa mtu mmoja 100%...maana yake sifa anazopata zitapungua......na wewe kujiamini kwako kutapungua sana!
   
 5. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Umtumikie Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote, kwa akili yako yote na kwa nguvu zako zote. Achana na mambo haya ya wivu na tamaa za kimapenzi. Mwombe Bwana Mungu wako akupe mpenzi wako uatakayemwoa na hakika maisha yenu ya mapenzi na upendo ktk ndoa yenu mtaufurahia sana. Mapenzi nje ya ndoa ni wizi. Bwana Mungu awabariki sana
   
 6. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Mkuu unayoeleza ni sahihi kabisa, lakini kwa hali kama hii nitawezaje kumkimbij? npo nae darasa moja, halafu ni mtu wangu wa karibu? au nivunje nae urafiki?
   
 7. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,313
  Likes Received: 2,271
  Trophy Points: 280
  Angekuwa mpenzi wako kabla ningesema ndiyo vunja urafiki kwa sababu unaweza kuumia, lakini kwa sababu ni rafiki yako ondoa mawazo ya kuwa mpenzi wako kabisa mchukulie kama rafiki tu. Kuumia kwako sasa hivi ni kwa sababu ulikuwa umeshampigia hesabu.............Sasa hesabu zimegota unarudisha mahusiano ya kirafiki.

  Na hutakiwi kufuatilia maisha yake. Piga story nae as if mnapitisha siku
   
 8. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Mkuu mimi sijaoa na sina mpango huo kwa sasa, lakini kama ilivyo ada, kabla ya kuingia kwenye ndoa inabidi umpate mtu kwanza ili msomane tabia na mambo mengine ya msing, ili msipate shida katika ndoa yenu.

  Mimi ni mwanachuo na nimekutana na huyu binti ambae nimemuelezea kwenye hii thread hapa. Ningeomba ushauri wako kutokana na nilichokieleza humu itasaidia sana.
   
 9. Ruttashobolwa

  Ruttashobolwa JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2012
  Joined: Feb 22, 2012
  Messages: 43,688
  Likes Received: 12,725
  Trophy Points: 280
  Na kushauri uzingatie masomo sana kuliko kumzingatia huyo msichana! Wala asikuumize kichwa!
   
 10. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 301
  Trophy Points: 160
  ngoswe, penzi kitovu cha uzembe.
   
 11. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Mtani wangu ulilosema ni jambo la msingi, lakini tukumbuke maisha sio shule pekee, hapa namaanisha kwamba kama nitazingatia shule, nikimaliza shule na nikipata kazi, utaniambia nizingatie kazi, lini nitazingatia moyo wangu na kutendea mwili wangu haki yake ya msingi?

  Mimi kwa umri wangu ninaweza kabisa ku-balance mambo yangu, lakini naogopa kutoa moyo wangu kwa mtu ambae sio sahihi.

  "don't give your heart to just anyone".
   
 12. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  We kijana wewe achana na hayo mambo..
  Si unasoma wewe? Kazana na masomo yako.
   
 13. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Bwana Kongosho nashukuru sana kwa mchango wako, ingawa umeutoa kwa namna yake lakini mwenye hekima atauelewa tu.
   
 14. Prisoner 46664

  Prisoner 46664 JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Dec 18, 2010
  Messages: 1,955
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 145
  Dah!..wanafunzi wa siku hizi..kaaz kwei kwei

  Kwani unachotaka ni nini hasa HAMY-D? Kama mnatumia muda wote pamoja unachotaka zaidi ni nini?..hadhari ndugu yangu, ukishaingia pale na huo urafiki utakuwa umeingia shakani..endelea kushikilia pembe hizo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 15. hovyohovyo

  hovyohovyo JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 8, 2012
  Messages: 540
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Nashangaa unampenda lakini hujamtokea, kisha wakati huo huo unapata wazimu ukihisi kuna watu wanakutaimu. Apply sasa.
   
 16. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #16
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Mkuu labda mngesoma thread kwa umakini kidogo, kwa hali hii michango mingi kwa namna ya ushaur nitaikosa, maana naona naambulia lawama kama vile nimefanya makosa.

  Ndio ni mwanafunzi na ninasoma, lakini nipo chuo kikuu. Mahala ambapo mahusiano ni mahala pazuri kuanzishwa na kama tukifanikiwa hapa chuo ni rahisi sana kwa watu kuoana.

  Naombeni ushauri utokane na thread na sio hisia binafsi jamani, nina heshimu sana michango yenu.
   
 17. kazikubwa

  kazikubwa JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2012
  Joined: Oct 8, 2010
  Messages: 598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Ah, kumbe watoto, napita tu jamani
   
 18. Root

  Root JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,116
  Likes Received: 12,825
  Trophy Points: 280
  Hao ni pasua vichwa hao yaani mi sipendi hii kitu
   
 19. Mgibeon

  Mgibeon JF-Expert Member

  #19
  Sep 22, 2012
  Joined: Aug 7, 2011
  Messages: 7,441
  Likes Received: 9,087
  Trophy Points: 280
  Kaka, mimi ni toto zuri kama limejiumba lenyewe, tatizo ni hizi simu....! Hua naumia sana, nimesurvive nae tangu nikiwa form 5 mpaka sasa namalizia degree yangu ya kwanza ila shughuli yake SI MCHEZO, natamani nijivue penzi ila nikihesabu muda na gharama nilizotumia najikuta natamani nimpige mimba tu.. Ushauri wangu huyo mtoto mnyukwa mpotezee tu, trust me 75% ya maisha yako na huyo mdada itakua ni kuzozana tu..! Education is a key..
   
 20. H

  HAMY-D JF-Expert Member

  #20
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 6,825
  Likes Received: 709
  Trophy Points: 280
  Mkuu nashukuru sana kwa ushauri wako, vilevile hiki kisa chako kimenipa mwanga fulani wa kufanya maamuzi kwenye hili swala langu.

  Nasema tena, nashukuru.
   
Loading...