Nafikiri hapa kinachokupa shida ni ikiwa hata kukubalia kwa sababu mbalimbali ikiwamo kuwa tayari kwenye mahusiano au kutokuwa tayari kuingia kwenye mahusiano.
Kumwambia hisia zako ni jambo muhimu sana. Lazima uwe jasiri. Jambo LA msingi, uwe tayari kiakili, unaweza kukutana na hali nilizozieleza hapo juu. Ukikataliwa, Kubali na ruhusu maisha yako yaendelee. Amino utakutana na mwingine na unaweza kujikuta una mahabs mazito zaidi.
Kama una nia ya dhati kabisa, tafuta njia nzuri ya kumueleza. Njia ya kwanza ningeshauri ukutane naye mwenyewe. Huna sababu ya kuwa na hofu kwani umeshajiandaa kisaikolojia.
Ukiona huwezi kukutana naye mwenyewe, basi tafuta rafiki yake wa karibu, akufikishie ujumbe. Pia, unaweza kumdodosa huyo rafiki ili kujua hali yake ya mahusiano, hii itakusaidia.
Kila LA kheri ndugu.