Nampenda binti wa kitajiri ila ana kiburi, jeuri na dharau. Je, nimuoe?

hata hayo maisha mazuri unayoyaona kwa familia ya huyo binti ujue kuna mwanaume alipambana..!,bado una muda wa kupambana na kufika walipo na hata kuwa zaidi yao as long as hujakata tamaa,weka kwanza vigezo vya mke unayemtaka mbele kama hajafit kwenye vigezo vyako na pia nafsi yako inakupa mashaka move on mkuu, usiendeshwe na woga wa maisha na mapenzi achana na hilo jipu kama hana values unazotaka.wazee walisema kosea vyote ila usikosee kuoa.

Sent using Jamii Forums mobile app
shukrani
 
Kijana acha ujinga narudia acha ujinga nasisitiza acha ujinga,Piga chini huyo manzi full stop.
 
Habari za uzima ndugu, nina binti mmoja nipo nae kwenye mahusiano. Huyu binti kiukweli kabisa kutoka moyoni ni binti ambaye si wife material (kwangu), ila kuna kitu huwa nakiwaza sana kichwani.

Huyu binti kwao ni watu wenye uwezo mkubwa sana kipesa, yaani wana pesa sana sana sana wameiacha familia yangu kiuchumi kwa asilimia kama 75%.

Nina kazi yangu na nina shughuli zangu zingine za kunifanya niishi mjini bila shida yeyote ile lakini kuna muda wazo kichwani linaniambia kwamba, nimuoe huyu huyu nimzalishe pia nikiwa na uhakika wa asilimia 100% watoto wataishi kwenye good-life hata kama ikitokea mungu amenichukua.

Nikiwa nawaza hivyo roho yangu inashindwa kunifanya nimuache huyu binti, ila ni binti mwenye kiburi, jeuri, dharau na mambo mengine mengi tu ila ndio nipo nae.

Naombeni ushauri wenu wa dhati ndugu zangu, ili nichukue maamuzi sahihi kabisa.
Lol mwanaume unataka mteremko wewe.Utadharauliwa wewe na ukoo wako wote.
 
Kidume kinaandika bila aibu nanukuu "eti najua nikifariki watoto wangu wataishi bila shida "je akitangulia huyo Mwanamke mada yake imenishangaza mno na kunisikitisha
atabaki bibi yake na babu upande wa mama, bado atasoma na kuishi kuzuri
 
Mapenz ya kizaz hiki ni balaa tupu yan tunapenda imradi tumependa tu.Me naona usiwe mnyonge kwake hata kama kwao wana wadhifa town...onesha uanaume wako nadhan akishajua upoje kichwani hata dharau atapunguza kwako.

Wanaume wengi tunafeli sana kuonyesha udhaifu wetu kwa wanawake ndo maana dharau zinakua kubwa sana.

kingine ni piga rungu, piga runguu mpk azilai ( joke )
Nakubaliana na ww mkuu...yan Ukishajionyesha ni dhaifu kwa mwanamke utadharaulika kama mtoa mada ..alivyo bwege
 
Wanaume wanazidi kupungua tu kila siku.

Kumbuka maisha mtakayo ishi kwenye mahusiano yenu ya ndoa ndio yatakayo zaa/jenga akili za watoto wenu
 
Back
Top Bottom