Namna ya kutengeneza Nywila (Password) imara

Life starts at 45

JF-Expert Member
Sep 22, 2015
976
932
Habarini wana jukwaa, ni matumaini yangu kuwa wengi wetu tu wazima wa afya.

Na ni wape pole wale wote walio wagonjwa pengine wapo kitandani au mahala pengine, basi Mungu awaponye na warudi katika hali zao za kawaida.

Basi bila kuwachosha niende moja kwa moja kwenye mada nilio waletea leo ambayo inahusiana na nywila(Password).

Nywila ni neno siri ambalo hutumika kumtambulisha mtu fulani katika mfumo. Nywila ndio imekuwa njia kongwe ambayo hutumika kutambua umiliki wa akaunti katika mifumo mingi japo kwa sasa kuna baadhi ya mitandao unaweza ingia pasipo kutumia nywila moja kwa moja.

Kutokana na umuhimu huo wa nywila basi imetupasa kuweka nywila imara katika mifumo tunayotumia kila siku, ili kuepusha mtu fulani kutumia account yako pasipo ridhaa yako wewe binafsi. Sasa ili kuwa na nywila imara kuna baadhi ya mifumo hupendekeza mchanganyiko wa vitu tofaouti tofauti na hivyo twende tukatazame sifa za nywila imara.

Sifa au vitu vinavyounda nywila imara(Strong Password).
1. Herufi ndogo(a-z), nywila imara inapaswa kuwa na herufi ndogo ambazo zitajumusha alphabet kutokea 'a' mpaka 'z'.

2. Herufi kubwa za alphabet (A-Z) mbali na herufi ndogo katika nywila, basi ni muhimu pia kuweka na herufi kubwa katika nywila.

3. Namba kuanzia sifuri mpaka tisa(0-9), ndio ili kuongeza uimara na kuweka ugumu kwa mtu kubashiri nywila yako basi ni muhimu pia kuweka namba katika nywila yako.

4. Special character('herufi maalum' sijui kama ni sahihi), herufi maalumu ni kama vile ~,@,#,$,%,^,&,*,(,),/ na zingine nyingi kama hizo. Hizi herufi nazo ni za msingi sana pale unapotengeneza nywila imara hivyo usiache kuziweka.

5. Sifa ya mwisho ni kwamba muunganiko wa sifa hizo hapo juu kuanzia namba moja mpaka nne inabidi angalau ziwe nane.


Sasa mara baada ya kuona nywila imara huundwa na vitu gani basi hii hapa chini ni mfano wa nywila imara lakini inayokumbukika,
1. *JamiiForum01#
2. U@w@e@z@o#Wa@Kawaida8

Sasa tuje kutazama vitu vya kuepuka pale unapotengeneza nywila yako.
Unapotengeneza nywila epuka kutumia taarifa zako kama nywila mfano majina yako, namba ya simu, tarehe, mwezi na mwaka wa kuzaliwa.

Pia epuka kutumia taarifa za mtu umpendae either mzazi, rafiki au mpenzi.

UPDATE
Pamoja na kuweka nywila iliyo imara lakini inashauriwa pia kubadili nywila yako kila baada ya miezi mitatu(3) na hapa ndipo wengi tunafeli maana kila baada ya miezi mitatu ubadili nywila na isitoshe wengi wetu tunamiliki mitandao mingi basi inakuwa ngumu.

Lakini ni vyema kujitahidi kwa ile mitandao uonayo ni ya muhimu kwako zaidi.

Asante kwa kuwa kusoma bandilo hili waweza ongezea niliposahau na kunisahihisha nilipokosea.
 
Ooh!! Somo zuri.

Inabidi nianze kuongeza na hizo Special Character kwenye nywila zangu kwani huwa nabase sana kwenye kuchanganya namba na herufi.
 
Password yangu ilikuaa nabadilisha herufi kuwa namba. Mfano Kama nialaikua nataka kutumia cybergates kama password nilikua naweka CY83R94T35 huu mfumo niliacha kuutumia baada ya kuona kuna baadhi ya tool kwenye debian zinauwezo wa ku cheza na password Za aina iyo
 
Waambie waweke na nywira ngumu lakini akaunti ziwe na maana sio unaweka nywira ngumu halafi akaunti yenyewe maandazi tu!
mkuu haijarishi account yako ni ya aina gani ni vyema kuwa na nywila imara watu wanaweza kuchafulia CV sababu ya kupata access ya account yako.
 
Back
Top Bottom