Namna ya kupata mfahili wa shahada ya pili?

blackdog

Member
Jan 9, 2011
89
8
Nina sikia watu wanapata mashirika kusaidia kujiendeleza kielimu,mimi naitaji sana lakini naona kama ndoto tu,nisaidieni nipate kusoma zaidi kwani bodi ya mikopo aitoi kwa shahada ya pili(master)
 
Nina sikia watu wanapata mashirika kusaidia kujiendeleza kielimu,mimi naitaji sana lakini naona kama ndoto tu,nisaidieni nipate kusoma zaidi kwani bodi ya mikopo aitoi kwa shahada ya pili(master)

jaribu kuwasiliana na hayo mashirika uliyoyasikia.
 
Nina sikia watu wanapata mashirika kusaidia kujiendeleza kielimu,mimi naitaji sana lakini naona kama ndoto tu,nisaidieni nipate kusoma zaidi kwani bodi ya mikopo aitoi kwa shahada ya pili(master)

Mpendwa wewe ni msomi wa shahada lakini unashindwa kuandika/kutamka neno haitoi, nahitaji badala yake unasema aitoi, naitaji? it is not fair.
Back to themain point/thread, naomba ujaribu kufungua hii link www.uio.no inaitwa Quota scholarship (kama umesoma undergraduate kwenye vyuo vifuatavyo:- UDSM, MUHIMBILI, TUMAINI, na KCMC). Huko utaona course ambazo ziko chini ya udhamini kulingana na chuo husika.

Ukipata ugumu usisite kuni PM kwa maelezo zaidi.

Good lucky!
 
Mimi ningekushauri tofauti kabisa kwamba achana na habari ya SPONSORS, why not be your own sponsor? Mimi namalizia dissertation yangu nasoma UDSM, sijalipiwa hata senti na hadi sasa nimeshalipa 2.2M bado kama laki tisa hivi naamini nitalipa ili nigraduate! Jiamini tu, try it, nikikuambia salary yangu na maisha yangu utashangaa but ni kwasababu najua ni mateso ya muda mfupi tu! kwanini usiniige? PM tushauriane, usitegemee kufadhiliwa bana! sorry kama ushauri wangu utaonekana kuwa mgumu
 
Hakuna haja ya kutafuta mdhamini,watanzania tumejizoesha vibaya kila kitu tunahitaji wadhamini,itafika wakati hata kuoa tutalazimika kusubiri msaada kutoka mataifa tajiri.RAHISISHA MAHITAJI YAKO,ONGEZA KIPATO CHAKO,UTAPATA UTAKACHO...kua mjasiriamali kwa kidogo upatacho na utaweza kujisomesha vizuri tu.jaribu sasa,na ipo siku utatembea kifua mbele na utawaeleza wengine siri ya mafanikio yako.
 
Blackdog ukisubiri kupata wafadhili ili usome, unaweza kushia hapo ulipofikia kielimu. Unaweza kuanza na mkopo kidogo kutoka kwenye taasisi zinazotoa mikopo. Nakushashauri utumie bank zetu. Kwa kufanya hivyo, utapata kianzio utakachotoa ili uwe registered. Baada ya hapo utaendelea kulipa kidogokidogo. Waweza kumalizia ada yote utakapokuwa umehitimu masomo yako kama chuo unachosoma ni cha public. Nilifanya hivyo nikafanikiwa. Kila lenye Kheri!
 
Back
Top Bottom