Namna ya kuongea wakati wa kumtongoza mwanamke

Namna ya kuongea wakati wa kumtongoza mwanamke

Kilaza

JF-Expert Member
Joined
Feb 28, 2013
Posts
3,324
Reaction score
1,379
Wakuu heshima mbele hii ni special kwa madomo zege "Ulishawahi kujikuta unatamani kuliko kumtongoza msichana mzuri sehemu fulani japo upate namba yake ya simu ila unajikuta huna jinsi yeyote au wazo juu ya nini cha kufanya au kuongea, unatamani kumfata nguvu miguuni zinakua zimekuishia unashindwa hata kupiga hatua moja kumsogelea, lile wazo pekee la kutaka kumsogelea linakufanya moyo uwende mbio, mikono iloane na jasho jembamba kukutoka huku akili yako ikishindwa kufikiria vizuri nini cha kuweza kuongea iwapo ukimsogelea?."

Unajua nini? haipaswi kuwa hivi ndo maana Waulizewanaume ipo kwa ajili yako ili kumaliza maswala madogo madogo kama haya, kukuondoa katika mazingira ya kutokua na maamuzi dhabiti na kutokujua nini cha kufanya ndani ya sekta ya utongozaji na kukufanya uwe mwanaume kiongozi na mtanashati kwa kujua ni nini cha kufanya na mda gani unapaswa kukifanya ili kuwa mtaalamu katika sekta ya mahusiano.

Kujiamini ni kitu kinachochukua nafasi kubwa na ndo msingi mkubwa katika mahusiano na hasa wakati wa utongozaji, na ndicho kitu mwanamke hutumia kumpima mwanaume na kumpa nafasi ya uwezekano wa kuwa na yeye au la, ila mara nyingi mtu hushindwa kujiamini kutokana na hofu ya kutokujua ni nini cha kufanya au kuongea wakati wa utongozaji.

Mwanamme ambaye huwa hafanikiwi kwenye utongozaji hufanya makosa madogo madogo kama kumpandisha hadhi mwanamke anayemtongoza mpaka kiasi ambacho anaifanya hadhi yake binafsi kuonekana ndogo na siyo tu anamtongoza mwanamke kwa wasiwasi na kutojiamini, bali anamtongoza hovyo hovyo bila mpangilio na zaidi ya hapo anamuweka wazi mwanamke kwamba anataka kumjua zaidi ya kawaida na anajitangaza bila kujijua kwamba, anahitaji na huyo mwanamke apendezwe naye hapo hapo.

Nayajua haya kwa sababu kwa muda mrefu na mimi nilikua hivi hivi, mtaalamu wa utongozaji huwa anasubira na huwa hapaparuki hovyo hovyo tu, kutongoza ni sanaa na inahitaji uelewa mkubwa na hata mimi iwapo ningelikua ndo huyo mwanamke sidhani kama ningelikubali hivi hivi, lazima atake kukujua kwanza ndo mambo mengine yafuate.

Ukitaka kuishia kusonywa na matusi juu ingia na mstari wa "Dada samahani nimetokea kukupenda nataka tuwe wote, kila nikikaa nakuwaza wewe, nikinywa maji nakuona kwenye glasi", bila kuangalia mazingira na papara za kusema yaliyo moyoni mwako, huu mstari lazima utakutokea puani, mwanadada ndo amekuona siku hiyo hiyo, hata alikua hajui mtu kama wewe upo katika hii dunia, hakujui na unategemea akuambie anakupenda pia, we vipi?, hapo unapoteza nafasi na utaishia kuambiwa usiyoyataka na kuumia moyo tu.

Naamini kabisa mwanaume yeyote mwenye mtazamo sahihi na mwenye hamu ya kujifunza anaweza kuelewa jinsi ya kutongoza mwanamke sehemu yeyote na mahali popote pale, kutongoza hakuitaji kukalili mistari ya kutongozea wala kumpulizia dawa kutoka kwa mganga, kama unania ya kujifunza endelea kusoma nakala za waulizewanaume. Mwanaume mtongozaji hajishushi na anatumia mbinu ya kuonyesha ujasiri wa kimaongezi na akiongea na mwanamke, mwanamke hutambua ya kuwa huyu jamaa ana nia naye kutokana na lugha anayoitumia wakati wa maongezi.

Makosa makubwa mawili ambayo nilikua nafanya wakati wa kutaka kumtongoza msichana, nilikua nasubiri na kusita kwa muda mrefu na kutojua nini cha kuzungumza. "Unakuwa na dakika tatu kutoka unapomuona msichana anayekupendeza na mpaka pale utakapomsogelea na kuanzisha mazungumzo yanayompendeza, ukisubili sana nafasi yako itakupita kama upepo na kupoteza nafasi hiyo muhimu".

Kama ni kwenye sherehe ndipo ulipomuona, piga moyo konde na mwendee na mwambie, "Nimekuona kutoka mbali ila moyo wangu ukang'ang'ania mpaka nije nikusalimie, mambo?" "Siku yako inaendaje?" "Upo upande wa bibi harusi au bwana harusi?" upande wa bibi harusi, ndo maana dada yako amewahi kuolewa! ukoo wenu mzima inavyoonyesha umelaaniwa kwa uzuri!"

Mchokoze kwa maneno matamu, muulize maswali ya kumfanya afurahie maongezi na kama ukiwa unatoa sifa ifiche ndani ya sentensi inayovutia, ukitaka kumjua uliza maswali ambayo majibu yake ni mepesi na rahisi, kama ukitaka kujua anachofanya muulize, "Kwa hiyo familia nzima mwanafunzi amebaki ni wewe tu, maana dada yako tayari ameshaolewa?"

Kwa maswali ya namna hio atajikuta anajiongelea kuhusu yeye na kukufanya akuzoee mapema, na ukiona maongezi yanaelekea ukingoni unatakiwa unakuwa shapu na mbunifu kwa kuanzisha mada nyingine inayovutia zaidi, itakayoleta maongezi matamu zaidi.

Kujua kitu cha kusema wakati wa kutongoza ni ngumu, ila inabidi ujiamini na ufanye kujisahau na kuweka akili kama upo unaongea na dada yako ila maongezi yaweke yawe ya kuvutia zaidi na uyapambe kwa sifa bila kuonyesha nia yako moja kwa moja, mwisho wa maongezi muombe namba ya simu au omba umtoe mtoko akuonyeshe maeneo hayo maana wewe ni mgeni na maongezi yamekupendezea na ungependa kuyaendeleza siku nyingine.

"Ukweli ni kwamba haijalishi utakachokiongea , unaweza ongelea kitu chochote kile ili mradi maneno yawe katika hali nzuri kihisia, onyesha tabia ya kujiamini na mipaka yako." Acha kuwa na wasiwasi na kufikiria nini cha kuongea, we mfate kwanza na maongezi yatajitengeneza yenyewe kwa jinsi ya mazingira mliyopo na weka akilini kitu kimoja, huyo msichana unayeenda kumtongoza inawezekana anatongozwa mara tano au zaidi kwa siku tokea alipokuwa na miaka kumi na nane, kwa hiyo inawezekana ameshatongozwa zaidi ya mara 1000, kwa hiyo usifanye vitu ambavyo ameshavizoea kila siku na kuishia kutoa maamuzi ya kutokubali maombi yako kama wengine waliokataliwa waliotoa maombi yao hapo mwanzo kabla yako, kuwa mbunifu na tumia mazingira yako kwa usahihi na uzuri zaidi.

Hakikisha katika maongezi yako usiongelee wala kugusia vitu vifuatavyo, Usimsifie sana, atakuona kama unambeza. Usijaribu wala kumuuliza kama ana mtu, ana mshikaji wake au anamahusiano na mtu yeyote yule. Usimuulize maswali magumu ambayo yanahitaji uelewa wa kitu fulani.

Vitu vifuatavyo ni ambavyo hutakiwi kuvifanya wakati wa utongozaji, Usiongee kwa sauti ya juu sana, Usijibu kitu au jambo kwa haraka sana, Usiwe unaondoka ondoka au kuhamisha mapozi, usiwe na papara na kuwa mtulivu.

Kitu cha kuweka akilini zaidi usifikilie sana unachokiongelea, ukifikiria sana utakaribisha wasi wasi na kutokujiamini. Wakati wa maongezi yako ya utongozaji, hakikisha unahusisha mambo yafuatayo, Vitu ambavyo anashauku navyo na anavipendelea, Vitu ambavyo unashauku navyo, Hadithi zenye vichekesho na mguso wa mahaba, Jifunze jinsi ya kuhadithia hadithi za kuvutia, Mfanye acheke na kutabasamu kwa kile unachokiona, Michezo ya furaha na ya kuvutia, Unaweza kujikweza kidogo ila usipitilize kilaza Mshauri wa madomo zege Afrika Mashariki.


PIA SOMA MADA HIZI:

1. Zijue mbinu 5 za kumtongoza msichana yeyote mrembo hadi akubali

2. Mbinu 15 za kumtongoza mwanamke akakupenda daima
3. Jinsi ya kumtongoza mwanamke club
4. Jinsi ya kumpata mwanamke bila kumtongoza
5. Mapenzi: Jinsi ya kumtongoza mwanamke unayemtaka na ukampata kwa urahisi
 
Kama ungekuwepo mtaani kwetu kipindi kile tuko 16-18 years old, ungelikua wewe ndo raisi wa maskani yetu. Wengi wetu tulishindwa lakini saivi wasubiri waje.
 
Mkuu Kilaza naomba nikutongoze kwa method hiyo uliyotufundisha,ukikubali ntawaambia watu jinsi tuition zako zilivyo reliable,ukinikataa ina maana hii shule yko haina faida,nianze?
 
Last edited by a moderator:
Mkuu mii nisaidie hv: kumiliki NOAH ya biashara au mgahawa mdogo, upi utakuwa uamuzi sahihi? Mtaji wng ni Tshs 12m!
 
Kilaza sijaona point ya hela,au unatusimulia enzi zenu jinsi ilivyokuwa kabla ya uvumbuzi wa mkwanja!?
 
Wewe unawakalilisha wasiojiamin kufanya vizur katka kuchana verses hawataelewa wape practical
 
wakuu

Heshima mbele. Hii ni special kwa madomo zege

"ulishawahi kujikuta unatamani kuliko
kumtongoza msichana mzuri sehemu flani
japo upate namba yake ya simu ila unajikuta
huna jinsi yeyote au wazo juu ya nini cha
kufanya au kuongea, unatamani kumfata
nguvu miguuni zinakua zimekuishia
unashindwa hata kupiga hatua moja
kumsogelea, lile wazo pekee la kutaka
kumsogelea linakufanya moyo uwende mbio,
mikono iloane na jasho jembamba kukutoka
huku akili yako ikishindwa kufikiria vizuri
nini cha kuweza kuongea iwapo
ukimsogelea?."

unajua nini?, haipaswi kuwa hivi ndo maana
waulizewanaume ipo kwa ajili yako ili
kumaliza maswala madogo madogo kama
haya, kukuondoa katika mazingira ya
kutokua na maamuzi dhabiti na kutokujua
nini cha kufanya ndani ya sekta ya
utongozaji na kukufanya uwe mwanaume
kiongozi na mtanashati kwa kujua ni nini cha
kufanya na mda gani unapaswa kukifanya ili
kuwa mtaalamu katika sekta ya mahusiano.
Kujiamini ni kitu kinachochukua nafasi
kubwa na ndo msingi mkubwa katika
mahusiano na hasa wakati wa utongozaji, na
ndicho kitu mwanamke hutumia kumpima
mwanaume na kumpa nafasi ya uwezekano
wa kuwa na yeye au la, ila mara nyingi mtu
hushindwa kujiamini kutokana na hofu ya
kutokujua ni nini cha kufanya au kuongea
wakati wa utongozaji.

Mwanamme ambaye huwa hafanikiwi kwenye
utongozaji hufanya makosa madogo madogo
kama kumpandisha hadhi mwanamke
anayemtongoza mpaka kiasi ambacho
anaifanya hadhi yake binafsi kuonekana
ndogo na siyo tu anamtongoza mwanamke
kwa wasiwasi na kutojiamini, bali
anamtongoza hovyo hovyo bila mpangilio na
zaidi ya hapo anamuweka wazi mwanamke
kwamba anataka kumjua zaidi ya kawaida
na anajitangaza bila kujijua kwamba,
anahitaji na huyo mwanamke apendezwe
naye hapo hapo.

Nayajua haya kwa sababu kwa muda mrefu
na mimi nilikua hivi hivi, mtaalamu wa
utongozaji huwa anasubira na huwa
hapaparuki hovyo hovyo tu, kutongoza ni
sanaa na inahitaji uelewa mkubwa na hata
mimi iwapo ningelikua ndo huyo mwanamke
sidhani kama ningelikubali hivi hivi, lazima
atake kukujua kwanza ndo mambo mengine
yafuate.

Ukitaka kuishia kusonywa na matusi juu ingia
na mstari wa "dada samahani nimetokea
kukupenda nataka tuwe wote, kila nikikaa
nakuwaza wewe, nikinywa maji nakuona
kwenye glasi", bila kuangalia mazingira na
papara za kusema yaliyo moyoni mwako, huu
mstari lazima utakutokea puani, mwanadada
ndo amekuona siku hiyo hiyo, hata alikua
hajui mtu kama wewe upo katika hii dunia,
hakujui na unategemea akuambie
anakupenda pia, we vipi?, hapo unapoteza
nafasi na utaishia kuambiwa usiyoyataka na
kuumia moyo tu.

Naamini kabisa mwanaume yeyote mwenye
mtazamo sahihi na mwenye hamu ya
kujifunza anaweza kuelewa jinsi ya
kutongoza mwanamke sehemu yeyote na
mahali popote pale, kutongoza hakuitaji
kukalili mistari ya kutongozea wala
kumpulizia dawa kutoka kwa mganga, kama
unania ya kujifunza endelea kusoma nakala
za waulizewanaume.

Mwanaume mtongozaji hajishushi na
anatumia mbinu ya kuonyesha ujasiri wa
kimaongezi na akiongea na mwanamke,
mwanamke hutambua ya kuwa huyu jamaa
ana nia naye kutokana na lugha anayoitumia
wakati wa maongezi.

Makosa makubwa mawili ambayo nilikua
nafanya wakati wa kutaka kumtongoza
msichana, nilikua nasubiri na kusita kwa
muda mrefu na kutojua nini cha
kuzungumza.

"unakuwa na dakika tatu kutoka
unapomuona msichana anayekupendeza na
mpaka pale utakapomsogelea na kuanzisha
mazungumzo yanayompendeza, ukisubili sana
nafasi yako itakupita kama upepo na
kupoteza nafasi hiyo muhimu".

Kama ni kwenye sherehe ndipo ulipomuona,
piga moyo konde na mwendee na mwambie,

>>"nimekuona kutoka mbali ila moyo wangu
ukang'ang'ania mpaka nije nikusalimie,
mambo?"

>>"siku yako inaendaje?"

>>"upo upande wa bibi harusi au bwana
harusi?"

>>"oooh, upande wa bibi harusi, ndo maana
dada yako amewahi kuolewa!, ukoo wenu
mzima inavyoonyesha umelaaniwa kwa
uzuri!"

mchokoze kwa maneno matamu, muulize
maswali ya kumfanya afurahie maongezi na
kama ukiwa unatoa sifa ifiche ndani ya
sentensi inayovutia, ukitaka kumjua uliza
maswali ambayo majibu yake ni mepesi na
rahisi, kama ukitaka kujua anachofanya
muulize,

>>"kwa hiyo familia nzima mwanafunzi
amebaki ni wewe tu, maana dada yako
tayari ameshaolewa?"

kwa maswali ya namna hio atajikuta
anajiongelea kuhusu yeye na kukufanya
akuzoee mapema, na ukiona maongezi
yanaelekea ukingoni unatakiwa unakuwa
shapu na mbunifu kwa kuanzisha mada
nyingine inayovutia zaidi, itakayoleta
maongezi matamu zaidi.

Kujua kitu cha kusema wakati wa kutongoza
ni ngumu, ila inabidi ujiamini na ufanye
kujisahau na kuweka akili kama upo
unaongea na dada yako ila maongezi yaweke
yawe ya kuvutia zaidi na uyapambe kwa sifa
bila kuonyesha nia yako moja kwa moja,

mwisho wa maongezi muombe namba ya simu
au omba umtoe mtoko akuonyeshe maeneo
hayo maana wewe ni mgeni na maongezi
yamekupendezea na ungependa
kuyaendeleza siku nyingine.

"ukweli ni kwamba haijalishi utakachokiongea
, unaweza ongelea kitu chochote kile ili mradi
maneno yawe katika hali nzuri kihisia,
onyesha tabia ya kujiamini na mipaka
yako."

acha kuwa na wasiwasi na kufikiria nini cha
kuongea, we mfate kwanza na maongezi
yatajitengeneza yenyewe kwa jinsi ya
mazingira mliyopo na weka akilini kitu
kimoja, huyo msichana unayeenda
kumtongoza inawezekana anatongozwa mara
tano au zaidi kwa siku tokea alipokuwa na
miaka kumi na nane, kwa hiyo inawezekana
ameshatongozwa zaidi ya mara 1000, kwa
hiyo usifanye vitu ambavyo ameshavizoea kila
siku na kuishia kutoa maamuzi ya kutokubali
maombi yako kama wengine waliokataliwa
waliotoa maombi yao hapo mwanzo kabla
yako, kuwa mbunifu na tumia mazingira yako
kwa usahihi na uzuri zaidi.

Hakikisha katika maongezi yako usiongelee
wala kugusia vitu vifuatavyo,
usimsifie sana, atakuona kama unambeza.
Usijaribu wala kumuuliza kama ana mtu, ana
mshikaji wake au anamahusiano na mtu
yeyote yule.

Usimuulize maswali magumu ambayo
yanahitaji uelewa wa kitu fulani.
Vitu vifuatavyo ni ambavyo hutakiwi
kuvifanya wakati wa utongozaji,
usiongee kwa sauti ya juu sana,
usijibu kitu au jambo kwa haraka sana,
usiwe unaondoka ondoka au kuhamisha
mapozi, usiwe na papara na kuwa mtulivu.
Kitu cha kuweka akilini zaidi usifikilie sana
unachokiongelea, ukifikiria sana utakaribisha
wasi wasi na kutokujiamini.

Wakati wa maongezi yako ya utongozaji,
hakikisha unahusisha mambo yafuatayo,
vitu ambavyo anashauku navyo na
anavipendelea,

vitu ambavyo unashauku navyo,
hadithi zenye vichekesho na mguso wa
mahaba,

jifunze jinsi ya kuhadithia hadithi za
kuvutia,

mfanye acheke na kutabasamu kwa kile
unachokiona,

michezo ya furaha na ya kuvutia,
unaweza kujikweza kidogo ila usipitilize

kilaza
mshauri wa madomo zege afrika mashariki


akikisha kama niusiku msiwe gizani,, nilishaona lodgeyq uncle mwanamke yukogetini anapiga simu jamaa akagoma kupokea akidai siohuyu,,wanamwambiq kata,kakata binti anapiga tena jamaa akqtumamtu qp amwambie aende ajafika,,,so kwenye mwanga nimuhimu usijetayaruki ukamkataa ndiohuyu kweli hukiu savannahzako zikiwa choonitayari sijakuulizq ngapi ulimopa
 
Mi nilishasahau kutongoza siku hizi. Huwa najichukulia tu. Mbona huhitaji hayo yote.
kikubwa pesa bhana.
 
kilaza sijaona point ya hela,au unatusimulia enzi zenu jinsi ilivyokuwa kabla ya uvumbuzi wa mkwanja!?

Mkuu wanao tumia pesa kutongoza 99% ni madomo zege lakini kama una sound kali unajilia mtoto kiulaini
 
Mkuu mii nisaidie hv: kumiliki NOAH ya biashara au mgahawa mdogo, upi utakuwa uamuzi sahihi? Mtaji wng ni Tshs 12m!

12 m zinatosha kufungua mgahawa tena sio mdogo ni mkubwa tu lakini uangalie na sehemu ya kuuweka
 
12 m zinatosha kufungua mgahawa tena sio mdogo ni mkubwa tu lakini uangalie na sehemu ya kuuweka

Hapa nilipo ni jirani na stend na muda mwingi kuna msongamano wa watu! Hasa hasa kuanzia saa 2 asubuhi mpk 1 usiku!
 
ngoja nianzie kwa mdada humu humu
 
Back
Top Bottom