Ngoja nikusaidie mkuu japo sio rasmi ila endapo utashindwa kabisa ku unlock.
N.B... Njia hii itakufanya kufuta na kupoteza vitu vyote ulivyokuwa navyo katika simu ni kama ku flash ila hii unafanya mwenyewe na haina gharama.
1.zima simu yako
2.switch on
3.wakati inawaka hakikisha umeshika batani hizi ya kuwasha, kuongeza na kupunguza sauti kwa mara moja.
4.tafuta neno (factor reset)
Hapo utatumia button ya sauti kushusha kisha utatumia button ya kuzima kama "ok".
Hapo utakuwa umereset simu yako na utapoteza kila kitu katika simu... Ikiwa nimekosea unaweza nirekebisha maana si mtaalamu sana.