Namna ya kuondoa madoa kwenye sink ya Ceramic

Namna ya kuondoa madoa kwenye sink ya Ceramic

mwana ally

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2014
Posts
363
Reaction score
119
Wana JF naomba msaada. Napenda sana kuona masink ya bafuni nk yakiwa katika weupe wake kama awali. Tatizo ni kuwa najitahidi sana kununua vifaa vya kuondoa madoa,mfano Vim, harpic nk, na kila baada ya siku mbili au tatu lazima niwajibike mimi mwenyewe kusafisha lakini haiwi kama awali. Kama yupo anayejua namna nzuri ya kuyaweka masink katika mng'aro mzuri
 
Hapo ndipo utakapoona ubora wa bidhaa,sink au tiles ya spain au brand nyingine iliyo na quality nzuri uwa ni rahisi sana kuisafisha na kurudi kwenye mng'ao wake wa mwanzo..Sijui Sink zako ni za wapi lakini jaribu clorox uwa ni nzuri sana kwa kuondoa madoa kwenye Sink.
 
Acha uvivu vifaa vya kusafisha ushavitaja vitumie vizuri litang'aa tu mkuu
 
mbona harpic nzuri?ile ya rangi ya blue,kama sinki lina alama ambayo ukisugua na sabuni haitoki,ukinyunyuzi harpic halafu acha kwa muda wa robo saa,safisha,sinki linakuwa safi kabisa.hata bleach inasaidia,pembeni mwa mabafu sometimes kunafanya weusi,ukinyunyuzia bleach ambayo ipo strong{kuna bleach nyengine strong nyengine nyepesi }uiache baada ya muda,inasaidia.au bafu jaza maji ya moto ndani ya bafu,mwagia ndani bleach,iache kwa muda halafu osha bafu linakuwa safi
 
Hapo ndipo utakapoona ubora wa bidhaa,sink au tiles ya spain au brand nyingine iliyo na quality nzuri uwa ni rahisi sana kuisafisha na kurudi kwenye mng'ao wake wa mwanzo..Sijui Sink zako ni za wapi lakini jaribu clorox uwa ni nzuri sana kwa kuondoa madoa kwenye Sink.

Kiukweli sijui brand ni ya wapi mkuu... ( hilo nalo yaweza kuwa tatizo) nashukuru kwa ushauri ngoja nisake hizo bidhaa za usafi ntawajuza matokeo.
 
A brother of mine alitumia indegenous knoweldge kijijini....yeye alitumia maji ya battery...alinisuprise but it was wonderful and marvelous.

you can chose to pick that as well.
 
A brother of mine alitumia indegenous knoweldge kijijini....yeye alitumia maji ya battery...alinisuprise but it was wonderful and marvelous.

you can chose to pick that as well.

Ni kweli maji makari ya betry tena ukianza kumwaga Jivu kisha ukamwagia maji ya betry choo au sink litang'aa zaidi ya jipya. Tahadhari uvae kikinga pua maana itatokea reaction inayoweza kukuafect upumuaji wako. Pia unga wa soda au mnaita baking powder pia husaidia.
 
Asante Likwanda. Je baking powder naitumiaje.
 
Back
Top Bottom