Udochi
JF-Expert Member
- Jul 25, 2015
- 782
- 1,056
Habari zenu wakuu,
Natumai baadhi ni wazima kiafya,
tumshukuru Muumba kwa kutuamsha salama na kuwaombea dua wanaoumwa wapone.
Mada:
Kwa hali ilivyokuwa kwa sasa,
Wilaya ya BAGAMOYO Ndio sehemu inayosifika sana kwa utapeli mkubwa wa viwanja,
Na inasemekana ni wengi sana wametapeliwa ama kwa kuuziwa kiwanja zaidi ya mara 1 au kuuziwa kiwanja kilichokwishauzwa kwa mtu mwingine hapo Kabla,
Au kwa namna yoyote ile wanayoweza kuitumia.
Na hii hufanyiwa sana wageni.
Pamoja na ushahidi wa serikali za mitaa,
Na Wakati mwingine hata mahakamani,
Kuibiwa/kutapeliwa kunakuwepo tu.
Waweza kutana na dalali feki,
Mmiliki feki,
Mwenyekiti/mtendaji feki,
Pia nyaraka FEKI
Na hivyo kupelekea mahakama kupitisha mauziano kwa kuwaamini
Kumbe ni matapeli.
Hayo ndio niliyopata kuyasikia kuhusu ardhi katika mji huu.
::
Kwa mazingira hayo wakuu,
Mimi ni miongoni mwa wenye dhamira ya kupata kipande cha ardhi ili nijenge kibanda cha makazi Katika huu mji (na si mwenyeji).
Sasa
kwa Jinsi utapeli ulivyshamiri,
Ningeomba wakuu mnisaidie Namna ya kununua kiwanja bila kutapeliwa Kabisa,
Maana'ke kwa siye wenye vipato vya chini kupoteza elfu 50 tu ni pigo Kubwa,
Sasa kutapeliwa milioni 2 au 3 ambazo tumezitafuta kwa jasho kwa miaka
twaweza poteza fahamu kwa siku kadhaa.
Michango yenu ni muhimu sana.
Nawasilisha wakuu.