Namna ya kumpiga kibuti mume mkorofi! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namna ya kumpiga kibuti mume mkorofi!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Mtambuzi, Sep 7, 2011.

 1. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #1
  Sep 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,674
  Likes Received: 907
  Trophy Points: 280
  Sio lengo langu kuwafundisha wanawake namna yakuachana na wapenzi au waume zao. Lakini hebu fikiria kwamba kila wakati wanandoa au wapenzi wako kwenye vita. Hakuna amani, hakuna masikilizano. Kutwa nzima mtu anawaza kuhusu uhusiano wake mbaya hadi anashindwa hata kufanya kazi. Je, hali kama hii ina maana kwa mtu kuendelea kuwa kwenye ndoa?

  Hapa nazungumzia wale ambao wanashindwa kutoka kwenye uhusiano, ambao wanajua kabisa kwamba, unawatesa na kuwaumiza. Kuna sababu nyingi kwa nini watu hawa wanashindwa, lakini nyingine zinatokana tu na kutojua namna ya kutoka, sio utegemezi wa aina yoyote.Moja ya sababu, ambazo ninaziona sana hasa kwa wanawake ni kujali jamii itasemaje.

  Mtu anaona kabisa uhusiano haufai na anatamani kutoka . lakini anajiuliza, hivi watasemaje? Kuna wakati ndugu wanamwambia, yeye ndiye mkorofi. Kama hii ndio sababu anachotakiwa kufanya mwanandoa ni kuhakikisha kwamba anajifunza kuishi kama yeye. Nijuavyo mimi, hata wanandugu au jamii hata ikisema vipi, anayeumia au kuepuka kuumia au kuuawa ni yule aliye kwenye mateso ya ndoa.
  Jambo la kujiliza hapa ni kama, jamii ndiyo inayopigwa, kutukanwa, kutelekezwa au kudhalilishwa?

  Lakini jambo kubwa zaidi la kufahamu ni kwamba mtu alishaolewa maana yake ni mtu mzima mwenye haki ya kuamua juu ya maisha yake. Akisbiri ndugu wamwamulie, basi huyo bado ni mtoto..
  Jambo lingine ni lile la, je nikimwacha nitapata mwingine? kwani wanaume siku hizi ni shida sana? Ni ujinga unaowafanya wengi kuuliza swali hilo. Unahitaji mwingine wa nini? Unahitaji mwingine ili maisha yako yawe ya maana zaidi au? Kama hakuna mwingine ni vyema kwa sababu maana yake ni kwamba hakuna mwingine wa kukutesa.

  Lakini wanasaikolojia wanaamini kwamba, ‘kila bidhaa ina mnunuzi.’ Kama unataka mwingine, hata ukiwa na miaka sitini utampata. Huwezi kumpata wakati ukiwa ndani ya tanuru la mateso. Ni lazima utoke kwanza.
  Kuna wale wanaoshindwa kutoka kwa sababu wanaamini kwamba mwanamke haruhusiwi kutoa talaka. Hi siyo kweli. Kuna wanaoshindwa kutoka kwa sababu dini zao zinakataza kuachana, hii pia siyo kweli.

  Mwanamke au mwanaume, yeyote anaweza kuomba talaka na ikatolewa, kama kuna sababu zenye kukidhi haja hiyo. Chombo pekee kinachoweza kutoa talaka au kuidhinisha wanandoa kuachana ni Mahakama, siyo dini au taasisi nyingine. Kinachoitwa ‘talaka tatu’ kwa mfano, ni ushahidi tu, na sio talaka.
  Itaendelea……………..
   
 2. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #2
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,248
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  Hii post sina hata haja ya kusave kama ninavo fanya zako zoote....lol... Maana hata wazo hamna...
   
 3. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #3
  Sep 7, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 36,992
  Likes Received: 18,369
  Trophy Points: 280
  kila bidhaaa ina mnunuzi........
   
 4. s

  shalis JF-Expert Member

  #4
  Sep 7, 2011
  Joined: Jun 30, 2011
  Messages: 272
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ni vyema unaelimisha jamii na kuwapa nari mpya ale wenye mahusiano yanayo sua sua....hasa akina mama
  i like keep it up
   
 5. BlackBerry

  BlackBerry JF-Expert Member

  #5
  Sep 7, 2011
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 1,844
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  thanks mkuu
   
 6. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #6
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 8,907
  Likes Received: 3,567
  Trophy Points: 280
  Umesahau wengine nikiondoka wototo je itakuaje?Ukweli ni kwamba hakuna ndoa yenye haleluya kila siku,ndo maana kuna neno UVUMILIVU.Mimi nitabanana humuhumu kwenye ndoa.KUACHANA SIYO SOLUTION KWANGU.
   
 7. Power G

  Power G JF-Expert Member

  #7
  Sep 7, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 3,878
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mai waifu baada ya kusoma hii thread yako naona anaanza kuwa na kakiburi kidogo. Usipoangalia utasababisha talaka nyingi sana. Hasa ukiwadanganya kwamba "kila bidhaa ina mnunuzi......".
   
 8. Mtambuzi

  Mtambuzi Platinum Member

  #8
  Sep 7, 2011
  Joined: Oct 29, 2008
  Messages: 8,674
  Likes Received: 907
  Trophy Points: 280
  Uko sahihi, lakini sio kwamba nimesahau, kama umesoma mpaka mwisho, naamini umeona hapo nilipoandika "ITAENDELEA....." kwa hiyo majibu yako yapo katika sehemu ya pili ya makala hii.
  Lakini sababu ziko nyingi na nyingine huwezi hata kuzifikiria kwa sababu tunatofautiana sana katika kufikiri. kuna binti mmoja alikuwa haishi kulalamikia mateso ya mumewe, alikuwa analalamika sana, na nilipomuuliza kwa nini haachani na huyo mwanaume.......... jibu lake lilikuwa ni kwamba......... anaogopa akiachika heshima yake itashuka na kwa kuwa yeye ni mmoja wa viongozi katika vikundi vya akina mama anadhani wenzake watakosa imani na yeye kwa sababu wanamtumia kama mshauri........Ebo! Ajabu kabisa.........
   
 9. k

  kisukari JF-Expert Member

  #9
  Sep 7, 2011
  Joined: Jul 16, 2010
  Messages: 3,478
  Likes Received: 708
  Trophy Points: 280
  maneno yako yana ukweli ndani yake,ingawa in reality neno kuachwa ni kama taboo,kwa baadhi ya watu{sio wote}ndio maana wengi wao wanaona bora waendelee kuteseka kuliko neno la kuachana.
   
 10. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #10
  Sep 7, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,841
  Likes Received: 2,069
  Trophy Points: 280
  mnnnnh......................hii aihuuuuuuuuuuuu
   
 11. Masikini_Jeuri

  Masikini_Jeuri JF-Expert Member

  #11
  Feb 13, 2012
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 6,816
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Lazia kushinda hii vita kwa gharama yoyote ile!
   
Loading...