Namna ya kumiliki Brand

seifutz

Member
Jul 18, 2021
34
113
Kama unataka kuanzisha biashara, au umekwisha anzisha, basi hii mada inakuhusu. Na hata unataka kuajiriwa au unatafuta kazi bora zaidi uliyonayo, ni jambo la msingi kujua namna ya kuwa na Brand inayouzika.

Maana ya Brand

Branding ni namna ya kutengeneza HISIA chanya mbele za hadhira. Ni namna unavyotaka wafikirie na waitambue bidhaa husika au asasi.

Kuna mengi ya kufanya ili kujenga hisia hizo- jinsi unavyowasiliana na hadhira , huduma kwa wateja, aina ya bidhaa zako, uwajibikaji wako kiutendaji n.k

Hii sio maana ya Brand

Brand sio rangi , sio logo, sio jina la bidhaa. , bali ni vitu kama hivyo vina leta hisia na vinasadia kufanikisha lengo la uwepo wa bidhaa/asasi au mtu husika.

Kwanini unahitaji kuwa na Brand

Kama tulivyoona katika maana ya Brand, lengo kuu la Brand ni kufanikisha kukubaliwa mbele ya wale unaowalenga, hivyo basi unahitaji Brand ili kujiwezesha kupata kazi bora unayoihitaji kwani kwa picha nzuri utakayoijenga kwa jamii , unaweza kupata watu watakaotaka kufanya nawe kazi.

Pia Brand inakusaidia pale unapotaka kuanzisha biashara , au kama tayari unayo biashara basi inakurahisishia kuuza bidhaa zako nyingine mpya.

Brand inakufanya ujenge mtandao na watu wa muhimu katika fani yako, ajira na biashara.

Je, unatengenezaje Brand yako ?

Kwanza kabisa inabidi ujijue unapenda kufanya nini na nini utakachotoa kwa jamii kama bidhaa. Mfano kama lengo lako ni kutoa huduma za michezo mfano mpira wa miguu, basi utajikita katika kujifunza kwa undani kuhusu mambo ya mpira wa miguu, kushiriki katika michezo na kushare habari za kina kuhusu mpira wa miguu.

Hata hivyo haitoshi tuu kuonekana upo fiti katika hiyo bidhaa yako , bali pia uwafanye watu wengine wapende kuwa karibu nawe. Hapa ndipo kazi ya ziada inahitajika katika namna yako ya kufanya mawasiliano.

Kumbuka mawasiliano ni zaidi ya unachozungumza, hata namna ya mavazi yako, lugha yako, umakini wako, tafakari zako, jinsi ulivyo na msaada, mtandao wako n.k vyote vitakusaidia kujitengeneza kama BRAND.

Jitokeze ufahamike

Kujifunza na kuwa na kitu cha maana cha kutoa kwa jamii hakutoshi kama haujafahamika na kuanza kujenga Brand. Tafuta nafasi ya kuzungumza na makundi ya watu unaowalenga.

Tumia mitandao ya kijamii kwa faida ili kuifanya jamii ikutambue kwa namna unavyolenga kuja kutoa bidhaa yako.

Hitimisho

Fikiria na amua leo, je wewe unataka kutambulika kama mtu wa namna gani? Anza kujijenga kama BRAND !

Kumbuka tunatengeneza BRANDS ili kunufaika hususani kifedha na kimaendeleo. Haijalishi muda gani utachukua kabla ya kuweka BRAND imara, ila kumbuka INALIPA kufanya hivyo.
 
Back
Top Bottom