Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,720
- 215,792
Dada yangu yupo kwenye ndoa kwa zaidi ya miaka 20, yeye ni mama wa nyumbani, ana miradi yake ya kufuga kuku na kupika kukiwa na shughuli. Nilimtembelea tilikuta taratibu zake za nyumba, akiamka asubuhi anafanya shughuli zake pamoja na kutengeneza chai ya baba, yeye baba wanapata chai pamoja.
Baada ya hapo hali kitu kingine chochote, mpaka baba arudi kutoka kazini, yeye na dada wa kazi watafanya shughuli zote za ndani na kupikia watoto, watoto wakisha kula ataandaa chakula cha kwake na mzee anamsubiri.
Mzee akitoka kazini inabidi awahi nyumbani akichelewa anajua kunamtu hajakula anamsubiri yeye. Baada ya kula obviously anakuwa amechoka kutoka tena inakuwa ngumu. In a way niliona ile ilikuwa njia nzuri ya kudhibit. Walio kwenye ndoa watujuze zaidi.