Namna ya kumchunguza mchumba wa kuoana naye

Kigodoro

JF-Expert Member
Apr 25, 2014
1,660
1,679
Kumekuwa na msisitizo mkubwa kwa vijana kuwa wachunguzane kabla ya kuoana. Lkn vijana wengi hawajui namna ya kuchunguzana. Wanadhani kuchunguzana ni kutoana out na kwenda kula bata. Mwisho wa siku wanaoana wakiwa hawajuani kitabia vizuri. Maana ktk hatua ya uchumba wengi huficha uovu wao.

Mm naleta mbinu za kuchunguzana zitakazowasaidia vijana kuchunguzana. Haijalishi wewe ni mwanadada ama mkaka, mbinu hizi ndiyo tiba ya fake love.

1. Anzisha varangati lisilokuwa na kichwa wala miguu ili uone mwenzi wako ana react vipi ktk mavarangati ama migogoro. Maana ndoa ni pishi la migogoro hivyo lazima umjue mwenzi wako akikasirika ana kaubinadamu kidogo ama hugeuka mnyama wa mwituni? Yuko tayari kukuua akichukia.

2. Mpige stop kufanya au kupenda jambo fulani ghafla bini vuu. Hii itakusaidia kujua kama mwenzi wako anatii maonyo? Kwa wepesi kiasi gani? Ama mpk ashikwe akili na marafiki au mashosti? Hafai huyu atavujisha siri za ndoa mkioana.

3. Tengeza tatizo kisha umsimulie kwa hisia ukionyesha ni jinsi gani tatizo hilo limekuumiza. Halafu usiombe msaada wowote toka kwake. Muache afikirie mwenyewe. Hii itatoa picha ni namna gani anajali.

4. Tumia nqmba ngeni kumtokea ukijifanya ni jinsia tofauti na yeye. Halafu sema simu yako ina mic mbovu ili mtumie sms zaidi kuwasiliana. Tafadhali tumia laini ya rafiki yako mwingine siyo yako. Utaje maeneo ambayo yeye hupendelea kutembelea kuwa ndiko ulimuona na ukatafuta namba yake na kiukweli umemzimikia. Ukiona anachangamkia gemu hili ujue huyu gumegume. Kimbia sana.

Huko ndiyo kuchunguzana siyo kuchekacheka kama mazuzu tu. Halafu tunawachangia siku 2 mnaachana.
 
Khee hujaeleweka mkuu kichwa cha uzi na maudhui haviendani tulitegemea utakua umeorodhesha hizo namna
 
Mkuu nadhan

Mkuu nadhani kiandikio changu kina virusi. Nimejikunja nikaandika weee nakuja kuposti nashangaa vitu vya ajabu kqma hivyo. Sasa niko hoi
 
Duu baasi tafuta namna nyingine tupate elimu cZ mada yako inavutia kutaka kujua yaliyomo
 
Mkuu nadhan

Mkuu nadhani kiandikio changu kina virusi. Nimejikunja nikaandika weee nakuja kuposti nashangaa vitu vya ajabu kqma hivyo. Sasa niko hoi
Umesomeka.

Ila, Nimeamini kuwa kumbe, KUSOMA na KUELEWA ni vitu viwili tofauti..
 
#Salut, i have been doing this almost all the time. Sio wengi they pass with flying colors exam kama hii.

Very few strong women around these days. Kama kuanzisha tatizo/argument na kuona kama she will be smart enough to find a solution to it, very few of women of this kind wapo. Atakimbilia towards one option and that's breaking up/having a break.

World is has more imbeciles than real women these days.
 
Bora ukajua ni chizi mapema na ukamuepuka kuliko kuamua kuishi na chizi ukaja kugundua ikiwa too late
 
Sawa !! Ila nadhani ni kupoteza mda. Wanawake wa sasahiv wana akili kweli na wanajua sana ku fake love. Mtu anaekupenda utamjua tu tangu mwanzo na wala haina haja kutafuta upendo kwenye mambinu yote hayo.
 
Utamjuaje sasa au ishara gani zinaonyesha hapretend?
 
Kumekuwa na msisitizo mkubwa kwa vijana kuwa wachunguzane kabla ya kuoana. Lkn vijana wengi hawajui namna ya kuchunguzana. Wanadhani kuchunguzana ni kutoana out na kwenda kula bata. Mwisho wa siku wanaoana wakiwa hawajuani kitabia vizuri. Maana ktk hatua ya uchumba wengi huficha uovu wao.

Mm naleta mbinu za kuchunguzana zitakazowasaidia vijana kuchunguzana.

1. Anzisha varangati lisilokuwa na kichwa wala miguu ili uone mwenzi wako ana react vipi ktk mavarangati ama migogoro. Maana ndoa ni pishi la migogoro hivyo lazima umjue mwenzi wako akikasirika ana kaubinadamu kidogo ama hugeuka mnyama wa mwituni? Yuko tayari kukuua akichukia.

2. Mpige stop kufanya au kupenda jambo fulani ghafla bini vuu. Hii itakusaidia kujua kama mwenzi wako anatii maonyo? Kwa wepesi kiasi gani? Ama mpk ashikwe akili na marafiki au mashosti? Hafai huyu atavujisha siri za ndoa mkioana.

3. Tengeza tatizo kisha umsimulie kwa hisia ukionyesha ni jinsi gani tatizo hilo limekuumiza. Halafu usiombe msaada wowote toka kwake. Muache afikirie mwenyewe. Hii itatoa picha ni namna gani anajali.

4. Tumia nqmba ngeni kumtokea ukijifanya ni jinsia tofauti na yeye. Halafu sema simu yako ina mic mbovu ili mtumie sms zaidi kuwasiliana. Tafadhali tumia laini ya rafiki yako mwingine siyo yako. Utaje maeneo ambayo yeye hupendelea kutembelea kuwa ndiko ulimuona na ukatafuta namba yake na kiukweli umemzimikia. Ukiona anachangamkia gemu hili ujue huyu gumegume. Kimbia sana.

Huko ndiyo kuchunguzana siyo kuchekacheka kama mazuzu tu. Halafu tunawachangia siku 2 mnaachana.

Mkuu mistari ni michache lakini imemaanisha yaani maneno ni mazima. nina uhakika itagusa wengi!! Mimi pia yamo yanaendana khasa na mchuchu angu kiasi some time nawaza kuachana nae.....
kama umenishtua flani....
yaani umegonga nipo...
mingine inapretend love, sad a ngoja muoane ulione lilivyo na rangi mingi!!
 
we pumzika achana na hizo fikra za kitoto ndoa haina fomula mkuu
kabla ujamuangalia mwanamkee jiangalie ww kwanza
ndoa nying wanaume wamekua chanzo cha migogoro bila kujia c
coz wanawake wanahifadh makosa kupita maelezo af wanalipa kisas kimya kimya
 
Hizo njia zako zote lazima ufeli kwenye hayo mahusiano....lazima ufeli. Khaaaaa,while all the trouble. Yaani nijitie asha ngedere for wat??Ndo hapo nijitie Asha Ngedere mara mwenzangu made John Cena....hapana kwakweli..m
 
#Salut, i have been doing this almost all the time. Sio wengi they pass with flying colors exam kama hii.

Very few strong women around these days. Kama kuanzisha tatizo/argument na kuona kama she will be smart enough to find a solution to it, very few of women of this kind wapo. Atakimbilia towards one option and that's breaking up/having a break.

World is has more imbeciles than real women these days.
Hiri rijamaa rimeandika madude gani haya?!
Hata hayasomeki!
 
Usicheze na akili ya mwanamke unaweza ukampa mtihani kuliko huo na akafaulu na mwengine pia lakini mwenye lake
hawachi,muombe mwenyezi mungu akupe mwenye kheir na wewe ,uchunguzi waachie Police...
 
Umeongea pointi sana dada!
Kama vipi ni pm nikutumie japo laki tatu ya kusuka!
 
we pumzika achana na hizo fikra za kitoto ndoa haina fomula mkuu
kabla ujamuangalia mwanamkee jiangalie ww kwanza
ndoa nying wanaume wamekua chanzo cha migogoro bila kujia c
coz wanawake wanahifadh makosa kupita maelezo af wanalipa kisas kimya kimya
Mkuu ushauri huu ni kwa wanaume na wanawake. Soma tena
 
Back
Top Bottom