Namna ya kujenga uwezo wako wa concentration

Namna ya kujenga uwezo wako wa concentration

Bujibuji Simba Nyamaume

Platinum Member
Joined
Feb 4, 2009
Posts
78,948
Reaction score
168,411
Charles Cosmas
NAMNA YA KUJENGA UWEZO WAKO WA CONCENTRATION.

Sehemu ya Kwanza
Kwanza concentration ni nini ?
Ni uwezo wa kuweka fikra au mawazo yako mahali pamoja au kwenye jambo moja kwa muda fulani.

Kwenye dictionary ya kingereza wametafsiri :
Definition of concentration : the ability to give your attention or thought to a single object or activity :

the ability to concentrate. : the act of giving your attention to a single object or activity.
Huu ni uwezo wa kuweka fikra zako au mawazo yako kwenye jambo fulani moja mpaka umelifanikisha.

Vijana na jamii kubwa ya wanafunzi na watu wazima wengi hawana uwezo huu, hata mimi nilikuwa kwa sehemu sina uwezo huu, ndio maana leo watu hawawezi kukaa hata ibadani masaa matatu wakisikiliza neno au darasani, mwanafunzi hawezi kukaa mahali pamoja kuanzia saa mbili asubuhi mpaka saa nne kabla ya break unakuta ameshakaa kwenye madawati kama nane hivi.

Hili ni tatizo kubwa na matokeo yake ni kwamba watu wengi hawawezi kupanga kitu na kukisimamia mpaka mwisho.

Mfano ni vijana wachache sana ukiwapa kitabu chenye kurasa 200 wanaweza kukisoma mpaka mwisho, hawawezi kufocus kwenye jambo moja kwa muda mrefu kwa sababu wakosa uwezo concentration katika jambo fulani.

Ni nadra sana kumkuta kijana akisoma novel siku hizi au ukiamua kutafuta vijana walioisoma biblia yote ni nadra sana kuwapata siku hizi, hata series zenyewe wanazongalia wengine hawezi umaliza hata epsode wanakimbilia kufoward mbele wakiangalia vipande vipande hawawezi kutuliza fikra zao kwenye jambo moja mpaka liishe.

Nilijigundua kuwa sina tabia hii na hivyo ilinichukua muda kuanza kujijengea tabia hii. Niligundua nikiwa mwanafunzi kuwa siwezi kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu yaani siwezi kumaliza masaa mawili kwenye benchi moja bila kuhama hama.

Matokeo yake kila siku nilikuwa wa kwanza kumaliza mtihani na matokeo yakitoka nashika mkia. Miongoni mwa mambo ambayo niliamua kujifunza ni pamoja na kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu, namshukuru Mungu mpaka namaliza kidato cha sita nilikuwa naweza kukaa mahali pamoja kwa muda mrefu mpaka masaa nane au hata tisa, unaenda unarudi unanikuta nimekaa palepale nafanya kitu kilekile.

Leo hii ni kazi ngumu kwa kijana kusoma gazeti lote na kulimaliza wanadai wana mambo mengi, hata kusoma vitabu shuleni ni tatizo vijana na wanafunzi wako tayari kusoma summary na sio kitabu kwa sababu uwezo wao wa kuweka fikra mahali pamoja kwa miezi miwili au mitatu hawawezi.

Mfano hebu anglia vijana au watu wengi wenye diary za kuweka kumbukumbu za matukio wengi wao wanazinunua january lakini february hawajui ziko wapi kama anayo ujue ameruka miezi kama saba hivi bila kuandika kitu.

Hili ni tatizo kubwa na ndio maana huku kwetu waandishi ni wachache sana, kwa sababu kuandika kunahitaji concentration ya hali ya juu.

Ugunduzi na uwezo wa kuona vitu kwa tofauti unahitaji concentration na muda wa kuweza kuweka fikra zako au mawazo yako kwenye jambo fulani.

Je ulishasema leo siku nzima ntakaa mezani nafikiria jinsi ya kuapata mtaji ? Siku nzima.
Tabia hii ilinichukua muda kuijenga ila nilipoigundua na kuizoea imekuwa chachu kubwa kwenye maisha yangu na mafanikio yangu.

Kwanin watu wengi hawawezi kuconcentrate ?

Majibu ni mengi ila naweza kusema kubwa ni malezi yetu tiliolelewa na makuzi tuliokulia. Vijana wengi tumekulia kwenye maisha ya mahangaiko kuzunguka na hali ya kukosa utulivu hasa wa akili tofauti na watoto wa siku hizi ambao wengi wao hukaa ndani mbali na hapo ni mazoea tu,

Sisi tumezoea kuwa na mahangaiko mengi yasiyo na tija hivyo imekuwa sehemu yetu. Technologia pia imekuwa sababu kubwa ya wengi kupoteza uwezo huu inasemekana kuwa ujio wa smartphone umepelekea watu wengi kupoteza uwezo wao wa kufocus kwenye jambo moja, leo hii mtu kila baada ya dakika mbili anaangalia amepata like ngapi au comment ngapi nk.... Kiasi kwamba kufocus kwenye maswala ya msingi imekuwa tatizo kubwa.

Nini madhara ya kukosa concentration ?
Je nawezaje kujenga concentration yangu ?
Nakaribisha maswali mbali mbali.

Tukutane Jumatano 27.09.2017 kwenye mwendelezo wa somo hili.
Na
Mshindi Mwenzako
Charles Cosmas mtaalam wa Merchandised Power Tongs TRS
 
Tukutane 27.09.2017

Hapa kweli tunahitaji concentration bila hivyo utatuuza mchana kweupe!
 
Sijaimaliza kuisoma maana naona inawalenga wanafunzi nikaachanayo
 
2hrs ago ,halafu tukutane 27/9/2017 kwani miaka inarudi nyuma
 
Back
Top Bottom