Namna ya kuishi na ndugu wa mume

Molembe

JF-Expert Member
Dec 25, 2012
9,898
11,745
Ndoa nyingine zinaingia kwenye migogoro kutokana na kuingiliwa na ndugu wa mme pamoja na gubu za wanawake wa siku hizi, pamoja kwamba hawa wanawake wa siku hizi hawana uvumilivu na ni wakorofi haswa, lakini wakati mwingine ndugu wanaweza kuwa tatizo kwenye mahusiano yako wewe mwenza wako.

Wanaume wengi tumekuwa tukilichukulia hili suala kijuu juu lakini inawaumiza wenza wetu, jambo la kufanya kama mwanaume ijue tabia ya mkeo, na ndugu zako, kuna wanawake wanaficha makucha lakini hakikisha unaigundua, ili linapotokea tatizo iwe ni rahisi kufanya uchunguzi wako na kugundua nani mkorofi na ni nani ana matatizo.

Ishi mbali na ndugu zako kama mama unaweza kumjengea nyumba mbali na unapoishi ukawa unatuma mahitaji yote huko,utashangaa urafiki utakaokuwepo kati ya mkeo na mamako, hata akitaka kuja kukusalimia asikae muda mrefu sana mpaka kujenga mazoea.

Wakanye ndugu wengine wasiingie ndoa yako, kama kuna anachombeza vimaneno mpe onyo kali ambalo linamfanya aongoze, kitendo cha kuruhusu kuwasikiliza ndugu hupelekea kuletewa maneno ambayo huleta misukosuko kwenye ndoa.

Vilevile hata kama mke analeta maneno naye aonywe.Usiruhusu dada zako kuzoea kwako kama wameolewa wakae kwao watulie na familia zao hizi habari za kuja kuishi kwako mara kwa mara zinaweza sababisha migogoro kati yao na mke.

Kwa upande wa wanawake,mchukulie mama mkwe kama mzazi wako chochote atakachokutamkia kichukulie kawaida, lakini kabla ya kuolewa tambua kuna karaha kama hizo za ndugu wa mme na jua jinsi ya kukabiliana nazo.
 
Mke awe mke atimize wajibu wake na awe na upendo.... kuna baadhi ya vitu visivyo na umuhimu aignore....

Mke ajifunze "kufunga chumba chake"

Awe na heshima....

Tatizo mabinti wanaingia ndoani tayari na vita kwa wakwe na mawifi
Na mawifi kuacha midomo.....mkwe kuheshimu nyumba ya mwanao.....

Mkwe na mke msigombee upendo wa kijana...na kijana ajue nafasi ya kila mmoja na awape uzito unaostahili pamoja na heshima

Lakini kama kuna upendo na kila mtu busy na kuhangaika na maisha yake vita hutokea mara chache... tabu ipo kama mwanaume ndio jicho la familia na mke ni mchoyo
 
Kama kila mtu atajifunza kujali mambo yake na kuheshimu mahusiano ya kindugu na kutambua mipaka yake familia zingekuwa na amani.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom