Namna ya Kuanzisha Biashara Itakayofanikiwa

newazz

JF-Expert Member
Mar 28, 2009
843
780
Nina wazo la kuingia katika biashara ya kusaidia wajasiriamali " Jinsi ya kuendeleza wazo la kibiashara kuwa biashara inayolipa"

Nina lenga kuwafikia wenye mitaji midogo midogo na ambao wanataka kuanza kwa kiwango kidogo.

Je wadau, kuna mawazo yeyote kama watu wanahitaji huduma hii ya biashara?

Asanteni kwa mawazo yetu.
 
Huduma hii inahitajika sana, mimi ni mmoja wa wanaohitaji, lakini unapoanzisha usifanye uhuni kama wa watu wengine ambao wanakuja kuiba mawazo yetu wao wanawaomba watu watume michanganuo , watu wengi wanatuma kisha wanamchagua mmoja na kumpa zawadi huku wakibaki na michanganuo ya watu wengine huo ni uwezi.

anzisha jitangaze tutakuja utusaidie
 
Wapo kibao ndo maana wakaenda deci. je kiwango kidogo ni kipi kwa mtizamo wako?
 
karibu mkuu...ila uwe kweli mshauri ...usijekuwa m-tapeli....kwani biashara inayolipa ni ipi?...msingi/mtaji mdogo kwa mtazamo wako ni kama tshs ngapi kwa kuanzia?....fafanua ili tujadiliane kwa kina zaidi.
 
Newazz,
Nakupongeza kwa moyo wako wa kujitolea kusaidia wafanyabiashara wadogo.
Nimeandika kijitabu kidogo kinaitwa "Mbinu za Ujasiriamali" - unaweza kujifunza mbinu mbalimbali ya kukabiliana na matatizo au vikwazo kwa wale wanopenda kujitumbukiza katika ujasiriamali.
Sijui uko nchi gani, lakini jaribu Mkuki na Nyota Dar es Salaam au ukishindwa tuwasiliane nitakutumia kopi kadhaa.
Kila lakheri.
 
Huduma hii inahitajika sana, mimi ni mmoja wa wanaohitaji, lakini unapoanzisha usifanye uhuni kama wa watu wengine ambao wanakuja kuiba mawazo yetu wao wanawaomba watu watume michanganuo , watu wengi wanatuma kisha wanamchagua mmoja na kumpa zawadi huku wakibaki na michanganuo ya watu wengine huo ni uwezi.

anzisha jitangaze tutakuja utusaidie
Nami nimeishtukia tabia hii, kila mara utaona wakitangazwa kwenye luninga. Wizi mtupu! ...just taking advantage of others. Biashara sio kujifaidisha kwa kumwibia mwingine.

Nawaunga mkono wale wanaoshindanisha watu kwa kutoa mafunzo ya kibiashara pia.
 
Woga lazima uingie kutokana na yanayowakumba wadau wanaosaka pesa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom